Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Kuna jamaa mmoja anayehisiwa anafanya kazi miundombinu jana akiwa maeneo ya Mbezi tangi bovu akipata kinywaji, baada ya kuwa amelewa kidogo alikasirika sana kuwasikia watu wa meza ya pili wakisifia uteuzi wa Magufuli na Mwakyembe kwenda miundombinu anadai tokea Jk alipomteua Magufuli na Mwakyembe kuwa mabosi wao wapya, hali ya hewa siyo nzuri sana pale Wizara ya miundo mbinu kila mtumishi anataka ikiwezekana ahamishiwe wizara ya uchukuzi kuepukana na huyu mtu, wenye uwezo wa ku-robe wameanza kufanya hivyo, wafanyakazi wengi hawajafurahishwa maana walisha wahi kufanya kazi chini ya magufuli hali ilikuwa ngumu sana kimaslahi, wanadai ni mtu anayependa sana sifa kwa kuendekeza zaidi maslahi ya Taifa huku akiwaacha watumishi wakihaha kwa kuwabania mianya ya kujipatia pesa za ziada. Huku akijua fika mishahara ya serikali haiendi na wakati.
Jamaa anasisitiza "Usije ukashangaa ukiona wakandarasi wa barabara wanafunga sana makampuni yao kipindi hiki maana hili eneo litakuwa halilipi kama awali, ukitaka kuamini haya nenda ile wizara ya mifugo na uvuvi uone jinsi wanavyofurahia huyu jamaa kuondoka, mi binafsi simtaki kabisa"
Jamani tujifunze kutokuyazungumzia masuala ya ofisini tukiwa bar, nina uhakika huyu jamaa hatima yake siyo nzuri. maana waliokuwa wanamsikiliza walikuwa wengi.