Magufuli anashinda, sababu 10 ni hizi

Magufuli anashinda, sababu 10 ni hizi

Watanzania wenzangu ikiwa imebaki siku moja tu tukafanye uchaguzi mkuu katika historia ya nchi yetu kuna baadhi ya mambo napenda tujadili kwa sasabbu propaganda katika media na magazeti zimezagaa sana kwamba ukawa wanakura nyingi zaidi ya CCM.

Binafsi sikubaliani na hilo na halina ukweli wowote. ukawa ana mtaji wa kura sana sana kwa vijana tena vijana wa kiume, na tukumbuke kuwa CCM ina vijana wengi sana wa jinsia zote kama mtaji wake, kwa hiyo ukawa wasijihesabie kwamba kura zote za vijana ni zao.

CCM ina mtaji mkubwa wa kura kwa wanawake na watu wazima hasa wanawake ambao ni idadi kubwa sana ya watu katika wapiga kura, tofauti na ukawa ambao mbali na vijana wao ambao asilimia zaidi ya 90 ni wa kiume, ni wanawake wachache sana na wazee wachache katika idadi ya wapiga kura wote ndiyo inayo wasapoti, pia ikumbukwe chama cha act imepunguza idadi ya wanachama kutoka ukawa, lazima ukawa wajue hawana kura zote pia kuna vyama vingine vya siasa.

Kitu cha pili ni kwamba Magufuli amezunguka maeneo mengi zaidi ya Lowassa na amekutana na wapiga kura wengi zaidi , na kafanya mikutano mingi zaidi mijini na vijijini na asilimia zaidi ya 99 amekubalika vikubwa katika mikutano hiyo, tofauti na lowassa ambaye mikutano yake ni mijini tu.

Kwa hiyo suala la ukawa kujihakikishia kura na kudiriki kuaminisha watu kuwa wao lazima washinde ni mbinu ya kujihami tu kwa sababu Magufuli ameonyesha kuwa anakubalika pia kwa asilimia kubwa tu, kwa sababu pia kuna wengi waliohama ukawa na kurudi CCM.

Pia ikumbukwe wapiga kura wengi wa CCM hawabishani mitaani wamekaa kimya wakisubiri mda wa kupiga kura ufike. kwa hiyo ukawa wasitufanye wajinga katuika hili, wajue kuwa Magufuli ana nguvu kubwa na ana watu wengi sana nyuma yake.

UKAWA wasitudanganye, tusimame kwenye uhalisia.
Kama ungekutana na Yesu, angekujibu tu: 'wewe wasema'
 
Nipe majibu
 

Attachments

  • 1445582852739.jpg
    1445582852739.jpg
    64.8 KB · Views: 132
hilo linajulikana mbona bila hata ya ubishi maana mpaka sasa ccm iuna hifadhi ya wanachama zaidi ya mil 8 sasa unategemea unaanzia wapi kuishinda wakati waliojiandikisha kupiga kura ni mil 22 tu ushindi kwa ccm ni lazima tena wa kishindo sana tofauti na mwaka 2010
 
Heshima kwenu wakuu.

Juzi nilkuwa napeleleza mawakala wa Chadema kwenye uchaguzi huu huku jimboni kwangu, cha kuchanganya, Asilimia kubwa ya mawakala hao walikuwa na ni wafuasi watiifu wa DR. Slaa na kwa kipindi kirefu wamejionesha waziwazi kuwa wanamkubali Dr. Magufuli kuliko mgombea wao.

Mawakala hawa kiu na hamu yao ni kumuona Dr.Magufuli akiingia magogoni... Hahaha..patamu hapo...
 
hilo linajulikana mbona bila hata ya ubishi maana mpaka sasa ccm iuna hifadhi ya wanachama zaidi ya mil 8 sasa unategemea unaanzia wapi kuishinda wakati waliojiandikisha kupiga kura ni mil 22 tu ushindi kwa ccm ni lazima tena wa kishiindo sana tofauti na mwaka 2010

Sasa embu tuambie ilikuwaje CCM na Kikwete wakapata kura milioni 5 mwaka 2010 wakati CCM ilikuwa na wanachama zaidi ya milioni 8
 
Nape analalamika chama kinahujumiwa Na kinana Na amechukua mapesa mengi ila hakuna chochote alichofanyia zaidi ya kutusaliti nimemwambia sana jk ila analeta urafiki niwaambie tu hatuwezi kushinda mwaka huu we are finished ,Naye Mkuu wa Mkoa Lindi akamwambia tumewatisha sana vijana ila hawaelewi kuhusu Lowassa ,Nape akajibu sio Lindi tu ni nchi nzima Lowassa sijui kawaroga watz kwa uchawi gani daaah ila yote chanzo kinana Na jk kama angekatwa kihalali yasingetokea haya ila hali mbaya hatushindi kila tunachofanya kinana anatusaliti anatoa nje.

Maneno ya nape leo akiwa hospitali Lindi.

C&P
 
Magufuli lazima ashinde kwa kuwa wapiga kura ni wengi na wako tayari kumfuata Magufuli,kumpa kura na kumsindikiza hadi ikulu ili aweze kuleta maisha bora kwa watanzania
 
Heshima kwenu wakuu.

Juzi nilkuwa napeleleza mawakala wa Chadema kwenye uchaguzi huu huku jimboni kwangu, cha kuchanganya, Asilimia kubwa ya mawakala hao walikuwa na ni wafuasi watiifu wa DR. Slaa na kwa kipindi kirefu wamejionesha waziwazi kuwa wanamkubali Dr. Magufuli kuliko mgombea wao.

Mawakala hawa kiu na hamu yao ni kumuona Dr.Magufuli akiingia magogoni... Hahaha..patamu hapo...

...... ile option ya ku upload video ipo wapi..........
 

Attachments

  • 1445584169346.jpg
    1445584169346.jpg
    21.3 KB · Views: 104
Huo ni uchambuzi Finyu kabisa.
Kwa sababu.

1/Wingi wa mikutano (tena mingi ni mikutano ya kuungauunga barabarani) sio uhakika wa kushinda. Hakuna Prove yoyote katika hiyo. Wakati mwingi kufanya hivyo ni kutafuta ufahamike(kwa vyama vichanga na wagombea wapya) au kutokujiamini(kwa vyama vikubwa na wagombea wanaojulikana) hivyo kiujumla huo mtindo ni kubahatisha(kujaribu jaribu) upepo wa kisiasa.
Kwa mfano Kikwete mwaka 2010 alifanya mikutano ya kampeni mara mbili zaidi ya ile aliyoifanya mwaka 2005 lakini matokeo yalipungua kutoka kura milioni 9 mpaka kura milioni 5.

2/Ushindi wa kisiasa katika dunia ya leo unategemea sana ushawishi katika kundi la vijana kwa sababu vijana wako wengi zaidi na wana ushawishi kwenye jamii. Kwa ujumla vijana wengi pasipo kujali jinsia zao au itikadi zao wanaunga mkono UKAWA.

3/Mtaji mkubwa katika Uchaguzi wowote ule duniani ni AGENDA, MGOMBEA na CHAMA.
Sote tunafahamu kabisa agenda inayozunguzwa zaidi ni MABADILIKO, Mgombea mwenye ushawishi mkubwa zaidi ni LOWASSA. CHADEMA(UKAWA) ndio chama chenye mvuto zaidi kwa sasa, na hilo halina ubishi kabisa.
Kiasili CCM ndio chama kikongwe na kipana sana lakini hapo hapo kiuhalisia kimochoka na kimochokwa sana na wananchi wengi(Ndio maana Magufuli anakwepa kujinadi kama mwanaCCM kwa sababu analijua hilo)

*Kama mtu hujui siasa na falsafa zake ni bora ukakaa kimya huku ukisoma post za watu wengine kuliko kuja kuanzisha Topic ya kuchambua wakati huwezi kuchambua mambo.




Nashukuru post yako inakukosoa, soma ulichoandika, jihurumie
 
Nape analalamika chama kinahujumiwa Na kinana Na amechukua mapesa mengi ila hakuna chochote alichofanyia zaidi ya kutusaliti nimemwambia sana jk ila analeta urafiki niwaambie tu hatuwezi kushinda mwaka huu we are finished ,Naye Mkuu wa Mkoa Lindi akamwambia tumewatisha sana vijana ila hawaelewi kuhusu Lowassa ,Nape akajibu sio Lindi tu ni nchi nzima Lowassa sijui kawaroga watz kwa uchawi gani daaah ila yote chanzo kinana Na jk kama angekatwa kihalali yasingetokea haya ila hali mbaya hatushindi kila tunachofanya kinana anatusaliti anatoa nje.

Maneno ya nape leo akiwa hospitali Lindi.

C&P



Tupe ushahidi
 
Magufuli ni kiongozi mpenda mabadiliko na mwenye dhamira ya dhati yakuwaletea watanzania maendeleo
 
Magufuli magufuli magufuli magufuli magufuli magufuli magufuli magufuli magufuli magufuli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom