watanzania wenzangu ikiwa imebaki siku moja tu tukafanye uchaguzi mkuu katika historia ya nchi yetu kuna baadhi ya mambo napenda tujadili kwa sasabbu propaganda katika media na magazeti zimezagaa sana kwamba ukawa wanakura nyingi zaidi ya ccm.
Binafsi sikubaliani na hilo na halina ukweli wowote. Ukawa ana mtaji wa kura sana sana kwa vijana tena vijana wa kiume, na tukumbuke kuwa ccm ina vijana wengi sana wa jinsia zote kama mtaji wake, kwa hiyo ukawa wasijihesabie kwamba kura zote za vijana ni zao.
Ccm ina mtaji mkubwa wa kura kwa wanawake na watu wazima hasa wanawake ambao ni idadi kubwa sana ya watu katika wapiga kura, tofauti na ukawa ambao mbali na vijana wao ambao asilimia zaidi ya 90 ni wa kiume, ni wanawake wachache sana na wazee wachache katika idadi ya wapiga kura wote ndiyo inayo wasapoti, pia ikumbukwe chama cha act imepunguza idadi ya wanachama kutoka ukawa, lazima ukawa wajue hawana kura zote pia kuna vyama vingine vya siasa.
Kitu cha pili ni kwamba magufuli amezunguka maeneo mengi zaidi ya lowassa na amekutana na wapiga kura wengi zaidi , na kafanya mikutano mingi zaidi mijini na vijijini na asilimia zaidi ya 99 amekubalika vikubwa katika mikutano hiyo, tofauti na lowassa ambaye mikutano yake ni mijini tu.
Kwa hiyo suala la ukawa kujihakikishia kura na kudiriki kuaminisha watu kuwa wao lazima washinde ni mbinu ya kujihami tu kwa sababu magufuli ameonyesha kuwa anakubalika pia kwa asilimia kubwa tu, kwa sababu pia kuna wengi waliohama ukawa na kurudi ccm.
Pia ikumbukwe wapiga kura wengi wa ccm hawabishani mitaani wamekaa kimya wakisubiri mda wa kupiga kura ufike. Kwa hiyo ukawa wasitufanye wajinga katuika hili, wajue kuwa magufuli ana nguvu kubwa na ana watu wengi sana nyuma yake.
Ukawa wasitudanganye, tusimame kwenye uhalisia.