Mimi ki itikadi ni chadema ila kwenye ukweli huwa nasimamia hasa.
Kwanza, asilimia kubwa ya wapiga kura ni wanawake. 58% na katika wanawake hawa 8 au 7 katika kumi wanamuunga mkono. Hii ni tafiti ambayo nimeifanya na sijajua mpaka sasa kwa nini wanawake wengi wanaipenda ccm.
Pili, magufuli amefikia wapiga kura wengi zaidi karibu kila kata tofauti na mzee wetu ambaye kampeni zake nyingi ni sehemu ya mijini.
Record yake ya utendaji ni nzuri ukilinganisha naya lowassa. Mpaka sasa ukweli ni kuwa watu wameichoka ccm lakini wengi wanasema rais nitampa magufuli, mbunge na diwani chadema.
Sababu ya nne, baraka za mwenyezi Mungu. Angalia jinsi alivyo chukua fomu ya ccm, ni mtu ambaye hakutegemewa kushinda kuteuliwa kugombea urais na akaja kushinda ki miujiza. Kwa watu ambao tunajua alama za nyakati na majira na kujua tanzania kwa sasa inaongozwa na Mungu mwenyewe na ni ISRAEL ya sasa duniani na ambako ukombozi wa kiroho umesha anza na kwenda ulimwenguni kote bila shaka huyu jamaa ameteuliwa na Mungu. Na Mungu angekuwa anataka lowassa ashinde asingeacha lowassa akakatwa jina.
Ni kweli ccm imefanya makosa mengi sana kama EPA, escrow ila ifahamike kwamba Mungu huangalia mtu sio chama. Pima hata mwenyewe kwa vigezo vya kibinadamu kati lowasa na magufuli nani anafaa zaidi usipoangalia mambo ya vyama.
Tano, chadema kujichanganya. Hata mkinitukana ila ukweli chadema tulikosea sana kumteua lowassa kugombea urais. Hatukufanya makosa kumpokea, ila angalia hoja ya kukemea ufisadi na utendaji mbovu iliyokuwa inatuvutia wafuasi wengi sasa tumeamua kuiziba. Mpaka sasa watu wanasema haya ni maigizo na kuna wafuasi wengi wa chadema wamesema hawataipigia kura. Ukivunja misingi siku zote mambo huwa yanaharibika. Unathani kwanini sasa hivi ccm wanasema mafisadi waende chadema? Kwa sababu tulishaanza taratibu za kuwapokea. Tumekuwa na haraka sana ya kwenda ikulu na hatujaangalia mbali na uhai wa chama chetu. Hivi unathani lissu, mbowe au lema kwa sasa wanaujasiri wa kukemea ufisadi wakiwa jukwaa moja na lowassa?
Mimi nimemaliza, mkitaka kutana tukaneni, ila msema ukweli ni mpenzi wa Mungu na ukweli huwa unauma. Ni swala la muda tu, vijana wa ukawa sijui watajifichia wapi baada ya matokeo.