Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.
Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.
Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.
Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.
:yield:
CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4
Ulikuwa na mtizamo kama wangu mkuu,nakuunga mkono
Juha aliyekuzaa,kwani hujui kuna wakurugenzi wa idara au mashirika ambao kwao kusafiri njeya nchi ni kama kwenda Kariakoo,najua sababu za kutoa povu ni kwa vile unamchukia Kikwete kwa kumchinjilia mbali jamaa yenu mliyedhani atakuwa raisi,nyumbu juha wewe.tulia juha wewe aliyezurura mara nyingi nje ya nchi zaid ya kikwete ni nani?
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.
Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.
Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.
Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.
:yield:
CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4
Mkuu, Rais Pombe ameshajua nini kinachotakiwa na wananchi wa Tanzania. Alianza kwenye kampeni kwa wimbo wa Chagua CCM/Chagua Magufuli, na utekelezwaji wa ilani ya CCM, akaona hakuna hamasa wala mwitikio, Akabadili Channel akatumia sera za wapinzani na kuiponda Serikali yake ya CCM na udhaifu mkubwa wa kiongozi wake na kwamba yeye atabadilisha hali hiyo, akaona mwitikio wake mkubwa na matumaini kwa wasikilizaji wake na mitandaoni pia, mwanaume akaona mambo si haya bwana! Akakomaa hapo hapo na kuiga kila kitu cha UKAWA na mabadiliko mpaka Nembo yao akitumia akondoa rangi tu na kuweka za magamba, akaitupilia mbali Ilani na hotuba alizoandaliwa akaendelea kuwaeleza watu yale ambyo ndiyo hasa walikuwa wanayategemea kuyasikia toka kwa wagombea, nayo ni mabadiliko; Wapiga kura wakamuelewa na kumchagua.
Sasa katika ufunguzi wa Bunge aliposema kuwa zile ahadi alizokuwa akizitoa za mabadiliko hazikuishia kwenye kampeni tu na ndiyo wakati wake wa kuzitekeleza, asingeweza kubadili maneno yaliyompa ushindi "just" kwa kumpa heshima mtangulizi wake, ingekuwa ni usaliti kwa waliomchagua. Kulikuwa hakuna namna nyingine kwa pale jana zaidi ya kuendeleza pale alipoachia kampeni zilipokoma. Na alichosema ndiyo ukweli mtupu. Kama JK aliona anadhalilishwa kwa hotuba ile angefanya mambo mawili: Angesimama akabisha na kupiga kelele AU angewafuata Ukawa kule nje akawaambie hata yeye ametoka huko ndani hakufai.
kwa sasa akubali tu kuwa ule wakati wa kusikilizwa yeye tu na kupigiwa vigelegele na wale wazee wa Dar es Salaam
hata anapotetea hadharani mambo ya wazi kama Escrow pale Diamond, yamekwisha.
Aliye madarakani ndiye JP Magufuli na si vinginevyo, na ana deni la ahadi alizowapa waTanzania ambazo ili azitekeleze lazima awe na uso wa mbuzi na asijali ka kuna wastaafu wanaokerwa na utekelezaji/utimizwaji wa ahadi hizo.
Mzee Ruksa alishasema kuwa " KILA NABII NA WAKATI WAKE", Kama JK hakumsikia angemuuliza maana walikuwepo pale wote watatu.
BIG UP MY PRESIDENT, YESTERDAY WAS YOUR DAY TO DISTANCE YOUR SELF FROM THE GRIP OF THE RETIRED TRIO.
Mkuu sikumbuki kama Dk.Magufuli alitaja majina,alizungumzia Wizara zinazo ongoza kwa safari za kwenda nje - hapo kamdhalalalisha nani?mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!
mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!
Mimi mwenzenu kama ni mwenzenu nashindwa kuelewa kama serikali ni mali ya Magufuli, ya CCM au ya wananchi. Maana tulitemwajiri hashirikishi hata ubongo wake, chama chake wala sisi wapiga kura tumekuwa watu wakusubiri huruma za mtu mwenye uraisi.
Hii ni mpya nasubiri kuona kitatokea nini mbele ya safari. Hi ni dhahiri kwa kauli anazotoa kana kwamba hapajawahi kuwa na serikali makini kabla yake. Wala hapajawahi kuwa na mihili mitatu kama wengine tunavyojua.
Ukweli, Mzee Kikwete alipewa za uso hadi aibu!
Mkuu utakuwa umemsoma jamaa vibaya. Soma vizuri post yake. Kwa upande wangu nachokiona ndani ya post hii ni kufurahia kitendo cha Kikwete kuvuliwa nguo na Mzee wa Hamnazo.We ni mpuuzi na kigeugeu.
Watu tumechoka na uozo ulioko serikalini tunataka mabadiliko we unaleta za kuleta.
Ulikuwa ni mmoja wa watu waliomkandia sana JK kwa michemsho yake hapa JF.
Sasa ulitaka JPM asifie?
Alishamsifu kwa mazuri yake mkamtukana..sasa ni wakati wa kurekebisha na kuzoa uozo uliolitrsa taifa we unaleta propaganda.
Watu wa aina yako hawana jema.
mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!