Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Acha waisome namba CCM....but remember we won't call a spade as a big Spoon, but we will call a spade as spade not a big spoon. tpaul
 
Last edited by a moderator:
magufuli aache kutafuta sifa za kijinga.alimchana live rais mstaafu,mpedwa wetu sana, mzee jakaya kikwete wa msoga,kwa kuwa tu ni muislamu. CC FaizaFoxy

Wacha ufataani.

Hivi we dada Kadoda una miaka mingapi? unaonesha bado u mwari.
 
Kikwete ngoma nzito ile hamuiwezi.

Nasikia ardhi ya Mvomero na Monduli inarudishwa Serikalini, unayajuwa hayo?
 
Tunamwombe Rais wetu apate pia ujasiri wa kutatua mgogoro wa uchaguzi 2015 Zanzibar kwa utamletea heshima kwa wanaichi na dunia kwa ujumla.Damu yamwanadamu inathamani kubwa mbele za Mungu.
 
Huyo ndio binadamu..Haridhiki! Ukiwa mkimya wanasema...Ukikemea wanasema! Kweli uongozi si lelemama.
 
Ameshasema yeye si mnafiki,mtaka awe mnafiki kama ccm walio wengi?acha afanye kazi kama amekuudhi hama nchi.
 
Ni bora ukalitoa la moyoni lisijelipuka ndan kwa ndan.......ukiwa na roho ya kinafiki unakuwa muoga xana....
 
Tunamwombe Rais wetu apate pia ujasiri wa kutatua mgogoro wa uchaguzi 2015 Zanzibar kwa utamletea heshima kwa wanaichi na dunia kwa ujumla.Damu yamwanadamu inathamani kubwa mbele za Mungu.

Hapo hawezi kupagusa ni mpango wao wote. Lakini nimemuona Magufuli akiwagusa zaidi ndani ya UTAWALA KULIKO HATA HAO UKAWA !!!
 
Mleta mada hajitambui au ni mmoja kati ya wanaosafiri zaidi ya kwenda kusalimia wazazi wake.
 
Nashindwa kuamini kwanini huoni anabadili mfumo kwa kurekebisha utendaji. Sioni kamsema kiongozi mwenzie yeyote bali ameona tatizo lilipo na anania ya kulitatua. Sisi tunayefikiri kamsema huyu kamvua huyo ndio wenye matatizo maana hata hao wanaosemwa kama wapo wanacheka na kufurahi maana waungwana wanarekebishana na maisha yanaendelea tatizo lipo kwenu mlio zoea viongozi miungu watu. Wacha uchochezi jenga umoja na upendo usiuze tindikali ya moyoni mwako kwenye nchi wewe peleka CHADOMO
 
Kikwete ngoma nzito ile hamuiwezi.

Nasikia ardhi ya Mvomero na Monduli inarudishwa Serikalini, unayajuwa hayo?

nani ngoma nzito wewe bibi? kikwete au jpm? acha kushabikia udhalilishaji ushakuwa mkubwa wewe!

kama vile tyson hawezi kujizolea umaarufu kwa kumchapa matumla, vivyo jpm asitafute kiki kupitia udhaifu wa kikwete.
 
kuna baadhi ya watu humu ni wabishi kuliko wabishi....hebu tazama hii video hapa chini halafu uniambie kama alichokifanya magufuli ni sahihi kwa watangulizi wake.


Hivi ndivyo Magufuli alivyo ‘msasambua' Kikwete Hadharani.

ninachotaka kusema ni kwamba kufeli kwa serikali ya kikwete kumechangiwa na mawaziri kama magufuli ambao wakati rais anatalii duniani walisimama mstari wa mbele kumtetea. sasa iweje leo jk aonekana mbaya kwa mtu huyohuyo aliyekuwa akimkubali wakati wa uongozi wake? acheni unafiki jamani, sio vizuri hata kidogo.

http://www.ippmedia.com/?l=86362
 
Do not afraid for the changes, accept it and find the way to coup with it--Magufuli kila la kheri tulio wengi tunakuunga mkono
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo.

Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana.

Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile.

Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

Acha uzembe ww hii siyo dunia ya kuogopana ivo......ww ni mtumwa wwkuwa hiru wacha raisi afanye kazi yake
 
mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!

Mmeanza kuisoma namba!! enzi zenu zimepita! fanya kazi acha majungu, raisi wetu yuko sahihi au ulizoea vicheko na tabasamu za kinafiki? HAPA KAZI TU! ukitaka kubembelezwa nenda .......! hahaha
 
Watanzania hamueleweki? Mnalalama matumizi ya serikali makubwa halafu Kaja mtu msema kweli anaguza maeneo ya kuthibiti na Anglia tena Huyu mleta Uzi anasema nini. Nahisi huyu bwana Ana bifu n.a. Magufuli n.a. atapinga chochote atakachokifanya. Poor you.

achana nao kaka hao wanafiki hao kaka wanatuakfa cjui mtu gaani
 
Back
Top Bottom