Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 217
- 860
Akizungumzia sifa za mtu kuteuliwa kuwa balozi nchini Tanzania, mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia (Dr. Salim Ahmed Salim Centre for Foreign Relations) na mchambuzi wa masuala ya uhusiano wa kimataifa, Dennis Konga amesema hakuna vigezo ambavyo vimewekwa rasmi vinavyotumika kumteua mtu kuwa balozi, lakini kuna vile vinavyoangaliwa na hapo kuna njia mbili.
“Kwanza kuna wale walioko kwenye mserereko (carrier diplomats), yaani wale wanaoanzia ngazi za chini mpaka wanafikia kuwa waandamizi, ambapo sasa wanaweza kuteuliwa.
“Kumbuka mteuzi ni Rais tu kwa sababu hao wanakwenda kufanya kazi kwa niaba ya Rais, sana sana atashauriana na waziri wa Mambo ya Nje au atashauriana na Waziri Mkuu, kuona nani atafaa katika hao kutegemea na mahitaji ya wakati huo,” amesema.
Ametaja kundi la pili la wanaoteuliwa, akisema ni kutegemea na mahitaji ya wakati uliopo.
“Kwa mfano mtu anateuliwa kuwa balozi kumwakilisha rais katika jambo fulani. Wengine wanapewa kwa sababu ni hadhi na haiondolewi mpaka yule aliyempa atakapomwondolea. Mfano wa karibuni ni Humphrey Polepole na wengineo. Tunao mabalozi ambao wanakuwa kwenye upande wa afya, uchumi, kutegeea na hali ilivyo,” amesema.
Mbali na njia hizo mbili, Konga amesema huwa kunakuwa na mwelekeo wa kulinda utendaji wa nafasi za viongozi wanaoteuliwa.
“Mfano, wa hivi karibuni ni pale Jenerali Jacob Mkunda alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ilibidi yule aliyekuwa akimfuata aliyekuwa mkuu wa majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, akateuliwa kuwa balozi ili kumwondolea sinikizo Jenerali Mkunda katika utendaji wake.
“Hiyo ilitokea pia wakati wa Mwalimu Julius Nyerere alipomteua aliyekuwa mkuu wa Majeshi, Meja Jenerali Mrisho Sarakikya kuwa Balozi ili kumwondolea shinikizo alitepandishwa badala yake,” amesema.
Sababu nyingine za uteuzi kwa mujibu wa Konga ni kuangalia matakwa ya Serikali na chama, ili kuepusha wwatu wenye nguvu ndani ya Serikali na chama tawala kutoathiri viongozi waliopo madarakani.
“Unajua kuna watu wengine wanakuwa na nguvu kubwa kwenye Serikali na chama, sasa mtu anapoingia madarakani anajaribu kujitengenezea himaya bila kuingiliwa. Kwa mfano kuna suala la Makamu wa Rais, Balozi Emmanuel Nchimbi ambaye aliteuliwa (na Hayati Rais John Magufuli) kuwa balozi na akapelekwa Brazili, kwa sababu alionekana kuwa na nguvu kwenye chama,” amesema.
Ametaja sababu nyingine kuwa ni watawala kulipa fadhila kwa watu wake wa karibu kwa kuwapa hizo nafasi.
Nyingine anasema ni ni kuwa na ukaribu na mteuzi, pia inaweza kuwa sababu.
“Kwa muktadha wa Tanzania, unaweza kusema ni adhabu, lakini kikubwa inakuwa ni kulinda sura aliyonayo anayeteuliwa na kufanya mambo yaendelee ili asiweze kuharibu utaratibu wa kiserikali uliopo. Nachelea kusema ni adhabu, bali ni kutengeneza dhima mpya ya Serikali iliyopo,” amesema.
Kwa njia zote hizo, Konga anaona njia salama ni ile ya kuwatumia carrier diplomats kwa sababu wao ni wana diplomasia wana makuzi hayo.
“Hata hivyo, sio kila mtu anaweza kuteuliwa kutoka kwenye kundi hilo, pengine kutokana na mahitaji ya wakati. Kwa mfano, kwenye carrier diplomat ana sifa za kuwa Balozi, lakini ile nchi anayotakiwa kupelekwa, kuna mtu mwingine ana ujuzi katika jambo Fulani, kwa mfano eneo la uchumi, kwa hiyo tunapeleka mtu mwenye uzoefu na uchumi ili aweze kusaidia. Kwa hiyo uandamizi pekee unaweza usitoshe kuteuliwa.”