Watanzania wenzangu, taarifa kutolewa sio kitu cha ajabu, tatizo ni ubora, utaratibu, na hata uzito/umuhimu wa jambo lenyewe kwa wakati huu tulionao. Yako maswali mengi ya kujiuliza juu ya taarifa iliyotolewa na TFDA. Nayo ni kama yafuatayo;
1. Je Utafiti huu umefanyika mara ngapi na ulianza lini?
2. Ni watu wangapi wamefanyiwa uchunguzi na hata kuonekana kwamba wameathirika kwa kutumia mafuta ya UBUYU?
3. Je Mafuta ya ubuyu yanaathari sawa na Uvutaji wa Sigara?
4. Kama sigara inaathari na hata katika mango yao chini kabisa kwa maandishi maadogo yanasomeka, Onyo UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO kwanini sasa bado iko sokoni inauzwa?
5. Na kwanini mpaka sasa mali ghafi yake(Tumbaku) bado inalimwa?
6. Je nyuma ya taarifa hii kuna mgongo wa mafisadi na matajiri wakubwa Tanzania?
7. Kama ni mafisadi/ matajiri wakubwa nia yao hasa nini ktk bidhaa hii iliyopata saoko kubwa ndani ya Tanzania
8. Kwanini hawakuwakusanya wajasiriamali wote kwa pamoja na kuwapa taarifa mapema kabla ya Sabasaba?
9. Je sabasaba ndio mahali pekee pa kusemea habari za afya ya mwanadamu?
10. Kama sabasaba isingekuwepo taarifa hizi zingetolewa wapi na kwa wakati gani?
11. Je historia inasemaje juu ya utumiaji wa Ubuyu kuanzia unga, majani yake, magome, mizizi na hata kiini chake?
12. Je historia inaonyesha watu wangapi wameshawahi kupimwa na kukutwa na saratani na hata kufariki kwa sababu ya utumiajia wa bidhaa hii?
13. Je kiwango gani cha mafuta mtu akinywa atakuwa katika hatari ya kupata maradhi hayo?
14. Je Tone moja? kijiko kimoja? Robo lita? Nusu lita?
15. kunywa mafuta haya kwa wingi uko hatarini kupata saratani za aina nyingi, Nyingi maana yake nini? na hizo nyingi ni zipi?
16. Kama ukitumia kidogo na si kwa wingi hautapata kabisa saratani au utapata je ni aina gani ya saratani?
15. Afya ya mwanadamu ni ya kungojea tukio maalumu au huku ni kuchezea uhai wa mwanadamu kwa kusubili matukio ndo jambo litangazwe?
Yako maswali mengi ya kujiuliza hayo ni machache tu kwa wakati huu. Nawasilisha.