Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,912
- 16,519
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji Ardhini (LATRA), Habibu Suluo, amesema kuwa kupanda kwa bei ya Mafuta ya sasa haiathiri nauli hivyo nauli zitaendelea kubaki vile vile.
Suluo ameongeza kuwa nauli zinaweza kupandishwa ikiwa bei ya Mafuta itapanda kwa kiwango kikubwa, ambapo wametoa siku 14 kupokea maoni ya wadau kuhusu mapendekezo ya mapitio ya nauli.
Aidha amesema kuwa mpaka kufika jana, April 7, 2026, hawajapokea maombi yoyote rasmi kutoka kwa wadau kuhusu kupandishwa kwa nauli.
Suluo amesema hayo Leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa kusikiliza maoni ya wadau kuhusu hatua zinazochukuliwa kufuatia mabadiliko ya bei ya Mafuta yanayotumika katika huduma za usafiri wa umma kwa njia ya barabara.
Anaongeza kuwa kutokana na taarifa za leo kuhusu kushuka kwa bei ya Mafuta duniani, baada ya Marekani na Irani kukubaliana kusitisha vita, kuna uwezekano wa kupungua kwa gharama za mafuta zinazotumika kushuka na kuwaomba wadau hao kuwa wavumilivu wakati wakifanyia kazi mapendekezo yao watayoyapeleka.
"Kazi yetu kama Serikali ni kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri na rafiki kwa sekta ya usafiri nchini na hatuwezi kupandisha bei ya nauli ghafla kupitia hiki kikao bila kuangalia kikotoo hivyo niwaombe kwa siku hizi 14 leteni maoni yenu tukae tujadili kwa pamoja na si kupanisha nauli ghafla bila kuzingatia kanuni na taratibu "Amesema Suluo
"Huduma zinazodhibitiwa na LATRA zinagusa maisha ya wananchi wengi, hivyo ni muhimu maamuzi yote kuhusu nauli yafanywe kwa umakini na kwa kuzingatia maslahi mapana ya umma."ameongeza
Awali, akifungua mkutano huo, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Barabara kutoka Wizara ya Uchukuzi, Andrew Magombana, anaeleza kuwa kupanda kwa bei ya mafuta kumeathiri kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji wa huduma za usafiri. Anaongeza kuwa tangu Desemba 8, bei ya dizeli ilikuwa Shilingi 3,358 kwa Dar es Salaam na Shilingi 3,556 kwa Mtwara, jambo ambalo limeongeza mzigo kwa watoa huduma za usafiri wa umma.
Chanzo: Kitenge TV