Mafuta ya ubuyu hatari kwa afya

Mafuta ya ubuyu hatari kwa afya

Mafuta ya Ubuyu ambayo yamejitwalia umaarufu siku za karibuni kiasi cha kufanya yawe ya bei mbaya sana yameelezwa kuwa si salama kwa afya..

TFDA wamepiga marufuku kwa kuwa yana Tindikali ya mafuta, na anayekunywa kwa wingi ana hatari ya kupata Kansa za aina mbali mbali.

TDFA inaonya jamii kuwa mafuta hayo si mazuri na si salama na inashauri watanzania kuacha kutumia.

HABARI KAMILI HII HAPA KUTOKA HABARI LEO

Imechapishwa Jumatatu, 08 Julai 2013 | Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko

BAADA ya kuonya wananchi wanaotumia dawa za tiba mbadala ambazo hazijathibitishwa, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), sasa inawataka wananchi kuacha kutumia mafuta ya ubuyu kwa kunywa kama dawa.

Akizungumza na gazeti hili juzi katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema Mamlaka hiyo ilipima na kubaini mafuta hayo yana tindikali ya mafuta.

Alifafanua katika maonesho hayo maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, kwamba mafuta hayo hayafai kuliwa na binadamu na anayekunywa kwa wingi, yuko hatarini kupata saratani za aina tofauti tofauti.

“Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wajasiriamali wanaouza mafuta ya ubuyu kama dawa, kwa kuwaelekeza wananchi kunywa. Napenda kuwataarifu kuwa mafuta hayo ni hatari kwani yana tindikali ya mafuta,” alisema.

Gazeti hili lilipata sampuli ya vielelezo vya matumizi yake na manufaa yake mwilini, kama inayotangazwa na wajasiriamali katika maeneo mbalimbali na hata katika mitandao.

Matangazo

“Ni mafuta yatokanayo na mbegu za ubuyu {au kokwa}. Hukamuliwa kiini chake na kutoa mafuta. Yana ubora kuliko mafuta mengine ya kupikia, yana Vitamin A, B, C, D na F. Pia yanatibu magonjwa mbalimbali,” kielelezo kimoja kilinadi ubora wake katika mitandao ya jamii.

Mafuta hayo yamedaiwa kutengeneza seli zote ndani ya mwili, kuzuia ngozi isiharibike wala kupata makunyanzi, kuondoa mafuta ndani ya mishipa ya damu na yanapunguza uzito uliozidi.

Pia inadaiwa yanarutubisha ini na figo, yanaleta hamu ya kula, yanaimarisha mifupa, kucha na nywele, yanaongeza kinga ya mwili (CD4), yanaondoa sumu na yanatengeneza sukari iwe katika kiwango kinachotakiwa.

Maelezo hayo yameendelea kusifu kwamba yanasaidia kuona vizuri na kujenga kumbukumbu, yanapunguza vitambi na matumbo makubwa, yana virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini.

Katika ngozi yametajwa kuondoa madoa, chunusi, fangasi, upele, mba na muwasho, yanafaa kwa walemavu wa ngozi (albino). Pia huondoa hamu ya kutumia dawa za kulevya na kuponyesha vidonda vya tumbo.

“Endelea kutumia mafuta bora ya ubuyu, ni bidhaa asilia ya kitanzania. Ni mafuta yasiyochanganywa na kitu chochote, ni mafuta asilia,” yamesifiwa katika maelezo hayo.

Kisukari

Mtumiaji ameelezwa kama ana ugonjwa wa kisukari, atumie kijiko cha chakula kimoja tu. Anatakiwa kutumia dozi hiyo ya kwanza nusu saa kabla ya kula chochote kwa muda wa siku 15.

Dozi ya pili na ya tatu kwa wagonjwa hao, inatakiwa kufuata baada ya siku 15 kisha mgonjwa apumzike wiki moja, huku akiendelea kupima kila wiki. Kipimo hapo ni cha hospitali.

Vidonda vya tumbo, figo, ini

Kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo, figo na ini, wameelekezwa na wajasiriamali hao kunywa kijiko cha chakula kimoja asubuhi kabla ya kula chochote, na usiku kijiko cha chakula kimoja kabla hajala chochote kwa muda wa siku 15 kwa dozi ya kwanza.

Baada ya hapo, mgonjwa anapumzika wiki moja kisha siku 15 zinazofuata dozi ya pili, mapumziko wiki moja halafu siku 15 nyingine dozi ya tatu.

Maelezo ya dozi hiyo ya kutibu ugonjwa wa vidonda vya tumbo, yanaendelea kumtaka mgonjwa baada ya dozi ya tatu, aanze kunywa kila wiki mara moja kijiko cha chakula kimoja asubuhi, tena nusu saa kabla hajala chochote kwa muda wa wiki nne.

Dozi inaendelea ambapo mgonjwa atatakiwa kunywa kijiko kimoja cha chakula kila mwezi mara moja asubuhi, kabla hajala chochote kwa muda wa wiki nne, kisha kunywa kila mwezi mara moja, asubihi kabla hajala chochote kwa muda wa miezi sita mfululizo.

Utoaji sumu, CD4

Kwa utoaji wa sumu, mgonjwa ametakiwa kunywa kijiko cha chakula kimoja asubuhi kila siku kwa muda wa siku 14, kisha kunywa kila mwezi mara moja kwa muda wa miezi sita mfululizo.

Kwa kuongeza CD4 mwilini, ametakiwa kupata kijiko cha chakula kimoja asubuhi nusu saa kabla ya kula chochote, na usiku kijiko cha chakula kimoja nusu saa kabla ya kula chakula cha usiku kwa muda wa miezi mitatu.

“Mgonjwa aanze kunywa baada ya kipimo cha mwisho (cha CD4) alichopima. Mafuta yanapatikana kuanzia ujazo wa lita moja na zaidi,” imesifiwa dawa hiyo.

Onyo

TFDA imeonya kuibuka kwa tabia ya wananchi kutaka matibabu ya haraka, kama ilivyo kwa baadhi ya watu kutaka utajiri wa haraka, na imehadharisha ni vema kabla ya kutumia dawa zinazoibuka kila siku, waulize kama zina ubora kwa afya zao.

“Nawasihi wananchi kuacha kukimbilia dawa ngeni mara tu baada ya kutangazwa… kama haya Mafuta ya Ubuyu, yamekuwa yakielezwa ni dawa na wajasiriamali tu, na wengi wamekuwa wakitumia bila kusikiliza mamlaka husika zinasemaje,” alisisitiza.

Semwanza alisema Mamlaka hiyo iko katika mkakati wa kuanza kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya mafuta hayo, ambayo wengi wanayaamini na kuyanywa kama dawa.

Teknolojia, matumizi sahihi

Kwa mujibu wa Semwanza, baada ya kupima mafuta hayo na kubaini hatari hiyo, waligundua pia inawezekana tindikali hiyo kutenganishwa na mafuta hayo, lakini imebainika utaalamu na teknolojia hiyo haipo nchini.

Hata hivyo, alisema Mamlaka hiyo haijabaini madhara ya matumizi mengine ya mafuta hayo kama kipodozi.

Msako Sabasaba

Kutokana na mvuto huo wa kibiashara, na shauku ya kupona haraka ya wananchi, Semwanza alisema TFDA imekuwa ikifanya msako wa dawa mbalimbali zinaouzwa na wajasiriamali katika maonesho hayo.

Alisema kuwa kuna baadhi ya waandaaji wanaowaalika wajasiriamali bila kufuata kanuni na sheria za kuingiza dawa hizo katika maonesho.

Kwa mujibu wa Semwanza, wanakagua dawa na kama wakikuta hazijathibitishwa na TFDA na mamlaka nyingine, wanamuamuru mjasiriamali kuacha kuzitangaza mpaka apate kibali na kuwaasa wanaowaleta wajasiriamali katika maonesho hayo ya kimataifa kuhakikisha wanafuata vigezo.

Wiki iliyopita TFDA, ilionya wananchi dhidi ya matumizi ya dawa za tiba mbadala, zikiwamo zinazokuza maumbile, ambazo bado hazijasajiliwa na Mamlaka hiyo baada ya kuchunguza usalama, ubora na ufanisi wa dawa hizo.

Mamlaka hiyo ilieleza kuwa, ilitoa nafasi ya watoa tiba mbadala kwenda kusajili dawa zao, lakini mwitiko umekuwa hafifu.

TDFA yenye dhamana ya kusimamia ubora na usalama wa bidhaa za vyakula na dawa, ikiwa ni pamoja na dawa za mitishamba, vipodozi na vifaa tiba vinavyouzwa katika soko la Tanzania, imeeleza kuwa watoa huduma wa tiba mbadala, wengi hawako tayari kubainisha aina ya mchanganyiko wa dawa hizo jambo ambalo ni hatari kwa walaji.

Duh! Ahsante kwa kutupa taarifa, Yatupasa tujue kuwa si kila kitangazwacho uzuri wake kwa matumizi ya binadamu/mifugo ni salama: ushauri: kabla hujakitumia ama kukinunua tafiti athari zake kabla, tambua yote haya yanatokana na ugumu wa maisha, watu wanajiingiza kutafuta bidhaa ambazo hazina usalama kwa mtumiaji ili tu siku ipite,(madhara ya ukosefu wa ajira) si kila ubunifu una maana, mwingine ni hasara tupu, tuwe makin watanzania, vingi vitakuja si mafuta ya ubuyu pekee, wimbi la wizi linaongezeka! Huu ni wizi jpo c wa mfukon!
 
Binafsi nshajiwekea utaratibu wa kutokurupukia mambo mageni. Kwenye nchi zetu hizi ambazo kila anasaka hela kwa njia yake kukiwa hakuna tecnologia au vyombo dhabiti vya udhibiti ni busara kujenga tabia ya mashaka. mara ngapi vitu vinaingia nchini vinatumika weee then tunatangaziwa havifai. Bora nkamsikilize bibi ni chukuchuku kwenda mbele.
 
Watanzania wenzangu, taarifa kutolewa sio kitu cha ajabu, tatizo ni ubora, utaratibu, na hata uzito/umuhimu wa jambo lenyewe kwa wakati huu tulionao. Yako maswali mengi ya kujiuliza juu ya taarifa iliyotolewa na TFDA. Nayo ni kama yafuatayo;
1. Je Utafiti huu umefanyika mara ngapi na ulianza lini?
2. Ni watu wangapi wamefanyiwa uchunguzi na hata kuonekana kwamba wameathirika kwa kutumia mafuta ya UBUYU?
3. Je Mafuta ya ubuyu yanaathari sawa na Uvutaji wa Sigara?
4. Kama sigara inaathari na hata katika mango yao chini kabisa kwa maandishi maadogo yanasomeka, Onyo UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO kwanini sasa bado iko sokoni inauzwa?
5. Na kwanini mpaka sasa mali ghafi yake(Tumbaku) bado inalimwa?
6. Je nyuma ya taarifa hii kuna mgongo wa mafisadi na matajiri wakubwa Tanzania?
7. Kama ni mafisadi/ matajiri wakubwa nia yao hasa nini ktk bidhaa hii iliyopata saoko kubwa ndani ya Tanzania
8. Kwanini hawakuwakusanya wajasiriamali wote kwa pamoja na kuwapa taarifa mapema kabla ya Sabasaba?
9. Je sabasaba ndio mahali pekee pa kusemea habari za afya ya mwanadamu?
10. Kama sabasaba isingekuwepo taarifa hizi zingetolewa wapi na kwa wakati gani?
11. Je historia inasemaje juu ya utumiaji wa Ubuyu kuanzia unga, majani yake, magome, mizizi na hata kiini chake?
12. Je historia inaonyesha watu wangapi wameshawahi kupimwa na kukutwa na saratani na hata kufariki kwa sababu ya utumiajia wa bidhaa hii?
13. Je kiwango gani cha mafuta mtu akinywa atakuwa katika hatari ya kupata maradhi hayo?
14. Je Tone moja? kijiko kimoja? Robo lita? Nusu lita?
15. kunywa mafuta haya kwa wingi uko hatarini kupata saratani za aina nyingi, Nyingi maana yake nini? na hizo nyingi ni zipi?
16. Kama ukitumia kidogo na si kwa wingi hautapata kabisa saratani au utapata je ni aina gani ya saratani?
15. Afya ya mwanadamu ni ya kungojea tukio maalumu au huku ni kuchezea uhai wa mwanadamu kwa kusubili matukio ndo jambo litangazwe?
Yako maswali mengi ya kujiuliza hayo ni machache tu kwa wakati huu. Nawasilisha.
Maswali haya haya na wajasiliamali wa ubuyu nao wayajibu.
 
binadamu wasichanganye kati ya ubuyu na mbegu ya ubuyu,,kitu chochote kinachotokana na ubuyu hakina mathara,,lakini bidhaaa zote zitokanazo na mbegu ya ubuyu sio nzuri kwa afya hasahasa zinazotumika kama tiba ndani ya mwili,,,,mafuta ya ubuyu yana tindikali ijulikanayo kama fat acid au tindikali huru inayoweza kusabababisha saratani tofauti tofauti katika mwili wa binadamu ,,,ambayo kiwango chake nikati ya 12-14,,wakati mwili wa binadamu unatakiwa kuwa tindikali ya mafuta(fat acid) isyo zidi 0.4,,,,teknolojia inayoweza kupunguza tindikali hiyo ni hydrogenation,,ni teknolojia ya kiwandani ambayo tanzania haijafika ,,inauwezo wakuondoa hiyo tindikali kwa asilimia 94,,lakini kuna njia nyingine yakaiwaida,,,,unatakiwa kuyachemsha mafuta ya ubuyu kwa joto nyuzi joto 180 kwa masaa 8,,na ufanisi wake ni asilimia 54,,,ambayo bado ni ndogo sana,,,kwa utafiti uliofanyika mpaka sasa,,mafuta ya ubuyu si salama kabisa,,,,kama ni barafu za ubuyu we bugia,,,,kama ni juice we kamua,,lakini mafuta acha kabisa mpaka tfda,,itakapotoa ruksa
onyo: Mafuta ya ubuyu ni athari kwa afya yako
 
TANZANIA KILA KITU KINAWEZEKANA. MBINU YA KIBIASHARA PIA INAWEZEKANA. KWA MTINDO HUU, HEBU TUPEWE TAARIFA ZA MIMEA YOTE AMBAYO NI HATARI, MIMEA NI MINGI INATUMIKA, WATUAMBIE WAMEGUNDUA MINGAPI NA INA MADHARA KIASI GANI. MAANA KAMA MMEA HUO UNA MADHARA BASI NA MIMEA MINGINE PIA KUNA KITU HATUFAHAMU. why ubuyu,why today, kiwango gani cha sumu WASEME KILA KITU, VINGINEVYO TANZANIA NI USANII MWINGI, usikute dispensaries au mafuta fulani wateja wameanza kupungua.
 
Hao nimafisadi wanataka kufisadi hadi uhai wamtu eti salatani nyingi nyingi gan? "HUWO NI MKONO WA MTU"
 
No research no right to talk,TFDA wamekurupuka bila kujiridhisha jambo linalozua maswali mengi,wafanye tafiti washirikiane na taasisi nyingine,vyuo na hata wataalam binafsi ndipo watueleze wananchi taarifa inayojitosheleza,mlikua wapi?
 
Wapendwa Wazalendo mimi nachosema ni Hiki: BORA NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI, hivi madawa ya Viwandani ni salama sana kuliko yetu ya asili? Watanzania lazima tufunguke macho na masikio kwani madawa ya asili ni bora kuliko hayo ya viwandani ambapo wengi wa watengenezaji wamekuwa si wa kweli sana, kwa mfano wanachanganya madawa yao na vifaa vingine lwa maana materials ili kupata wingi wa madawa wakati wanazalisha, matokeo yake ni kuwanywesha watu madawa ambayo hayana viwango, lakini ikumbukwe kuwa hata KIJIKO cha chakula nyumbani huwa kinafika mahala kinakuwa kimelika kiasi kwamba inabidi kinunuliwe kipya, kwa kifupi mashine za viwandani zinazotumia vyuma husagika na kuleta madhara makubwa kiafya, hicho chaweza kuwa ni moja ya vyanzo vya saratani, sasa ni bora kutumia miti shamba yetu kuliko madawa yenye sumu ya viwandani ikiwemo unga vyuma!!!! TFDA waeleze ukweli na siyo kuzuia tu!
 
...hao watafiti wangekuja huku kwetu Mongowamono watutafiti kama tuna kansa.....kweli mkuu hao ni WAZUSHI TU...

Mkuu Earthmover, on a serious note,unayosema ni kweli ? kuwa hizi mbegu wapo watu wamekuwa na wanaendeela kuzitumia tangu enzi na enzi bila madhara yoyote?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Earthmover, on a serious note,unayosema ni kweli ? kuwa hizi mbegu wapo watu wamekuwa na wanaendeela kuzitumia tangu enzi na enzi bila madhara yoyote?

.....Mkuu kweli sikudanganyi ...kuna bonde liko Mbulu ....linaitwa YAEDA CHINI...huko wanaishi Wahadzabe na Waman'gati ....wahadzabe hutumia mbegu za mbuyu kwa kuzisaga na mawe kuwa unga unga na kuzichaganya na maji na kuzinywa.......miaka mingi tuu... hata mimi nilikuwa huko kwa maswala ya utafiti wa mimiea!!!
 
.....Mkuu kweli sikudanganyi ...kuna bonde liko Mbulu ....linaitwa YAEDA CHINI...huko wanaishi Wahadzabe na Waman'gati ....wahadzabe hutumia mbegu za mbuyu kwa kuzisaga na mawe kuwa unga unga na kuzichaganya na maji na kuzinywa.......miaka mingi tuu... hata mimi nilikuwa huko kwa maswala ya utafiti wa mimiea!!!

Mkuu, asante kwa taarifa hii. Mi naona hawa TDFA hawana uhakika na wanachokisema...
 
Wakuu hili ni jambo la kushangaza sana.

Tukiwa wadogo, tulipokuwa tunakwenda na kurudi shule darasa la kwanza hadi la Saba, njiani tunapita miti mingi sana ya ubuyu na tulikuwa tunakula kwa fujo, kwa ile mibuyu michanga mbegu zake ni laini na tulikuwa tunazitafuna na kumeza, hii ni kwa muda mrefu sana na hatujapata madhara yeyote, upo ushahidi, wengine ni viongozi wastaafu. Hii habari inashitua inahitaji utafiti wa kina.
 
Kama mambo ndio haya walalahoi hatuponi kwamfano mimi nalala kwenye chandarua kilichowekwa ngao lakini hipiti miezi 4 naugua malaria sasa net ya ngao ni ya nini? Huo nimpango wa kupunguza wtu duniani.tungewaona wa maana wangeleta madawa ya kuangamiza mazalia ya mbu na sio net madawa fake ya malari.
 
Kama mambo ndio haya walalahoi hatuponi kwamfano mimi nalala kwenye chandarua kilichowekwa ngao lakini hipiti miezi 4 naugua malaria sasa net ya ngao ni ya nini? Huo nimpango wa kupunguza wtu duniani.tungewaona wa maana wangeleta madawa ya kuangamiza mazalia ya mbu na sio net madawa fake ya malari.

Mkuu maisha ya Watanzania yako hatarini na hakuna mtu anayejali!

Kuanzia mboga za majani ambazo zinapigwa dawa za ajabu ajabu, kuku wanaolishwa ARV's, dawa feki, mafuta ya kupika
feki, n.k. Mungu atusaidie tu maana hatuna njia ya kukwepa vyote hivi!
 
Back
Top Bottom