BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, tarehe 5 Julai 2023 saa 6:01 usiku. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
(a) Bei za rejareja za mafuta ya petroli na dizeli yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimeshuka kwa shilingi 137/Lita na shilingi 118/lita, mtawalia, ikilinganishwa na bei za toleo la tarehe 7 Juni 2023. Pia, bei ya
rejareja ya mafuta ya taa kwa Julai 2023 itaendelea kuwa ni ile iliyotangazwa katika toleo la tarehe 7 Juni 2023 kwa kuwa hakuna shehena iliyopokelewa mwezi Juni 2023.
(c) Kwa Mikoa ya Kusini (Lindi, Mtwara, na Ruvuma), hakuna shehena ya bidhaa za mafuta iliyopokelewa kupitia Bandari ya Mtwara kwa Juni 2023. Hivyo basi, bei ya rejareja ya dizeli kwa mwezi Julai 2023 itaendelea kuwa ni ile iliyotangazwa katika toleo la tarehe 7 Juni 2023.
Kutokana na upungufu wa bidhaa ya petroli katika maghala ya kuhifadhi mafuta yaliyopo Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta katika mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta hayo kutoka katika bandari ya Dar es Salaam. Hivyo basi, bei za rejareja za mafuta ya petroli katika mikoa hiyo zitazingatia bei kikomo ya rejareja ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.
(d) Aidha, kwa kuwa hakuna mafuta ya taa katika maghala yaliyopo katika 2 Bandari za Tanga na Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta katika mikoa ya Kaskazini na Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta hayo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo zitazingatia bei kikomo ya rejareja ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.