Mafunzo ya VETA yawe ni muhimu kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,591
4,278
Nimekuawa nikiwaza

Hivi tukipata kampuni kubwa mfano toyota ijenge kiwanda Tanzania ihitaji vijana 1000 walio somea kupaka rangi kwenye magari tutapata?

Wakihitaji vijana 1000 walio somea Kuchomea tutapata?

Wakihitajika vijana 500 waliosomea kutengeneza pancha na kujaza upepo kwenye magari tutapata
Bado mechanics nk

Hapo sijaongelea Viwanda vingine vinavyo hitaji vijana wenye ujuzi

Kimsingi tunahitaji sana wawekezaji waje kuekeza viwanda ila inabidi tujiandae kuwa na skilled labour ya Vijana waliopata mafunzo (18 to 30yrs)

Hapa naongelea vijana wenye Certificate na Diploma ambao ndio wazalishaji

Nafikiri pa kuanzia; Tuweke mkakati wa kuanzisha vyuo vya Veta kila Wilaya; na sio sio lazima kiwe chuo kikubwa sana

Viwe tu ni Vyuo vya kufundisha skills za kila siku

Mfano: Kupaka rangi magari, kuziba pancha, udalali, ushonaji, kutengeneza cherehani, uvuvi, mapishi, kilimo, ujenzi, udereva wa magari na mitambo nk Kutengeneza Baiskeli, Pikipiki, kutengeneza TV, Simu nk, kufanya wiring kwenye nyumba nk

Vijana wanao maliza form IV; wale ambao hawatapata nafasi waende veta kujifunza chochote watakacho chagua kwa miezi angalau 6

Form six wakati wanasubiri kuingia Chuo Kikuu waende Veta wajifunze ujuzi wowote kwa miezi 3 kulingana na kozi nk
NYONGEZA: Moja ya sababu ya kupasuka tairi barabarani na kusababisha ajali hutokana na kujaziwa upepo na watu wasio kuwa na ujuzi hivyo huweka upepo mwingi au Kidogo au kutokulinganisha tairi

ni mtazamo wangu.
 
Upo sahihi kabisa, naunga mkono hoja.

Waende kama wanavyoenda jkt kidato cha 6
 
Back
Top Bottom