Mimi nijuavyo mambo ya kijeshi, hakuna upendeleo wowote wanaopewa kisa unayo elimu ya juu. Utaenda jkt utapiga
kozi miezi 6, ukumaliza utapelekwa National Service kwa malezi ukisubiri nafasi za kwenda kozi (unaweza kumaliza miaka miwili pia).
Baada ya hapo ukibahatika kwenda kozi ya JWTZ utafanya kozi na utakua private popote utakapopangia ndani ya nchi yetu,
kama kitatokea nafasi ya kwenda TMA utafanya usaili ukifaulu utaenda TMA na ukishindwa kozi utarudishwa kikosini kupangiwa majukumu mengine kama askari wengine.
Baadae hutarusiwa kwenda kozi tena ya TMA, baada ya hapo utapewa cheo cha WOI/WOII, ukaa lindo kama kawa na sheria za jeshi itabidi usomee upya tena.