Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Ninasema watanzania tunashinda kila siku kwa kumaanisha kwamba kila siku tunapiga hatua mbele katika , Kuhoji na kushiriki katika mambo mbali mbali ya maendeleo. Vijana wengi sasa wameshaanza kuamka na kuanza kudai nchi yao. Tupo katika Safari ya Ushindi kuelekea maendeleo, unaweza ukafikiri hatupigi hatua ila mimi ninaona tunapiga hatua.
Ninachompinga mwanakijiji ni ile notion ya kwamba RA ndie anayesababisha umasiki wa Tanzania, Kwanini anaogopa kuitaja CCM ambayo kwa mika 40 bado imeshindwa kutufikisha tunapotaka kufika.
Mwanakijiji ana agenda yake ya siri , Mimi ninamwomba atueleze nafasi ya CCM katika kutupa huo umasikini, pili atuambie nafasi ya CCM katika kumpa nguvu RA .
LeoKweli, pamoja na point zako, nafasi aliyo nayo RA ndani ya hii awamu ya nne si ya kupuuzia hata kidogo. Dr. Slaa alipotaja listi ya mafisadi iliyomhusisha si tu JK mwenyewe bali hata BWM na vigogo wengine, hatukusikia cha waziri wa habari ama utawala bora wakikurupuka. Swala la Richmond lilipowaka moto jitihada zilifanyika kuzima moto wake zilizopelekea Waziri Mkuu pamoja na mawaziri wawili kujiuzulu lakini hakuna aliyemnyoshea vidole RA. Hata Kamati ya Mwakyembe ilishindwa kumhoji RA na kuishia kulalamika tu na siku RA alipotishia kumwaga yote bungeni tulishuhudia jitihada za NEC na kamati ya wabunge wa CCM zikikutanishwa kwa kikao cha dharura sababu ya RA. EPA ilipofumuka serikali iliyowekwa madarakani na wananchi ilikiri kuwa kuna vigogo wasiokamatika na wakiguswa taifa lingeyumba. Kampuni zote zilizohusishwa na wizi wa EPA viongozi wake walichukuliwa hatua isipokuwa zilizohusishwa na RA kama KAGODA. Mh. Mwakyembe alipojibizana na RA, tulishuhudia serikali kupitia mawaziri wake wakiingilia kati na kudai ugomvi wa hawa ungeliipeleka taifa pabaya. Hivi sasa Reginald Mengi amethubutu kuligusa mbuyu RA na tena tumeshuhudia serikali kwa mara nyingine ikiingilia kwa kudai malumbano yao yangeweza kulipeleka taifa kubaya.
Huyu RA ni nani mpaka kulumbana naye kuhatarishe usalama wa taifa. Huyu RA ni nani mpaka jina lake lisipatikane kwenye daftari la usajili wa makampuni yanayodaiwa ni yake. Huyu RA ni nani serikali iliyochaguliwa na wananchi imtetemekee na kumlinda kwa hali yoyote hata ikibidi kumpoteza Gavana Mzima wa Benki. Kujiuliza haya maswali hatutaweza kupata majibu lakini nina hakika tukiacha kumwangalia kama individual na kuanza kumjadili kama institution labda tunaweza tukafikia majibu. Swali what is RA is more appropriate at this stage badala ya who is RA. Kwa nini serikali imwogope na kumlinda RA, what does he represent and who is he representing and why ? Kwa nini Raisi wetu hatulii nyumbani Tanzania na kwa mantiki hiyo hiyo kwa nini aliutaka Uraisi. Kwa nini Mzee wetu Malecela kaanza kupiga filimbi mapema hivi apewe kipindi cha pili. What is the connection between these three - Iran ? I am just talking to myself or just plain day-dreaming - hizi ndoto za mchana zina matatizo, I admit.