Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Hatimaye nimefikia hitimisho kuwa juhudi za kupambana na ufisadi nchini hazitofanikiwa na ya kuwa upepo wa ushindi unavuma kuelekeza merikebu za mafisadi kuelekea ushindi! Zaidi ya watu kulalamika pembeni na kuonesha kuchukizwa na ufisadi, himaya ya ufisadi itazidi kujikita na kupenya katika vyombo vingi zaidi kwani sasa hivi dalili zote zinaonesha ufisadi haufanywi na mtu mmoja bali umekuwa ni mtandao wa uhalifu ambao umeundwa na wasomi, wanasiasa, wafanyabiashara na watu wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.
Mwanzoni ilipotajwa kuwa ni Tanzanian Mafia nilidhani ni hyperbole lakini wiki hizi chache zilizopita na taarifa ambazo ninazipata hasa baada ya kuanza kuandika suala hili ni wazi kuwa ipo "familia ya kihalifu" ambayo imejipanga vilivyo na iko tayari kutumia nguvu zao zote kuzima juhudi zozote zile za kunyofoa meno yao kwenye migongo ya Watanzania.
Sitoshangaa joto linavyozidi kupanda waandishi mahiri wa uchunguzi wakajikuta wanashambuliwa na kitakachoelezewa kuwa ni "majambazi" na kwa mwendo huo kuleta hofu kubwa kwa waandishi na kuwalazimisha waoga kati yao kunywea na kuchukua upande wa familia hiyo.
Kama vile Jitu Kubwa linavyoshika kwa kuminya mkono wa mtoto mdogo na kumburuza ndivyo ufisadi utakavyoendelea kuburuza taifa na Watanzania wengi. Lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa watawala wenye uwezo wa kifisadi wataendelea kutawala tena bila kuulizwa. Ufisadi utakaofunuliwa baadaye mwaka huu yawezekana ukawa ndiyo msumari wa mwisho kabisa utakaowafanya mafisadi kuja na silaha zao zote kuhakikisha Taifa zima linapiga magoti na kwa sauti kali kama ya wale nyani wa kwenye filamu ya Planet of the Apes watapiga ukelele "Bow"!
Kuelekea uchaguzi mkuu mwakani himaya hiyo imepanga sasa watu wapya kabisa kuanza kuingia katika safu za uongozi na hasa Bungeni ili hatimaye usalama wao uzidi kuhakikishwa. Kiwango kikubwa cha fedha kimeshatengwa kuhakikisha (na hili limeshasemwa na wengine) wabunge wote ambao wanapigia kelele ufisadi wanaaungushwa kwenye kura za maoni na watu wapya kuingia. Lengo la hilo ni kuhakikisha kuwa inapofika Bunge jipya ule upinzani ambao umekuwa ukisikika utakuwa umezimwa kwa kiasi cha kutosha na ukabakia kuwa ni upinzani wa magazetini.
Juhudi kubwa ya kujipanga huko sasa hivi ni kuelekea pia katika Mahakama za juu kitu ambacho kinafanywa kwa uangalifu mkubwa na tahadhari. Kwa macho ya uchunguzi tuangalie sana teuzi zinazokuja za Mahakama na kuzielewa vizuri.
Vyovyote vile ilivyo, naomba niwakatishe matumaini kabisa kuwa kufikiria kuwa "vita ya ufisadi ambayo bado inaendelea" kwa mujibu wa Mkuchika ni vita ambayo mafisadi watashinda. Watashinda kwa sababu kubwa tano.
a. Wamejipanga vizuri zaidi kuliko wanaopinga ufisadi (well organized). Wanaopinga ufisadi they are a fragmented bunch!
b. Wamewekeza fedha pale wanapokula na hawaoni haya kufanya hivyo (well funded). Wanaopinga ufisadi wanatumia maneno tu, wenye kuwekeza fedha wanaonekana wanataka kujitajirisha na wale ambao wanatumia fedha zao kupigana na ufisadi na wenyewe wanageuziwa kibano alimradi kuvuruga juhudi zao. Mtu mmoja (ambaye sistahili kufunga kamba za viatu vyake) ameniambia kwenye sakata hili la RA na RM nisichague upande kwa sababu nitaonekana nampendelea mmoja wao!
Yaani, mtu asichague upande kwa kuogopa kuonekana yuko upande mmoja. Ushauri wangu ni kuwa upande niliopo sihami, mtu anayetaka abadili yeye upande aje upande wangu, na ukija upande wangu wewe mwenzangu, ukiwa kinyume changu najua upande wako, neutrality is the position of the weak and the coward, I'm neither weak nor a coward!
Nawapongeza wale waliochagua upande mmoja kati ya hizi!
c. Wamejikita vizuri na kuwabana watawala na vyombo mbalimbali na hivyo kama utando wa buibui wanajua na wanaweza kujua chochote wanachotaka kujua (well connected). Wanaopinga ufisadi wachache walioko serikalini au madarakani wanafanya hivyo at their own risk hakuna wa kuwakinga na muda si mrefu wataanza kupukuchwa kama hindi.
d. Wanaogopesha; wanatumia serikali na vyombo vyake kuingiza hofu kwa watu wa kawaida kwa kauli za "kuvunjika kwa amani", "watachukuliwa hatua za kisheria", n.k (they command fear). Wanaopinga ufisadi bado hawajaanza kuleta itikadi ya matumaini na badala yake wamejikita na kupiga kambi kwenye mazungumzo ya ufisadi na kauli za dhidi ya CCM ambazo ni sawa (kwa maoni yangu) na mtu kuupuliza mbuyu, likianguka buyu moja anafikiri ni kwa sababu yake!!
e. Wako tayari kwenda umbali wowote ule kuhakikisha hawaondoki madarakani au mirija yao kukatwa (ready to sacrifice). Katika hili watawatoa sadaka wenzao wachache ili kutuliza munkari wa jamii lakini wakati huo huo wakiwapanga wengine.
Ninachosema kwa maneno mawili ni kuwa 'we are screwed!" (najua ni matatu!) hakuna matumaini, hakuna njia ya kutokea, na hakuna mashujaa wetu wa kutuongoza vitani. Tufike mahali aidha tusalimu amri, au tujiunge humo humo na kula nao "sahani moja". Tufike mahali aidha tuendelee kupiga kelele kwenye mtandao na kuibua mambo kadha wa kadha au tukubaliane kujiunga nao.
Huko tunakokwenda neutrality is not an option! Ni waoga na wasio na msimamo ndio watajifanya kuwa neutral wengine wetu itabidi tuchague upande au tukae kimya na kusubiri upande unaoshinda! aidha tuko kinyume na familia na himaya hii ya ufisadi (kwa vitendo siyo mawazo) au tuko sehemu ya familia hii na sisi tukipata nafasi tutakuwa hivyo hivyo!
Je kuna matumaini? Je, tuwaachie nchi kwani nasibu iko kinyume yetu? Je tukubali yaishe ili tuendelee kuzungumzia mambo mengine ya maendeleo? Je, Je tuwaachie nchi watawale wapendavyo!? Je tujiunga nao ili tuwabomoe kutoka "ndani"?