Mafisadi watashinda! - A somber look

Mafisadi watashinda! - A somber look

Kama ni vita basi jeshi linalopenda mabadiliko( na wana CCM wachache wakiwemo) bila kujali itikadi ya chama linabidi litumie silaha na mbinu mpya.

Nina hakika wanajamii % chache sana tunatumia mtandao, %wachache sana hasa wale waliominywa kule vijijini na majimboni hawapati habari ( magazeti, press release)zakile kinachondelea jikoni.

I wish kungekuwa kuna vyama vya wanaharakati ( nje vyama vya siasa) vingeanzisha midahalo kama hii iliyopo jamii forum huko majimboni, vijijini. I wish jamii forum ingekuwa ni NGO kubwa yenye kuwekza kuwapeleka midahalo kama hii kwa wanachi na wenyewe kuchambua pumba na mchele

Ukweli vita hii mafisadi watashinda sio tu kwa sababu ulizozizatja bali pia watashinda sababu kwa upande mwingine wa shilingi wa Wanchi wengi HAWAJAWA WELL RIGHTLY, and CORRECCTLY INFORMED .

WEAKNESS hii ya wananchi kutokuwa na taarifa za kweli na sahihi Ni STRENGHTS yao hao KUPE.

Tunahitaji resouces zaidi ya vyama vya siasa. tunahitaji format midahalo kama hii iende nje ya TOVUTI. Na Tunahitaji kuwashirikisha wananchi wengi zaidi.
 
Kama ni vita basi jeshi linalopenda mabadiliko( na wana CCM wachache wakiwemo) bila kujali itikadi ya chama linabidi litumie silaha na mbinu mpya.

Nina hakika wanajamii % chache sana tunatumia mtandao, %wachache sana hasa wale waliominywa kule vijijini na majimboni hawapati habari ( magazeti, press release)zakile kinachondelea jikoni.

I wish kungekuwa kuna vyama vya wanaharakati ( nje vyama vya siasa) vingeanzisha midahalo kama hii iliyopo jamii forum huko majimboni, vijijini. I wish jamii forum ingekuwa ni NGO kubwa yenye kuwekza kuwapeleka midahalo kama hii kwa wanachi na wenyewe kuchambua pumba na mchele

Ukweli vita hii mafisadi watashinda sio tu kwa sababu ulizozizatja bali pia watashinda sababu kwa upande mwingine wa shilingi wa Wanchi wengi HAWAJAWA WELL RIGHTLY, and CORRECCTLY INFORMED .

WEAKNESS hii ya wananchi kutokuwa na taarifa za kweli na sahihi Ni STRENGHTS yao hao KUPE.

Tunahitaji resouces zaidi ya vyama vya siasa. tunahitaji format midahalo kama hii iende nje ya TOVUTI. Na Tunahitaji kuwashirikisha wananchi wengi zaidi.

Hii ni muhimu sana ktk kufanya mabadiliko kuelimisha wapiga kura
 
Mkjj, Mafisadi washinde mara ngapi ndugu yangu? Mbona wameshashinda siku nyingi tu!!! Kesi za EPA za bilioni 133 hatuzikii tena.

Rostam na Richmond kishashinda na kuuza mtambo wake na huku TANESCO wakiendelea kumlipa. Waliohusika na ufisadi wa rada bado wanapeta tu akina Vijisenti, Idrissa Rashid na wengineo.

Mafisadi wa Kiwira wala hawajaguswa na mgodi unadaiwa umerudishwa mikononi mwa Serikali na mafisadi wamelipwa "gharama" zao za kuhudumia mgodi huo, inadaiwa wamelipwa bilioni 10 lakini ni siri kali sana hii labda kainzi kafanye kazi ya kupata info zaidi.

Akina Jeetu, Subhash Patel, Manji na mafisadi wengine bado wanapeta tu na baada ya uchaguzi hapo October 31, 2010 kesi zao zitafutwa kwa kukosekana ushahidi wa kutosha.

Kwa hiyo kama utakavyoona mafisadi walishashinda siku nyingi sana na wengine sasa wanamwagiwa misifa na Kikwete kila kukicha. Ndiyo Tanzania yetu hiyo ya maisha bora kwa kila fisadi.
 
a. Wamejipanga vizuri zaidi kuliko wanaopinga ufisadi (well organized). Wanaopinga ufisadi they are a fragmented bunch!

asante kwa hii thread MM. nimekusoma vizuri tu na nadhani hii sababu ya kwanza inabeba hizo nyingine zote. hawa jamaa wako vizuri katika kila angle...kuanzia rasilmali watu mpaka material bila kusahau sabuni ya roho..PESA. ili kuwashinda ni kuwa na mipango ambayo itaweza kupambana na mipango yao...je tunayo? hapa MUNGU hana nafasi ikiwa wenyewe tuko shaghalabaghala kwani tabia ya MUNGU ni kusaidia waja pale wenyewe wanapokuwa mstari wa mbele kujisaidia...


Ninachosema kwa maneno mawili ni kuwa 'we are screwed!" (najua ni matatu!) hakuna matumaini, hakuna njia ya kutokea, na hakuna mashujaa wetu wa kutuongoza vitani.

they screwed us long time ago....tangu tulipowaachia wapitishe azimio la zanzibar..wakaiba uchaguzi wa znz na dsm mwaka 1995 bahati mbaya sana na mwalimu alikuwa hai...wakaiba mapesa kupitia kagoda mwaka 2000 lili Ben apite kwa kishindo...wakaiba tena kagoda 2005 ili Kikwete ashinde kwa tsunami...wakawa wamepata uhalali wa kufanya kila walitakalo kwa wasaa.

Huko tunakokwenda neutrality is not an option! Ni waoga na wasio na msimamo ndio watajifanya kuwa neutral wengine wetu itabidi tuchague upande au tukae kimya na kusubiri upande unaoshinda! aidha tuko kinyume na familia na himaya hii ya ufisadi (kwa vitendo siyo mawazo) au tuko sehemu ya familia hii na sisi tukipata nafasi tutakuwa hivyo hivyo!

bahati mbaya wengi kati yetu vijana tu sehemu ya familia hii...maisha yanatusukuma huko...kama unafanya kazi na huna mchongo mwingine wa halali wa kuongeza kipato na unajiwa na dili ya kifisadi..utaipitisha ili mwisho wa siku nawe upate uwezo wa kununua RAV 4 na kujenga huko kimara, kinyerezi.....na pia uweze kuchangia harusi za wenzio kwa michango mikubwa mikubwa...

kwa hiyo ni kweli kuwa neutrality is not an option lakini bahati mbaya wengi tutaangukia upande wa mafisadi.



Je kuna matumaini? Je, tuwaachie nchi kwani nasibu iko kinyume yetu? Je tukubali yaishe ili tuendelee kuzungumzia mambo mengine ya maendeleo? Je, Je tuwaachie nchi watawale wapendavyo!? Je tujiunga nao ili tuwabomoe kutoka "ndani"?

matumaini yapo lakini si kwa kizazi hiki cha wazee wetu ambao ndiyo mafisadi wenyewe wala sisi watoto wao ambao ni zao la hao mafisadi....pengine matumaini yatakuwepo kama tutawekeza katika kujenga jamii yenye maadili ya kuheshimu haki na usawa bila kujali rangi, kabila, dini, cheo wala chochote kitachoweza kutumiwa kumfanya mtu mmoja aonekane kuwa ni bora kuliko mwingine...haya yatawezekana kwa kizazi cha watoto au wajukuu wetu.
 
Mafisadi ni sehemu ya jamii wengine ni marafiki zetu hata kwenye facebook. Tunacheka nao na hata kufurahia matokeo ya ufisadi wao na wakati mwingine tunawapa big up. Kuua ufisadi ni kubadili mfumo mzima na kitu hicho si cha muda mfupi ni gradual change. Isipokuwa kuna maeneo ambayo inatubidi tupaze sauti hata kama kuta za ikulu zitapasuka .
 
Hatimaye nimefikia hitimisho kuwa juhudi za kupambana na ufisadi nchini hazitofanikiwa na ya kuwa upepo wa ushindi unavuma kuelekeza merikebu za mafisadi kuelekea ushindi! Zaidi ya watu kulalamika pembeni na kuonesha kuchukizwa na ufisadi, himaya ya ufisadi itazidi kujikita na kupenya katika vyombo vingi zaidi kwani sasa hivi dalili zote zinaonesha ufisadi haufanywi na mtu mmoja bali umekuwa ni mtandao wa uhalifu ambao umeundwa na wasomi, wanasiasa, wafanyabiashara na watu wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.

Mwanzoni ilipotajwa kuwa ni Tanzanian Mafia nilidhani ni hyperbole lakini wiki hizi chache zilizopita na taarifa ambazo ninazipata hasa baada ya kuanza kuandika suala hili ni wazi kuwa ipo "familia ya kihalifu" ambayo imejipanga vilivyo na iko tayari kutumia nguvu zao zote kuzima juhudi zozote zile za kunyofoa meno yao kwenye migongo ya Watanzania.

Sitoshangaa joto linavyozidi kupanda waandishi mahiri wa uchunguzi wakajikuta wanashambuliwa na kitakachoelezewa kuwa ni "majambazi" na kwa mwendo huo kuleta hofu kubwa kwa waandishi na kuwalazimisha waoga kati yao kunywea na kuchukua upande wa familia hiyo.

Kama vile Jitu Kubwa linavyoshika kwa kuminya mkono wa mtoto mdogo na kumburuza ndivyo ufisadi utakavyoendelea kuburuza taifa na Watanzania wengi. Lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa watawala wenye uwezo wa kifisadi wataendelea kutawala tena bila kuulizwa. Ufisadi utakaofunuliwa baadaye mwaka huu yawezekana ukawa ndiyo msumari wa mwisho kabisa utakaowafanya mafisadi kuja na silaha zao zote kuhakikisha Taifa zima linapiga magoti na kwa sauti kali kama ya wale nyani wa kwenye filamu ya Planet of the Apes watapiga ukelele "Bow"!

Kuelekea uchaguzi mkuu mwakani himaya hiyo imepanga sasa watu wapya kabisa kuanza kuingia katika safu za uongozi na hasa Bungeni ili hatimaye usalama wao uzidi kuhakikishwa. Kiwango kikubwa cha fedha kimeshatengwa kuhakikisha (na hili limeshasemwa na wengine) wabunge wote ambao wanapigia kelele ufisadi wanaaungushwa kwenye kura za maoni na watu wapya kuingia. Lengo la hilo ni kuhakikisha kuwa inapofika Bunge jipya ule upinzani ambao umekuwa ukisikika utakuwa umezimwa kwa kiasi cha kutosha na ukabakia kuwa ni upinzani wa magazetini.

Juhudi kubwa ya kujipanga huko sasa hivi ni kuelekea pia katika Mahakama za juu kitu ambacho kinafanywa kwa uangalifu mkubwa na tahadhari. Kwa macho ya uchunguzi tuangalie sana teuzi zinazokuja za Mahakama na kuzielewa vizuri.

Vyovyote vile ilivyo, naomba niwakatishe matumaini kabisa kuwa kufikiria kuwa "vita ya ufisadi ambayo bado inaendelea" kwa mujibu wa Mkuchika ni vita ambayo mafisadi watashinda. Watashinda kwa sababu kubwa tano.

a. Wamejipanga vizuri zaidi kuliko wanaopinga ufisadi (well organized). Wanaopinga ufisadi they are a fragmented bunch!

b. Wamewekeza fedha pale wanapokula na hawaoni haya kufanya hivyo (well funded). Wanaopinga ufisadi wanatumia maneno tu, wenye kuwekeza fedha wanaonekana wanataka kujitajirisha na wale ambao wanatumia fedha zao kupigana na ufisadi na wenyewe wanageuziwa kibano alimradi kuvuruga juhudi zao. Mtu mmoja (ambaye sistahili kufunga kamba za viatu vyake) ameniambia kwenye sakata hili la RA na RM nisichague upande kwa sababu nitaonekana nampendelea mmoja wao!

Yaani, mtu asichague upande kwa kuogopa kuonekana yuko upande mmoja. Ushauri wangu ni kuwa upande niliopo sihami, mtu anayetaka abadili yeye upande aje upande wangu, na ukija upande wangu wewe mwenzangu, ukiwa kinyume changu najua upande wako, neutrality is the position of the weak and the coward, I'm neither weak nor a coward!

Nawapongeza wale waliochagua upande mmoja kati ya hizi!

c. Wamejikita vizuri na kuwabana watawala na vyombo mbalimbali na hivyo kama utando wa buibui wanajua na wanaweza kujua chochote wanachotaka kujua (well connected). Wanaopinga ufisadi wachache walioko serikalini au madarakani wanafanya hivyo at their own risk hakuna wa kuwakinga na muda si mrefu wataanza kupukuchwa kama hindi.

d. Wanaogopesha; wanatumia serikali na vyombo vyake kuingiza hofu kwa watu wa kawaida kwa kauli za "kuvunjika kwa amani", "watachukuliwa hatua za kisheria", n.k (they command fear). Wanaopinga ufisadi bado hawajaanza kuleta itikadi ya matumaini na badala yake wamejikita na kupiga kambi kwenye mazungumzo ya ufisadi na kauli za dhidi ya CCM ambazo ni sawa (kwa maoni yangu) na mtu kuupuliza mbuyu, likianguka buyu moja anafikiri ni kwa sababu yake!!

e. Wako tayari kwenda umbali wowote ule kuhakikisha hawaondoki madarakani au mirija yao kukatwa (ready to sacrifice). Katika hili watawatoa sadaka wenzao wachache ili kutuliza munkari wa jamii lakini wakati huo huo wakiwapanga wengine.

Ninachosema kwa maneno mawili ni kuwa 'we are screwed!" (najua ni matatu!) hakuna matumaini, hakuna njia ya kutokea, na hakuna mashujaa wetu wa kutuongoza vitani. Tufike mahali aidha tusalimu amri, au tujiunge humo humo na kula nao "sahani moja". Tufike mahali aidha tuendelee kupiga kelele kwenye mtandao na kuibua mambo kadha wa kadha au tukubaliane kujiunga nao.

Huko tunakokwenda neutrality is not an option! Ni waoga na wasio na msimamo ndio watajifanya kuwa neutral wengine wetu itabidi tuchague upande au tukae kimya na kusubiri upande unaoshinda! aidha tuko kinyume na familia na himaya hii ya ufisadi (kwa vitendo siyo mawazo) au tuko sehemu ya familia hii na sisi tukipata nafasi tutakuwa hivyo hivyo!

Je kuna matumaini? Je, tuwaachie nchi kwani nasibu iko kinyume yetu? Je tukubali yaishe ili tuendelee kuzungumzia mambo mengine ya maendeleo? Je, Je tuwaachie nchi watawale wapendavyo!? Je tujiunga nao ili tuwabomoe kutoka "ndani"?
Those days...

Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom