Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Nadhani huyu GT anayemlinganisha Mako-meo na Nyerere, hamfahamu Nyerere.

Kwa waliokula sukari nyingi wala hawawezi kufikiria kuwalinganisha hao wawili. Ni sawa na kulinganisha milima ya Dodoma na Kilimanjaro. Sawa, yote ni milima lakini hailinganishwi.

Huyu wa sasa kafanya nini cha maana kiasi cha kuwapa watu ujasiri wa kumlinganisha na Nyerere? Nyerere alikuwa jabali na huyu wa sasa ni jiwe tu. Kama wa sasa ni bwawa basi Nyerere alikuwa bahari. Kwa wale wanaodai kuwa Nyerere hakufanya kitu na vitu vingi vimefeli, wanajidanganya. Baadhi ya miradi mikubwa kabisa ya Nyerere ni kuanzisha nchi inayoitwa Tanzania. Je, imefeli (kama itafeli itakuwa chini ya hawa wa sasa lakini si chini ya mamlaka ya Nyerere). Nyerere aliamini katika ukombozi wa Afrika jambo ambalo limefanikiwa sana.

Wee! Unamlinganisha Mako-meo na Nyerere? Julius alimtwanga Idd Amin wa Uganda. Huyu wa sasa sidhani hata keshasimamia mapigano na vibaka, achilia mbali jambazi.

Ingawa binadamu ameumbiwa faraja kubwa sana ya kusahau, na wakati mwingine kutumia fursa hiyo kubadili ukweli wa kihistoria, bado Nyerere hana mfano wake. Kwa taarifa yako, wakati wake hakuna ambaye angethubutu kutoa makontena bila kulipa ushuru. Tafuta kwenye historia vita dhidi ya wahujumu uchumi, upate muziki wake. Acheni kumtania Mako-meo maana hata mwenyewe anajua kuwa ama mnamvika kilemba cha ukoka au mmebobea katika kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Huo ni uatani m-baya sana kwa rais wa nchi!
 
Suala la ukombozi wa bara la Africa tu, hakuna atakaye lingana nalo, hata wazungu hadi sasa wanashindwa organization ya Nyerere hadi leo. Alisema, akatenda, Africa yote ikiwa huru achilia mbali mambo mengine ndani ya nchi. Nyere is uncomparable. Ingawaji Magufuli yes, nampa zote kwa wakati huu wa enzi za ufisadi hadi sasa kazi nzuri sana, keep it up
 
Mmh Nyerere usimlinganishe na Magufuli aisee, sana sana mi namwita Magufuli Nyerere Jr

1. Magufuli ni mwanafunzi wa Nyerere ana NIA NJEMA na UZALENDO,
2. Magufuli ni mwanafunzi wa Nyerere, anasimamia kwa dhati ANACHOOMINI,
3. Magufuli ni mwanafunzi wa Nyerere, anahuruma na wa Tanzania wanyonge,
4. Magufuli ni mwanafunzi wa Nyerere, yupo tayari kumfunga fisadi jela na kumchapa fimbo 12 kabla na baada ya kutoka jela akamwoneshe mkewe!!!!!!!!!!!!!!!1

Chapa kazi MAGUFULI, mziki wako tmeupenda......
 
Aendelee na kasi tu atakae jaribu kumzuiya ashindwe na alegee

Anachokifanya Magufuli ndio ilikuwa kilio cha UKAWA hivyo hawawezi kumkwamisha, bali atakwamishwa na majizi sugu yaliyobaki ndani ya CCM ambayo anayaumbua sasa kuanzia na former presidaaa
 
Anachokifanya Magufuli ndio ilikuwa kilio cha UKAWA hivyo hawawezi kumkwamisha, bali atakwamishwa na majizi sugu yaliyobaki ndani ya CCM ambayo anayaumbua sasa kuanzia na former presidaaa

Ivi bado mnapokea makapi? Maana majizi yote yanatapatapa uku yanataka kuja kuungana na majizi yalotangulia ukaawa
 
Huyu sasa hana mpinzani hata chagadema wanafahamu hilo.

Jamaa anasubiri kuapishwa tu 2020

MPINZANI WAKE MAGUFULI NI CCM WENYEWE, HUONI HAWAJAFANYA MAANDAMANO JAPO YA KINAFIKI KUMUUNGA MKONO, SISI CHADEMA TUNAFURAI KWANI ANAYOTEKELEZA NI TOKA KTK ILANI YA CHADEMA NA SI YA CCM, Home chopping centre tulipanga kumtia nguvuni.
NA CHAGUO LA CCM NA JK ILIKUWA MEMBE, UYU MAGUFULI NI MATOKEO YA UPINZANI MAHIRI
 
Sasa ni muda wa watanzania wote tuwe kitu kimoja tufanye kazi kwa bidii ndio njia sahihi ya kumuunga mkono Mh.rais
 
Anachokifanya Magufuli ndio ilikuwa kilio cha UKAWA hivyo hawawezi kumkwamisha, bali atakwamishwa na majizi sugu yaliyobaki ndani ya CCM ambayo anayaumbua sasa kuanzia na former presidaaa

Good thinking; bravo
 
Kwa kasi hii ya Magufuli, Lowassa si kuwa kapoteza pambano bali kapoteza vita. Labda asubiri mteule mwingine wa ccm 2025 apambane nae, wakati huo Lowassa atakuwa na miaka 73, ccm wakiwa makini tena atasubiri 2035 wakati huo atakuwa na miaka 83, ccm wakiwa makini tena....... Endelea kujaza maana kuna kila dalili zinaonyesha atafuata nyayo za maalim Seif.
 
Kwa muda wa mwezi sasa tangu JPM aingie Ikulu nimeona tofauti kubwa kiutendaji kwani matukio ambayo yangeundiwa tume na JK watu wako nje ya kazi na pasport za kusafiria zimezuiliwa pia wengine wako chini ya ulinzi wa polisi. Kweli HAPA KAZI TU ni kiboko
 
Back
Top Bottom