Amani kwenu wazalendo wenzangu:
Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.
Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.
Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.
Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.
Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
Hilo la mabadiliko ya katiba ndiyo jibu la matatizo yetu ya uchaguzi. Hongera kwa wazo hilo la kuanzisha vuguvugu ili kesho kama tunarudia kumchagua Dr. Slaa, tunajua tuko salama vinginevyo tutakuwa tunafanya biashara ya kubeba maji kwa gunia
Ninachofikiria mimi ni kwamba kama hatutaridhia katika uchangiaji wa mawazo na hisia zetu juu ya mswaada wa katiba utaokuja tutakuja kuuana mbeleni. madaraka aliyonayo rais juu ya mswaada ya jinsi ya kuanzsha mchakato ni ya kifalme and I wl never support. Asanteni CHADEMA na hyo tume ndogo mkaongee na huyo anayesafiri angani daily na mmwambie What you feel on our bhalf! siku njema wakereketwa wenzangu
@ Gurtu. Mie natumai mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya Tanzania si kwa ajili ya kumpata Dr. Slaa. Kama hivyo ndivyo unavyofikiri basi jielimishe zaidi. Katiba mpya ni kwa maslahi ya watanzaania wote na si Chama cha Siasa. Usalama unaousema hapo ni upi????? Tunajua Dr. Slaa alikuwa akichunga WANAKONDOO WA MUNGU NA KWA MAKSUDI ALIAMUA KUWATEKELEZA HUKO PORINI. Je unauhakika gani katiba ITALINDWA?????