Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Nchi yetu ina matatizo ya aina 2
1. Matatizo ya kimfumo ambayo haya chanzo kikuu ni Katiba
2. Matatizo ya kiasili ambayo haya msingi wake ni Ujinga na mada hii ni pana sana.
Ili tuweze kupambana na matatizo ya kiasili ni muhimu na vizuri turekebishe matatizo yetu ya kimfumo ambayo msingi wake ni Katiba.
Katiba yetu ina matatizo makuu 2
1. Imetoa nguvu/ mamlaka makubwa kwa Wanasiasa kuliko watendaji wakati kiuhalisia mifumo thabiti ya nchi inajengwa na watendaji maana wanasiasa ni watu wa kupita na wa msimu
2. Katiba yetu haijaweka misingi imara ya uwajibikaji hasa kuwajibishana katika level ya Wanasiasa. Ni mara nyingi Sheria zinavunjwa na kukiukwa lakini hakuna kinachofanyika. Hii ni kwa sababu hakuna misingi ya kuwajibishana kikatiba.
Matatizo makubwa ya Nchi yetu yana msingi wa kikatiba. Na endapo mkazo ungewekwa katika Katiba basi nchi hii ingepiga hatua sahihi za kimaendeleo.
Nikiwasilikiza Chadema nacheka sana. Wanafanya siasa za pata potea tu. Haya maandamano yangekuwa na msingi sana endapo hoja kuu ingekuwa mabadiliko ya muhimu na haraka ya Kikatiba badala ya Sheria za uchaguzi.
Kama kilio Chao ni sheria za uchaguzi. Nina uhakika matatizo ya Tanzania hayataondoka hata kama wakija kuongoza chadema kama hatujatatua tatizo la msingi ambalo ni umbwe la Kikatiba.