Katiba ya Tanzania ni nzuri, lakini ya Kenya ni bora zaidi kuliko ya Tanzania

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,990
8,257
Inasemekana, Naibu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Kenya, Jenerali Ogolla, alitumwa kuzuia Ruto asitangazwe kuwa mshindi wa kiti cha Urais Kenya, lakini azma hiyo haikufanikiwa.

Viongozi wa Tume ya uchaguzi hawakuuogoopa Ujenerali wake. Waliiheshimu na kuisimamia Katiba yao kikamilifu!

Kwa nchi zingine, hata RPC tu angeweza kulifanikisha hilo, kulingana na udhaifu wa Katiba zao.

Lakini kwa nchi kama Kenya, hata Rais asingeweza kuufanikisha uovu kama huo. Na hiyo ni kwa sababu Wakenya wana Katiba nzuri waliyoikubali na hivyo wanaiheshimu kuliko kitu kingine cho chote.

Natamani na sisi tuwe na Katiba bora kuzidi ya Wakenya.
 
Attachments

  • Ruto__Ogolla_is_among_the_people_who_tried_to_overturn_my_victory,_but_he_was_the_best_to_be_G...mp4
    4.9 MB
Mimi nafikiri katiba inaendana na watu. Kwetu hata ukileta katiba ya Marekani machawa wataikanyaga na raia asijue cha kufanya huku mwenyekiti wa tume huruia ya uchaguzi, mwanasheria mkuu na jaji mkuu wakikenua meno wakiimba nyimbo za kusifu na kuabudu
 
Lakini Watanganyika wa zamani hawakuwa hivyo. Ndiyo maana akina Mkwawa waliupinga uvamizi wa kikoloni hadi dakika ya mwisho.
 
Back
Top Bottom