Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

bongo kinatakiwa tuamue wenyewe na sio kutegemea viongozi tu.. na siku zote mabadiliko ya sehemu yanaletwa na watu wa sehemu hiyo pindi wanapoamua wao kubadilika....
 
asante kaka hu ni muda wa wabongo wachache wenye sumu za uelewa wazisambaze kwa watu wengi tutapata katiba pamoja na chama kipya
 
Thanks for the blog, Zakumi i am one of those who would like to join hands with you.pls tell me what to do next, i am ready to do anyhting for my country and my people!
 
I fully supports this all initiative, we need a movement in TZ to shape the political leadership of this nation. Guys lets fight hard, the start is good and we can do better for "Umoja ni Nguvu."

Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.[/QUOTE]
 
Binafsi napongeza sana mjadala huu.

Niseme tu kwamba watanzania tulishatiwa umaskini mkubwa kifikra. Tumeminywa kiasi kwamba hivi sasa mtu si tu kwamba hawezi kusema ila hawezi hata kusema kwamba hawezi kusema.

Watanzania tunaendeshwa na genge la watu tu. Hatuwezi kujiamulia tuongozwe na nani, kwa mfumo gani na kwanini? Mafisadi ndo wanaamua nani awe rais muhula huu na atafuatia nani. Unadhani wanaweza wakatumia pesa zao kupanga safu kwa manufaa yako? Never!

Ndio maana viongozi hawa wakishaingia madarakani hawamsikilizi mwananchi hata kidogo. Na wana haki ya kufanya hivyo. Si wanamsikiliza aliyeaingiza madarakani! Hii si ndo kawaida, uongo jamani?

Tatizo lilipofikia sasa, ni kwamba sisi hao hao ambao kesho tutakufa na watoto wetu wataangamia, ndo tunakubali kuolewa na mafisadi na kuuza utu wetu, namaanisha uhuru wetu, mamlaka yetu, haki yetu, vyote tunawapa kwa vijipesa uchwara tu. Tunajisaliti wenyewe, tunasaliti familia zetu, tunamsaliti hata muumba wetu. Mbaya zaidi, hao hao mafisadi, wanatugawa kwa propaganda za maslahi yao, wanapandikiza chuki za kidini, kikabila, kikanda, kichama...! Jamani, watanzania tuamke, inatia hasira. Kuna wat wengine wenye rohi nyepesi na uzalendo hafifu wanaweza wakaamua kutafuta nchi nyingine na kuomba uraia huko kujihifadhi inhawa huu si uungwana, lakini watafanyaje na washauzwa?

Hivi jamani, kweli mtu aje amechafuka tope mwili mzima unanuka na watu wanamfukuza aende akaoge halafu anakuja kwako anakuambia "wananifukuza kwa vile mimi ni mpagani", ni lazima ukubali na usahau machungu ya nchi yako na badala yake uanze kupigana na jirani yako kwamba wapagani tunapigwa vita? Na wewe unayetaka kutumia ngao hii dhaifu kabisa huoni kweli kwamba unalipua bomu la skadi? Una akili kweli wewe? Hauna hata porojo zingine nafuu kidogo kwa taifa na watanzanaia?

Oh, God help me...!
Nawaomba ndugu zangu tuwe kitu kimoja. Tanzania inayoporwa ni moja, sote tumo humuhumu na tunauzwa huku tunaona. Fisadi hana dini, hana huruma wala upendo, japokuwa anaweza kuwa na jina la dini na hata kabila. Leo atajifanya ni rafiki yako ili afanikiwe mambo yake lakini madhara yake utayapata.

Let us fight as one. Tuvunje ukimya, tuna haki ya kuamua tunataka Muuungano wa namna gani, Rais mwenye mamlaka yenye mipaka ipi, tasisi huru zinazoteuliwa kwa uwazi na haki na kwa kumshirikisha vipi mwananchi, mfumo wa serikali upo, serikali yenye wajibu upi kwa wananchi na wananchi wanaweza kuiwajibisha vipi inaposhindwa kutimiza wajibu, jeshi la polisi lenye uwezo upi na wajibu upi, rasilimali zigawanywe vipi baina ya watanzania na hasa katika kutoa elimu na huduma muhimu za jamii. Kubwa kabisa, TUNAWABANA VIPI WATAWALA WATEKELEZE YALE YOTE TUTAKAYOYAWEKA KATIKA HIYO KATIBA MPYA!.

Asanteni wana JF kwa fursa.
 
Mimi nafikiri hili suala limefika pazuri, ni wakati wa wananchi kudai katiba mpya, makongamano yafanywe kwa vijana na wamachinga wasiachwe nyuma ili kujadili kwa kina.inauma sana kuona wazee wanatuburuza.
 
Niukweli usiopinga kwamba maamuzi wanayo yafanya wazee leo ni ss vijana ambawo yatakuja kutuharimu mbeleni nadhani vijana tunakila sbb yakuona kwamba wanayo yaamua yatakua mbali na utashi wa itikadi zao
 
Safi sana mkuu, mawazo yako mazuri, anyway tunajipanga, tutachangia thread yako baada ya kujiandaa kikamilifu.
 
Ni kweli katiba mpya ni muhimu sana lakini kwa upande wangu napata wasiwasi na mchakato mzima unavyoendelea na namna wenye madaraka wanavyouenenda utaratibu mzima wa mchakato huo. Na ni maoni yangu kwa mchakato huu hatutafika kokote. Mtu aliyeshindwa kufanya mambo mazuri katika kusimamia maendeleo ya nchi kamwe hataweza kuusimamia mchakato huu wa katiba.
 
Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.

Zakumi,
Umeanza na mapungufu ya katiba yaliyojitokeza takriban katika chaguzi zote, lakini mkuu hukutoa mfano wowote hai unaothibitisha madai yako. Naomba utuelimishe ni vifungu vipi au kipi na matatizo yake ni yepi? Ili tusaidiane hoja za kutoa maoni ya marekebisho.

Kwa mfano mimi kifungu 46 na 46A Vinanikera,vinawapa Marais nguvu ya kudhulumu haki na kufisidi mali za Taifa na kujihalalishia kinga kwa vifungu hivyo. Kwa hiyo vifungu kama hivyo lazima tuvishadidie vibadilike kabisa visituwekee/kutujengea Miungu watu. (JF Mkapa above the LAW?).
 
Hilo la mabadiliko ya katiba ndiyo jibu la matatizo yetu ya uchaguzi. Hongera kwa wazo hilo la kuanzisha vuguvugu ili kesho kama tunarudia kumchagua Dr. Slaa, tunajua tuko salama vinginevyo tutakuwa tunafanya biashara ya kubeba maji kwa gunia

@ Gurtu. Mie natumai mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya Tanzania si kwa ajili ya kumpata Dr. Slaa. Kama hivyo ndivyo unavyofikiri basi jielimishe zaidi. Katiba mpya ni kwa maslahi ya watanzaania wote na si Chama cha Siasa. Usalama unaousema hapo ni upi????? Tunajua Dr. Slaa alikuwa akichunga WANAKONDOO WA MUNGU NA KWA MAKSUDI ALIAMUA KUWATEKELEZA HUKO PORINI. Je unauhakika gani katiba ITALINDWA?????
 
Ninachofikiria mimi ni kwamba kama hatutaridhia katika uchangiaji wa mawazo na hisia zetu juu ya mswaada wa katiba utaokuja tutakuja kuuana mbeleni. madaraka aliyonayo rais juu ya mswaada ya jinsi ya kuanzsha mchakato ni ya kifalme and I wl never support. Asanteni CHADEMA na hyo tume ndogo mkaongee na huyo anayesafiri angani daily na mmwambie What you feel on our bhalf! siku njema wakereketwa wenzangu
 
Kifupi na kata Ubishi wote DECEMBER 9 siku ya IJUMAA, Tukisherehekea miaka 50 ya Uhuru...iwe ndio siku ya wananchi kuandamana nchi nzima kudai haki zao..Vyama vya siasa na taasisi zote za kijamiii itumieni siku hiyo...Mkishindwa kutumia nafasi hiyo haitatokea tena nyingine...
 
Wazo zur.i pia jitihada zifanyike kuwaelimisha wadau hasa katiba ni nini, kwa nini iwepo, na inatakiwa iweje. Maana wengine wanaweza kuingia kwenye mkumbo bila kujua hasa wanataka nini.
 
Ninachofikiria mimi ni kwamba kama hatutaridhia katika uchangiaji wa mawazo na hisia zetu juu ya mswaada wa katiba utaokuja tutakuja kuuana mbeleni. madaraka aliyonayo rais juu ya mswaada ya jinsi ya kuanzsha mchakato ni ya kifalme and I wl never support. Asanteni CHADEMA na hyo tume ndogo mkaongee na huyo anayesafiri angani daily na mmwambie What you feel on our bhalf! siku njema wakereketwa wenzangu

Hata mm naunga mkono mchango wako its true that the authorities given to a president is so highly that way he seen lik king of the state so we need to dicrease the power of the president in order 2develop our country. Big up brother
 
@ Gurtu. Mie natumai mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya Tanzania si kwa ajili ya kumpata Dr. Slaa. Kama hivyo ndivyo unavyofikiri basi jielimishe zaidi. Katiba mpya ni kwa maslahi ya watanzaania wote na si Chama cha Siasa. Usalama unaousema hapo ni upi????? Tunajua Dr. Slaa alikuwa akichunga WANAKONDOO WA MUNGU NA KWA MAKSUDI ALIAMUA KUWATEKELEZA HUKO PORINI. Je unauhakika gani katiba ITALINDWA?????

Sikia this is not tim for marumbano bt this is a tim for feeling hw we can changes our country through katiba so mambo ya uchaguz ya shapita na upepo wake so we need to see forwad with new vesion not back because the writer of one novel called OUR DEVELOPMENTS of Germans written by Brayarn N Jonson say's that THE BACK IS OVER BT NOW IS CONTINUE.
 
Brother kwanza umetisha waz lak ni zur tena zaid ya sana. Ila na mm ningependa kusema kwamb katiba hii si ya ccm wala ya Kikwete na wanawe bt katiba hii niyakwetu sisi sote watanzania, pia katiba hii ndo maisha halisi ya mtanzania yoyote anayeishi Tanzania na wale wa nje ya Tanzania. Sasa bac kama katiba hii niyawatanzania wote kwanin selikali na wabunge wa CCM wanataka waifanye kama wao wanavyo taka badala yakufuata matakwa ya wananchi ambao ndo wenye katiba? Brother nikweli umeomba tujitokez kwenye mchakat huu pindi utakapo anzishwa kwenye kumbi tofauti! Lakini kwa selikali yetu hii ninavyo ifahamu imekuwa sio sikivu kwakuweka pamba masikoni pia imekua katili kwa kutupilia mbali mapendekezo ya wananchi yanayo tolewa kuhusu mabadiliko. Mfano mzuri wa hili tuna ona pale wananchi na wanaharakati walipochangia kuhusu kuhusu kusomwa kwa katiba bunge kwa mara ya pili lakin usiwe kama muswada lakn selikali ilipuuza hili na tunaona wabunge wa CCM waliisoma kama muswada tena kwakiburi na kutukebehi. Pia tulimwona Raisi wa nchi Mh.JK Kikwete akijigamba kwa mabavu kabisa kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka na atasign ulemswada. Huo ndio ukatili ulio onyeshwa na hii selikali nakuonyesha kwamba sio sikivu. Sasa basi point yangu ni nini?? Point yang ni kwamb kwel umetuomba kwamb tujitokeze kwenye kutoa maoni ya katiba ni vizur siuatai!! Swali langu ni kwamba unauhakika gan kwamba selikali katili ya Tanzania itayafanyia kaz maoni mengi ya maskin katika kuunda katiba ikiwa yale ya mwanzo machache tena ya msingi waliya puuza???
 
Nafanya kazi kampuni fulani ya ulinzi.waliitisha intake ya kuwaajiri watu,kwa msamaha wa raisi wa kubuni ajira waliitisha hata watu wa darasa la saba.ila wao walikuwa na target ya wanaoweza kuongea kiingreza,kwa ajenda yao hio wa darasa la saba walipewa moyo tu ila hawakuwa na sifa walizotaka kwa hiyo walisha feli.kwanini wasaili wapoteze mda wao na walioaminishwa watapata kazi?je itakuwa na kwenye katiba yetu tulioshauriwa kukusanya maoni.kama ilivyo kwa wanyonge wale ambao ni lasaba waliokuwa shauku ya ajira,yaweza tokea kwa maskini na katiba.kama laiti wangewasikia walicho ongea wasaili,"waacheni wafanye interview ila wafelisheni,"wasingekuwa na haki ya kulalama na hata kushtaki kulipwa mda waliopoteza?wazo la kuvuta kumbukumbu hizi ni baada ya kuwaza nani wa kumuokoa maskini na maoni yake na katiba,kama nilivyo wasikia wasaili wale nilikuwa na uwezo wa kuwasaidia ila kwa kuwa labda sikuwajua sikufanya hivyo,je ndivyo itavyotokea kwenye katiba yenye mapungufu.<mfano>....eti kunakipengele kuwa kiongozi wa nchi kuwa na haki ya kumnyima haki mtu bila ya kufafanuliwa ni haki gani.pili kama taifa moja tusiwe na matumizi ya rasmali kwa pamoja,kwani kodi ichukuliwe toka upande fulani tuu?WATANZANIA TUISOME KATIBA NA KUFICHUA MAFUMBO YAKE!
 
Kwa namna katiba ya sasa isivyokidhi mahitaji ya watanzania wengi basi kuna umuhimu wa kila Mtanzania kuhakikisha anitumia nafasi iliyopo ya kutoa maoni yatakayoingizwa katika mchakato wa kuipata katiba katiba mpya.Hiyo itapunguza madhaifu yanayoonekana katika utendaji kazi wa sekta katika wizra mbalimbali
 
Back
Top Bottom