Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Mchakato wa Kikatiba mda fulani umelipa hasara ya billion ya fedha na ukaachwa hewani bila kukamilika,kwa kuwa Selikali ya awamu ya tano kipaumbere chake sio Katiba mpya ,mijadala mazungumzo ya Katiba mpya inaweza kuwepo kwa sehemu mijadala isilete confilct na vipaumbere vya selekali ,inaweza kuendelea taratibu na mda ukifika ikapelekwa bungeni na ikajengewa hoja then Bunge likiona umhimu litashauri Selikali ilete hoja lasmi kuhusu Katiba mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
Wenye Tanzania ni Mimi na wewe,wenye kuamua Tanzania iweje ni Mimi na wewe,wanasiasa wanajaza watu hofu na tumepokea hofu tumejawa hofu,wanasiasa wanahubili umasikini tumejawa umasikini vichwani,tunayo changamoto moja tu kama taifa tunajua kuongea sana kwenye vijiwe na mitandao.Hatujapenda katiba ndio maana tumebaki KULALAMIKA
 
Jecha! Mhuuu,Alifuata katiba lakini alivunja sheria.Maana ili ufute uchaguzi ni lazima uwe na vigezo ,kikibwa chao iwe upigaji kita uligubikwa nafujo ,mauwaji,upotevu wa visanduku na au lolote lilisababishwa mchakato wa kupiga kura na kuhesabu usifanyike.Tena ili ufute uchaguzi iwe hali hii ni kwa nchi nzima.siobaadhi ya vituo.
Hivyo alivyoamua jecha bila vigezo hivyo ni wizi wa mchana kiba kwa ajili ya maslahi ya chama fulani dhidi ya kingine ambayo kwa mujibu wa sheria ni jinai.
Lakini katiba inampa nguvu kuwa maamuzi yake ni ya mwisho hayahojiwi mahakamani.Hata kama ni batili hashtakiwi.
Hapoooooo ndipo palipo na ulazima wa kuitafuta katiba kwa hali na mali na kwa maana hiyo ni bora kutoshiriki chaguzi zifuatazo mpaka katiba ibadilike,kinyume chake ni kuumizana na kutiana vilema au kupotezeana uhai.
Au tupambane kwa nia hiyo kufa kupona mpaka kieleweke kuliko kukimbizana kwenye mikutano na kampeni za siasa tukiamini eti ccm itajitia kitanzi yenyewe kuachia madaraka kwa hiari.
t

Refer

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtoa post umekiri kwamba "toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi" na unatushawishi tukuunge mkono tubadilishe katiba.mimi nadhani ni vyema kwanza tuielewe iyo katiba iliyopo ili tujue ubaya unaotaka kutuaminisha ndipo tupige kelele ibadilishwe kuliko kutubebesha mzigo tusiuelewa kama ulivyosema hapo juu.
 
Hoja hii ilitolewa mwisho mwa 2010. Na miaka iliyofuatia mchakacho wa katiba mpya ulifanyika na bunge la katiba lilikuwepo na rasmi ya katiba mpya ilitolewa.

Hivyo watu walishasoma katiba hii na vitu gani vinatakiwa kufanyika vinaeleweka.
 
Kuna mabadiliko mawili tuu ya katiba

1. Urais miaka 7
2. Urais bila kikomo
Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
 
Ninani mwenyedhamana ya kuongoza au kuanzishamchakato huu? Na ni nani anayeuzuia usifanyike? Anauzuia kwa maslahi a nani?Je sis kama raia tusio na mamlaka yeyote ya kuitisha mchakato wa katiba na kusimamia mwenendo wake tufanyeje,?
Mimi binafsi siridhiki na hali hii ya sasa,lakini sina namna wala njia ya kuleta mabadiliko.
 
Pigeni ukulele pamoja na zumari, katiba ya Tanzania haibadilishwi ati kwa sababu wale waliokuwa wanaiba pesa za walipa kodi na kuwadhulumu raia matunda ya uhuru wao wameshindwa kuiba tena, wameshindwa kuendeleza dhuluma zao, wameshindwa kwenye medani ya ushindani. Hata mkitoa machozi ya mamba katiba haibadilishwi ng'o! Ingieni madarakani then muibadilishe. Mtalia sana lakini hapa Tanzania mmegonga mwamba. Hata hivyo vibeberu vinavyowapa pesa vinafahamu hivyo. Mlimwonea JK lakini kwa chuma cha pua kutoka Chato mmegonga mwamba.
 
Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa
By
Mtanzania Digital
-
March 17, 2019

maxresdefault-2-1024x515.jpg

Awaasa wenye siasa za malengo, tamaa Ikulu

NA AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inaonyesha kuwa Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kutokana na kile kinachoitwa ‘kinga ya urais’ kuwa na mipaka yake.

Jaji Samatta ambaye amepata kuwa Jaji Mkuu kwa takribani miaka saba kabla hajastaafu mwaka 2007 alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwasilisha mada ya ‘Uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika vyombo vya dola pamoja na utekelezaji wa sheria na utoaji wa haki’ katika kipengele cha wajibu wa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) na Takukuru kwa wanafunzi wa Shule ya Sheria nchini.

Akiwasilisha mada hiyo katika mkutano wa uwajibikaji ulioandaliwa na taasisi isioyo ya serikali ya Wajibu, Jaji Samatta ambaye amekuwa akisifika kwa misimamo na kusimamia haki alirejea Ibara 46(3) ya Katiba akisema kinga aliyopewa Rais katika ibara hiyo haihusu vitendo Rais alivyovifanya akiwa Rais lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais.

“Ni ukweli kuwa chini ya Katiba ya nchi hii Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka Mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).Ni muhimu sana ukweli huu ukaeleweka.

“Ni sahihi kabisa kusema kuwa chini ya Ibara 46(3) ya sheria mama hiyo rais aliyeacha madaraka ana kinga dhidi ya mashtaka, hata hivyo kinga hiyo ina mipaka. Inahusu tu “jambo …..alilofanya……kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba…..”kinga hii haihusu vitendo alivyofanya Rais akiwa Rais,lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais,”alisema Samatta.

Alisema kuna tofauti kubwa na iliyo wazi kati ya maneno ya ‘akiwa’ na ‘kama’,kwa mujibu wa kifungu hicho cha Katiba aliyekuwa rais hana kinga dhidi ya mashtaka kuhusu jambo lolote ambalo hakufanya kama Rais.

“Kuhusu jambo la aina hiyo Mkurugenzi wa mashtaka ana mamlaka ya kumfungulia mashtaka na mahakama zina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi hiyo kama ilivyo kwa kesi za jinai zinazoweza kufunguliwa dhidi ya watu wengine nchini.

“Kwa mfano kama alipokuwa madarakani Rais aliamua siku moja kuendesha gari yeye mwenyewe na akamgonga mtu na kusababisha kifo chake kutoakana na uzembe mkubwa kinga chini ya Ibara 46(3) ya Katiba haitamwokoa kutokana kwenye mashtaka ya kitendo hicho,vitendo vya ufisadi navyo vitakosa kinga hiyo,”.

Katika hilo hilo, Jaji Samatta alikwenda mbali na hata kuwaasa wale aliowaita wenye siasa za malengo au tamaa ya kuwa mpangaji Ikulu akiwataka watambue fika kwa faida ya nchi,ukweli huo.

Alisema watawala pia wanapaswa kuzingatia kuwa safari yao ya kuelekea huko na wakati wote watakapoongoza nchi kwenye jumba hilo kwamba ukweli ni kuwa Rais aliye madarakani hana mamlaka ya kutoa msamaha kwa mhalifu yeyote kabla hajapatikana na hatia mbele ya mahakama isipokuwa tu kama ibara ya 45(1) ya Katiba itabadilishwa kumpa mamlaka hayo.

Alisema hakuna shaka yeyote kuwa ofisi ya DPP ni moja ya ofisi kuu muhimu ndani ya dola hivyo jinsi Katiba inavyoelekeza ndivyo inavyopaswa kuwa katika nchi yenye kufuata utawala wa sheria.

“Ofisi ya DPP ikiyumba na utawala huo utatereka vibaya, hilo likitokea hakuna mwananchi ambaye hataathirika kwa namna moja au nyingine, moja ya malengo ya sheria ni kumpa DPP uhuru katika kutumia mamkala yake na kuhakikisha hakuna woga, uonevu au upendeleo katika kuamua mshukiwa ashtakiwe au mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya mtu huyo yafutwe au laa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema utenganisho huo wa mamlaka hayo pia unalenga kuzuia siasa kuingilia au kutumika katika masuala hayo nyeti na kitaalamu.

Alisisitiza kuwa ofisi ya DPP haipo kwa lengo la kuhakikisha kuwa mshukiwa lazima ashitakiwe au mshitakiwa lazima aonekane na hatia.

Alisema DPP na maafisa walio chini yake ni watumishi wa nchi ambao wajibu wao ni kulinda maslahi ya umma yakiwemo yale yanayohitaji mtu asiye onyeshwa na ushahidi kuhusika na utendaji wa kosa la jinai hashtakiwi na mshitakiwa ambaye ushahidi dhidi yake hauthibitishi kwamba alitenda kosa hatiwi hatiani.

Alisema kutumia njia za uonevu na udanganyifu hakuwezi kuyafanya mapambano dhidi ya uhalifu likiwemo kosa la rushwa yafanikiwe kinyume chake hatua hizo zitafanya mapambano dhidi ya uhalifu kutofanikiwa na chuki dhidi ya watawala kujengeka.

“Mwananchi aliyeshitakiwa na kosa la rushwa na inaonekana na mahakama kuwa haijathibitishwa kutenda kosa hilo ana haki ya kuachiliwa ,kama mshitakiwa aliyeshitakiwa na kosa lingine lolote na ushahidi dhidi yake unaposhindwa kulazimisha atiwe hatiani.

“Wakati mwingine siku hizi ninaposikiliza taarifa ya habari kupitia vituo vya televisheni napata picha kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wanateka mamlaka ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, bila shaka yoyote hatua hizo ni kinyume cha Katiba na zinaweza kusababisha viongozi wakahukumiwa kama watafunguliwa kesi za madai mahakamani na kuwalipa wanaonewa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema hatua hizo za watawala zinaweza kusababisha kuharibika kwa kesi ambazo vinginevyo zingeweza kuthibitisha hatia za washtakiwa, uovu huo unaweza kutokea hata kwenye kesi za rushwa na mapambano dhidi ya uovu huo lazima yafanyike kisheria na si vinginevyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa taasisi ya Wajibu ambaye ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh alisema a alisema lengo la taasisi hiyo ni kuongeza ushirikishwa wa wananchi katika suala zima la uwajibikaji.

Alisema aliamua kumualika Jaji Samatta kwakuwa ni mmoja kati ya viongozi waadilifu ambao wanaongea na kutenda vitu ambavyo wanaviamini na kwamba ni miongoni mwa watu wanaochukia rushwa kutoka moyoni.

Alisema mkutano wa jana ambao ni wa tatu baada ya kufanyika mikutano mingine mwishoni mwa mwaka jana katika Chuo Kikuu Dodoma pamoja na Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro ni muendelezo wa kutoa elimu kuhusu uwajibikaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Mwisho

Source : Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa | Mtanzania
 
06 JUNE 2020
Utawala wa Sheria

Uchambuzi wa Mswada Na. 3 wa Mwaka 2020, mtaalamu wa sheria afafanua

Uchambuzi wa Mswada Na. 3 wa Mwaka 2020 Mei 29, 2020, Bunge la Tanzania limekaribisha wadaua na wananchi kutoa maoni yao kuhusu Mswada Na. 3 unaorekebisha sheria mbalimbali ikwemo Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Kimsingi na Wajibu, 1994 (BRADEA) na Sheria ya Uongozi wa Mahakama namba 4 ya 2011.

Moja ya mambo yanayopendekezwa katika mswada huo wenye lengo la kubadili sheria 13 ni pamoja na kuongezwa kinga ya kisheria kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, na Jaji Mkuu kutokushitakiwa moja kwa moja na badala yake mashitaka kuelekezwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mapendekezo hayo pia yanapekwenda kuwapa kinga wafanyakazi wa mahakama, ambapo kinga hiyo ikitumika vibaya itapelekea uvunjifu mkubwa wa haki. Tazama uchambuzi huu kisha toa mano yako.

Source : HAKI TV
 
Wataalam wanao ongelea mambo ya kama etc hawataweza kutupatia mawazo mbadala kwenye taifa letu. Tunataka mambo ambayo ni live, hivi sasa haya mambo ya kina mburukenge yamepitwa na wakati. Kama sheria zetu tu za sasa watu wanapindisha mtaweza kuturundikia sheria za kukaa vitabuni?
Sheria zilizopo kama zitafuatwa bila kupindisha zinatosha kabisa kuliokoa taifa hili katika kuleta maendeleo kwa wote sio wachache tu ambao wanataka kuendeleza status quo.
 
Kweli kabisa . Magufuli atosha sana
 
Back
Top Bottom