Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Napinga kwa nguvu zangu zote kauli ya Mwanasheria Mkuu kwamba katiba mpya haitajiki bali Katiba inatakiwa kuwekwa viraka,kwanza najiuliza ni wapi ametoa jeuri Mwanasheria mkuu kutuzungumzia wananchi kwa kusema hakuna Katiba mpya jamani hawa viongozi wangekuwa wanaangalia matamshi yao yaani mtu mmoja anaweza akawazungumzia watu milioni 43 kwa kweli nastaajabu sana
 
Who is werema to take this country to hell? Ukisema katiba mpya kuna watu wanapata pressure yeye ni mmoja wapo, utasikia wanakwambia wananchi , wananchi gani hao tofauti na waliokwisha kuongea?? Maaskofu wanataka katiba mpya, cwt wanataka katiba mpya, waislamu wanataka katiba mpya, tucta/wafanyakazi wataka katiba mpya, wanazuoni wanataka katiba mpya, wanasheria na wanaharakati mbalimbali wanataka katiba mpya, jaji samata, jaji warioba, jaji kisanga, jaji manento, jaji bomani,jaji ramadhani wanataka katiba mpya , media wanataka katiba mpya,chadema, cuf, nccr,tlp, udp wote wanataka katiba mpya, yeye ag ni nani hasa kuzuia katiba mpya na kwa malsahi ya nani hasa??? Anaogopa nini kuandikwa katiba mpya????? Je hofu hii inatoka wapi???
 
hongera sana ndugu zangu kwa kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kupigania haki ya kuwa na mkataba mpya baina ya wananchi na wale waliopewa dhamana ya uongozi. vp sifa za kuwa mmoja wa kamati hiyo ni pamoja na zipi?( namaanisha kamazipo sifa za ziada) maana wapo watu wengi tungetamani kuwa washirika wa mkakati huo. aksante
 
hajajua kuwa kwa matamshi yake na utendaji wake anazidi kuonyesha umuhimu wa kuwa na katiba mpya itakayokuwa inasimamia mtu kuwajibika kwa watu anaowaongoza na si kwa mtu aliyemteua tu. hayo yote anayasema kwa sababu katiba hii ya sasa inampa mwanya wa kuthubutu kuwa na jeuri namna hiyo. ndio maana hata waziri mwenye dhamana ya katiba anaweza kukaa akajiamlia mwenyewe tu kuwa serikali haina fedha za kuratibu mchakato wa katiba mpya lakini serikali hiyihiyo ikawa ipo tayari kuwalipa wezi wa mali ya umma fidia yakukatiza wizi wao tena kwa mabilioni ya shilingi tu.
 
Watanzania ndio wenye nchi wakihitaji katiba mpya wataidai.

yeye nadhani analokundi lake ambalo ndilo analoliita watanzania. maana kama ni watanzania hawa ambao ni mimi wew yule na huyo sote tunadai katiba mpya na hatuombi tunadai maana ni haki yetu kudai.
 
Prof issa shivji kusaidiana na dr slaa wanafaa kuongoza tume ya katiba mpya
Kama jk anataka kweli kuondoa fitina na kulitakia mema taifa hili-basi watu hawa wawili wanafaa kabisa kwa vyovyote na kwa maslahi ya umma kuongoza tume ya katiba mpya.

1. Prof issa shivji amekuwa katika mchakato wa kudai katiba mpya kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi. Sio mnafiki, hanunuliki kama wasomi wetu wengi -anayetaka ukweli asome raia mwema la wiki ya jana atapata ukweli huu kutoka katika makala yake. Hayumbishwi. Nampendekeza awe mwenyekiti wa tume hiyo

2. Dr w. P. Slaa ni mtanzania mwenye msimamo aliyesababisha chachu ya katiba mpya, kama ilivyo kwa shivji slaa(phd) hanunuliki na hayumbishwi. Ni mtanzania aliyekuwa anagombea urais agenda yake kubwa ya kwanza ikiwa ni kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Ni mtanzania anayeona mbali na anayeitakia mema nchi hii, mwenye kuchukizwa na umaskini, ufisadi, ujinga, na maradhi ya nchi. Huyu anafaa kuwa katibu wa tume hii -aombwe ashiriki hatakama yeye mwenyewe hakubaliani na approach ya serikali ya jk. Lakini kwa jk kumuomba na kumtumia katika tume hii wote wawili watakuwa wameweka historia ya aina yake kwa maslahi ya umma.

Tunao watanzania wengine kama jaji kisanga,ulimwengu, ayoub lioba, amiri maneto, bomani -hawa wanaweza kutumika kama wajumbe pamoja na mama nkya, ila hoja kubwa ni kutaka watanzania wazalendo wa kweli -nilisikitishwa na tume ya bomani ya madini ambayo mpaka leo bado wizi wa madini unaendelea -ndio maana slaa(phd) hataki tume hizi kwa kuwa zinakuwa hazipo huru.

Haya ni maoni yangu na ninaamini wapo wana jf watakubaliana na mimi kwa kupitia reference ya tume zilizowahi kuundwa huko nyuma na matunda yake.​
 
Ni wakati wa kuainisha Mapungufu yaliyopo katika katiba iliyopo! Vitu vya msingi tuangalie ni vipengele gani vinatufanya tuendelee kuwa masikini! labda ni katiba? Afya na Elimu vinazungumzwaje? Rasilimali za nchi kama watu na maliasili? Siasa kwa ujumla na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Watendaji wa Serikali na watakaosimamia Sheria zote kwa ujumla! watendaji wa serikali kama Mkuu wa TAKUKURU, JESHI LA WANANCHI NA POLISI, USALAMA WA TAIFA, MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, na JAJI MKUU wanafaa kuteuliwa na Rais au Bunge lipewe jukumu hilo? Madaraka ya Rais yawe na kikomo kipi? Ni wakati mzuri kama Rais akifanya makosa akiwa madarakani basi ashitakiwe?
Mimi ni Scientist! Niambieni nyie mliobobea kwenye sheria, Uchumi, mambo ya siasa, wana habari na wote mnaofahamu. Tufungueni macho wakati huu muhimu ili nasi tuweze kutoa mchango wetu!

Inasikitisha Wakati wa ukoloni na mara baada ya uhuru Mambo yalikuwa yakienda vizuri, wakati shule ni chache, wasomi wachache na Teknologia kwa ujumla ilikuwa chini! lakini leo wasomi wengi, shule nyingi na Teknologia juu lakini mambo halijojo!!! Na President naye haelewi kwa nini nchi yetu inaendelea kuwa masikini wakati ana wataalamu wanaomsahidia!!!! KATIBA! KATIBA! KATIBA! KATIBA! ndio suluhisho? kama ndivyo hivyo basi tunangoja nini?
 
Ladies and Gentlemen,
Not a few men who cherish lofty and noble ideals hide them under a bushel for fear of being called different.
First and foremost we need to educate the public on what the current constitution stands for basically; On legislature, Judiciary and Executive.
The public needs to engage the ruling elite through forums organised by Human rights commissions, NGO'S, Churches, other denominations,business community etc.
Also, we must understand that a constitution is a backbone to growth of a growing and upcoming economies marshalled by leaders who are open to change and believe change is envitable.
You all will agree with me that the leadership has to bow in to the demands of many and not unless the agenda is pushed forth and forth and down to their throats then we must keep on waiting for another 5yrs on and on.
Remember, the government is for the people, people and the people.
And i quote in 1757 Maxims prefixed to Poor Richard's Almanac that A little neglect may breed mischief: for want of a nail the shoe was lost; for want of a shoe the horse was lost; and for want of a horse the rider was lost.




Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
 
Ni kweli kabisa ndugu yangu mi nakuunga mkono asilimia zaidi ya mia. katiba yetu imepitwa na wakati, kuna haja ya kukaa chini viongozi wote kuunda mpya, kwa sababu mambo yanaenda yanabadilika kulingana na technolojia mpya, sasa kwa nini sisi tuendelee na yale yaliyopitwa na wakati yasiyo na manufaa kwa jamii? watanzania tuamke sasa kudai haki zetu!!
 
Hilo ndilo badiliko la ukweli ila linatakiwa kufanyiwa kazi mapema kabla ya 2015.. Kwani katiba ya leo ni copy ya katiba aliyokuwa akitumia gavana wa uingereza kutuongozea hapa bongo enzi ya tanganyika.

Mapungufu ni mengi

mfumo wa uchaguzi kwa katiba ya sasa ni aibu tupu.. Raisi anafanya kampeni akiwa bado rais.. Vile vile huwezi kupinga matokeo yake..

Uendeshaji wa serikali nao ni shida tu.. Waziri mkuu ndiye msimamizi wa serikali ila hapo hapo kuna rais naye anamaamuzi yake wakipishana shida ipo na wakivurunda hakuna wa kumlaumu.. Mf. Dowans ni matokeo ya kikao cha baraza la mawaziri ambacho mwenyekiti wake ni rais na katibu mkuu kiongozi ambaye hayuko kikatiba ndiye katibu mkuu. Sasa waziri mkuu ni nani? Je uozo wa dowans nani aadhibiwe???

Mbunge kama mwakilishi wa wananchi katika bunge anakuwa pia ama mkuu wa mkoa, waziri, mjumbe wa bodi.. Sasa hapa ataangalia maslahi yapi??

Uteuzi wa wabunge wa vitu maalumu hii hata kwenye katiba haipo ni nini tija yao bungeni?? Kwanza ndiyo hao wanaoleta shida kwenye chaguzi za madiwani huko arusha.. Kwani mbunge kachaguliwa tanga<<chitanda>> na sokoine<<monduli>> halafu wanakuja kupiga kura ya meya arusha, kweli hiyo inakuja???

Uteuzi wa mabalozi, wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi wa mashirika ni wa kupeana hivyo hauangalii ufanisi wa mhusika hata kidogo..
Mfano:

Mataka kuwa mkurugenzi wa atlc wakati ameuwa shirika la bima hiyo ni akili kweli.
Omari mapuri ambaye hata kiingereza kinampiga chenga kuwa balozi tena china hiyo ni kashfa.
Mwakipesile kuwa mkuu wa mkoa wa mbeya wakati wananchi wameona hafai kuwa mbunge wao hii ni nini?
Mwanajeshi wataafu ambao hawana hata elimu ya kutosha kuwa wakuu wa mikoa / wilaya ni aibu.
 
My biggest nightmare is JK has reluctantly 'ACCEPTED' the wananchi rally for constitution simply kunyamazisha wapinzani then buy time amalize term yake tukiwa tunaamini MCHAKATO unaendelea.
Kumbuka kuna tume kama tatu before hii anayotaka kuunda vipi kuhusu mapendekezo ya tume zilizopita? Huoni kama mapendekezo yaendelee ku evolve toka kwa tume zilizopita na kutumia billions za taxpayers yaani wanaolipa PAYE?:shetani::shetani::shetani:
 
My biggest nightmare is JK has reluctantly 'ACCEPTED' the wananchi rally for constitution simply kunyamazisha wapinzani then buy time amalize term yake tukiwa tunaamini MCHAKATO unaendelea.
Kumbuka kuna tume kama tatu before hii anayotaka kuunda vipi kuhusu mapendekezo ya tume zilizopita? Huoni kama mapendekezo yaendelee ku evolve toka kwa tume zilizopita na kutumia billions za taxpayers yaani wanaolipa PAYE?:shetani::shetani::shetani:

Kwa moto huu, sasa JK hana ujanja! Wenye nchi tumeamua kuipokonya kutoka kwa mafisadi watawala!
 
Zakumi, Father Masanilo na Malecela mko wapi siku hizi wenzetu?? Ndio tuseme mumeamua kuegesha jumla?? I for one is greatly missing your critical minds around.
 
Kama RAIS ana Masikio amesikia maoni ya wanakongamano kama atakiuka kilio cha Wanazuoni nitaona Tulikosea hata Kumtoa Idd Amin Dada kule Uganda..na Bora hata Hitler angekuja kututawala kieleweke
 
Hilo la mabadiliko ya katiba ndiyo jibu la matatizo yetu ya uchaguzi. Hongera kwa wazo hilo la kuanzisha vuguvugu ili kesho kama tunarudia kumchagua Dr. Slaa, tunajua tuko salama vinginevyo tutakuwa tunafanya biashara ya kubeba maji kwa gunia

haswaaa nakuunga mkono ndugu
 
Dogo lazima Katiba iwe centered kwa Wa Tanzania na sio watu kada kada. JK na watu wake wajui kabisa kwa wasikubali Katiba mpya itakua TANZANIA aita kalika. WATANZANIA WEEEEE WEKENI SHASHA na SIME tayari. Mtu wa kwanza kula shasha ni Rostam na Makamba. Hawa watu wanatutia kichefuchefu sana nchi yetu.

WATANZANIA WEEEEE - APAKAKALIKI MPAKA IELEWEKE. Hiyo CHAMA CHA MAFISADI mwisho wake ni karibu. JK kama anataka chema ya WATANZANIA na WATANZANIA basi he has to accept people of TANZANIAN's opinion otherwise, he is digging his own grave.
 
Huyo werema ni tumbo tuu inamsumbua amesahao kwa kuna kesho na kesho kutua na watoto na wajuku wakua wanaendelea kuishi. He is a shit and a pain in the ass. Although he is educated lakini akili ana sufuri kabisa.
 
Back
Top Bottom