Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,062
2,000
Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
 

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,232
1,500
Hilo la mabadiliko ya katiba ndiyo jibu la matatizo yetu ya uchaguzi. Hongera kwa wazo hilo la kuanzisha vuguvugu ili kesho kama tunarudia kumchagua Dr. Slaa, tunajua tuko salama vinginevyo tutakuwa tunafanya biashara ya kubeba maji kwa gunia
 

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,470
1,225
Huu mchakato upo na tuna kamati ya vijana wapiganaji tunakutana tena next Monday then tutaandaa press conference kuwaeleza waandishi wa habari nia yetu na jinsi tutakavyoifanikisha.
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,215
2,000
Huu mchakato upo na tuna kamati ya vijana wapiganaji tunakutana tena next Monday then tutaandaa press conference kuwaeleza waandishi wa habari nia yetu na jinsi tutakavyoifanikisha.
Mkuu,labda uongezee hapa:
-Nyie ni akina nani na mko wapi(if you dont mind)!
-Bila shaka ni inputs nyingi zinahitajika, mngeacha milango wazi kwa wengine kuleta hizo inputs.
 

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
170
Asante sana kwa hili. This is a serious issue. Lastahili kuungwa mkono na kila mtu. Nadhani wengi tuko tayari, mtakapojitokeza tutajiunga kwa gharama zote.
 

muhulo

Member
Jul 15, 2010
43
0
nimekuwa nikifuatiria programs (discussions) kenye tv chanel kwa muda sasa na wote wanaojaribu kuonngerea katiba wanahitaji mabadiliko ya hii katiba.Insue ni kuwa organisations na viongozi waliopo madarakani hawako tayari kabisa kwa kuona ndo ngao wanayotumia kuendeleza maficho yao. we have to be ready kwa propaganda za hawa jamaa. IS THE BEST THING TO BE DONE IN THIS ERA
 

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,062
2,000
Kwa kuongezea tu. Kubadilisha katiba ni wajibu wa kizalendo. Hivyo mtanzania yoyote bila kujali dini, kabila, itkadi, umri, elimu ana haki za kuchangia na kusikilizwa.

Kwa kuwa maendeleo ya technologia ya internet yanaendelea kukua kwa kasi kubwa na kuwafikia waTanzania wengi, nina uhakika matumizi ya technologia hii yatafanya waTanzania wengine kutoka sehemu mbali mbali na wenye mitazamo tofauti kutoa mawazo yao.

Kwa sasa hivi katiba za nchi ni lazima ziende sambamba na sheria za kimataifa kuhusu haki za kibinadamu. Kuna wazalendo ambao ni wanasheria na wenye uzoefu wa masuala ya kimataifa ambao wanaweza kutoa kutoa michango kwa manufaa ya wote. Hivyo basi tuliangalie suala la katiba katika anga za kisiasa pekee yake.
 

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,062
2,000
nimekuwa nikifuatiria programs (discussions) kenye tv chanel kwa muda sasa na wote wanaojaribu kuonngerea katiba wanahitaji mabadiliko ya hii katiba.Insue ni kuwa organisations na viongozi waliopo madarakani hawako tayari kabisa kwa kuona ndo ngao wanayotumia kuendeleza maficho yao. we have to be ready kwa propaganda za hawa jamaa. IS THE BEST THING TO BE DONE IN THIS ERA


Muhulo:

Kuna sababu nyingi za wao kukata. Moja wapo ni kuwa katiba inalinda madaraka yao. Lakini vilevile inawezekana mabadiliko ya kikatiba tuyaachia kama Elite Discussion. Tunataka Jaji Warioba aendee kwenye TV na Jenerali Ulimwegu amuulize maswali.

Lakini tukiweza kufanya mazungumzo ya katiba kuwa ya kawaida, watu wengi wanaweza kushiriki. Mfano mkubwa mimi ni mshabiki wa Simba, leo ukienda Msimbazi kuchukua uongozi kinyemela viboko vitatembea. Vilevile pale kwa watani zangu Jangwani viboko vinatembea kwa katiba.

Suala la watanzania kuwa na miongozo katika jumuia zao ni kitu kinachojulikana. Hivyo changamoto langu ni kuwa majadiliano ya wazi. Tatizo la katiba ya Tanzania ni kuwa tuna utamaduni wa kuamini kuwa kuna wazee wenye busara na hekima wenye mamlaka ya kutupangia vitu gani tufanye.
 

Rugemeleza

Verified Member
Oct 26, 2009
668
195
Muhulo:

Kuna sababu nyingi za wao kukata. Moja wapo ni kuwa katiba inalinda madaraka yao. Lakini vilevile inawezekana mabadiliko ya kikatiba tuyaachia kama Elite Discussion. Tunataka Jaji Warioba aendee kwenye TV na Jenerali Ulimwegu amuulize maswali.

Lakini tukiweza kufanya mazungumzo ya katiba kuwa ya kawaida, watu wengi wanaweza kushiriki. Mfano mkubwa mimi ni mshabiki wa Simba, leo ukienda Msimbazi kuchukua uongozi kinyemela viboko vitatembea. Vilevile pale kwa watani zangu Jangwani viboko vinatembea kwa katiba.

Suala la watanzania kuwa na miongozo katika jumuia zao ni kitu kinachojulikana. Hivyo changamoto langu ni kuwa majadiliano ya wazi. Tatizo la katiba ya Tanzania ni kuwa tuna utamaduni wa kuamini kuwa kuna wazee wenye busara na hekima wenye mamlaka ya kutupangia vitu gani tufanye.

Ni lazima kuweka vuguvugu kali la kudai katiba katika nyanja zote. Hapa ushiriki wa asasi za kiraia, wasomi, madhehebu ya dini, vyama vya wafanyakazi na kijamii pamoja na watu wa kawaida hii ndio italeta shinikizo la kweli. Vilevile ni lazima hoja ijengwe kwa wale washirika wa kimaendeleo nao kuunga mkono jitihada hizo. Kwa upande wa vyama vya siasa ni bora kuwapata wabunge wazalendo kutoka vyama vyote kuunga mkono hoja hii na kuanzisha mjadala bungeni. Lakini ili wao wafanikiwe ni lazima kuwe na nguvu kubwa ya watu na kisiasa juu ya umuhimu wa hilo.
 

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,062
2,000
Bado matokeo ya uchaguzi yanaendelea kutawala. Lakini tusipoangalia uchaguzi wa 2015 unaweza kuwa na kasoro zilizotokea mwaka huu. Hivyo kama waswahili wasemavyo usipo ziba ufa utajenga kuta. Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu zinaonyesha kuwa kuna nyufa nyingi. Hivyo leo nachukua jukumu la kuonyesha kasoro (nyufa) hizo.

Mojawapo ni madaraka makubwa aliyopewa rais. Rais wa Tanzania anateuwa wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na watu wengi ambayo moja kwa moja wana maslahi ya kuona rais aliyopo madarakani anaendelea. Kwa mtaji huu inabidi tuliangalie madhumuni ya kugawa mikoa ya miaka ya 70. Ugawaji wa mikoa uliambatana na sera za madaraka mikoa ambazo zilikuwa na nia ya kuwapa watu madaraka ya kujihamulia mambo wenyewe.

Ukweli wa mambo viongozi wa mikoa na wilaya waliendelea kuteuliwa na rais kwa kushirikiana na waziri. Hivyo basi sera nzima za madarakani mikoani zilibakia kwenye makaratasi tu.

Hivyo basi kwa maoni yangu mkuu wa mkoa, wilaya na viongozi wengine wanaoteuliwa kufanya kazi mikoani, wachaguliwe na wananchi. Kuchaguliwa kwao kutakuwa na faida mbili au tatu.
1./ Kutapunguza madaraka ya rais
2./ Kutawapa uhuru viongozi hao. Kwa mfano katika kipindi cha uchaguzi wasikilize kile wananchi wanachosema sio viongozi wa taifa wanataka nini.
3./ Itatoa changamoto kwa wananchi kuchagua viongozi watendaji. Viongozi watendaji ndio wanaotakiwa kujenga shule, mabarabara, hospitali nk.
4./ Vilevile mabadiliko hayo yatatoa nafasi kwa watanzania wenye vipaji kuleta mabadiliko katika mikoa yao ambayo yatakuwa kama maandalizi yao kuchukua uongozi wa taifa.
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
Inasemekana Katika maswali ambayo humuudhi Muheshimiwa Jakaya mrisho Kikwete, ni pamoja na swala la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Ameshasikika mara chache akisema kubadili katiba si maendeleo ya nchi huku akijua kuwa Katiba ndiyo inayobana maendeleo ya nchi.

Tazama Zambia, tazama Rwanda, nchi hizi mbili zilikuwa na rushwa na ufisadi wa kutupwa, lakini marais wake wameamua kujikubali kuwa lazima Wananchi waumie kwa kuwabana na sheria ngumu zinazoleta maendeleo ya nchi ili baada ya maendeleo hayo kupatikana watafurahia maisha

Haya na hili tukio la Gongo la mboto we utasikia tu.. maana Viongozi waroho wa Madaraka wameanza kumeza Mate wakijua wanakaribia kuneemeka kupitia matatizo ya watuu,, katiba yetu ingekuwa mzuri tunge wafunga lakini mmm

Wananchi wengi tunaishi kwa kukosa basic needs kwa kiwango kile kinachotakiwa,,,

Katiba hii inatakiwa ibadilishe jamaniniiii
 

Paul J

Senior Member
Oct 25, 2010
193
0
Rais kama Kikwete hawezi kudiriki kuibadili katiba maana anajua misingi na dhamira nzima ya CCM, kwa kubadilisha katiba ccm na mafisadi watakuwa wamekoma kuhujuma rasilimali za taifa. Kiongozi anayeongelea kuibadilisha katiba ni yule tu mwenye dhamira ya kweli kuwakomboa watanzania kutoka kwenye hali ya umasikini, ujinga na maradhi walivyonavyo kwenda kwenye hali iliyobora zaidi. Kiongozi wa namna hii hawezi kutokea ndani ya CCM ambayo tayari inaumwa ugojnwa wa kansa ya uongoziikiwa ni pamoja na viongozi wake!
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
Mi ningekuwa na uwezo ninge Force ibadilishwe bwana lakini bado nachechemea,, lakini naamini kati ya watu watakao shiriki kuibadilisha katiba hii ni mimi, na wewe Rafiki
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
Hivi kwanini tusi washawishi Watanzania tuungane Tanzania Nzima Kudai Katiba mpya?
Tuungane kuidai Katiba mpya
 

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,831
2,000
Watanzania ndio wenye nchi wakihitaji katiba mpya wataidai.

Mpaka mtakapoacha uwoga.

Dhambi ya uwoga inawatafuna Watanzania walio wengi. Munashindwa kudai haki kwa kuogopa kufa. Munaogopa virungu. Aibu yenu Watz. Acheni kina Malaria Sugu wawatese.

Lakini sisi wasukuma uwoga mwiko. Tunaweza kuvumilia matatizo. Lakini tukichoka.


Yaya gete!!!
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
|Haya yote yanawezekana Tukidai katiba mpya Watanzania wote itabadilishwa tuu
 

Mzalendo

Senior Member
Mar 10, 2006
181
195
hii ni swala la muhimu labda wananchi wahamasishwe kudai katiba mpya,yani kupitia kampeni mbali mbali za kijamii kama za malaria
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom