Unasema Sumaye kaondolewa kwa sababu ya maelekezo kutoka kwa mwenyekiti then unasema alishapoteza mvuto, kutoka waziri mkuu mpaka kwenda CDM!, akawa anatafuta sababu ya kuondokea!, hivi wewe unajielewa ulichoandika kweli?!
Unasema siku hizi huoni viongozi wa vyama vingine wakijiunga CDM, kwani viongozi wakihamia CDM ndio kuimarika kwa chama?, CDM haihitaji tena viongozi toka nje, huu ni wakati wa kuwa na viongozi wao waliowatengeneza wenyewe, wanao vijana wakutosha, mambo ya kumsubiri sijui nani toka wapi yameshapitwa na wakati.
Eti Lissu hataki kurudi nchini kwa sababu CDM haina muelekeo!, kwamba yale yaliyompata Lissu unayaona madogo sio, unatunga kisababu chako cha ajabu kujidanganya hapa, Lissu harudi kwasababu ya usalama wake, hiyo ndio sababu anayoitoa yeye kila akiulizwa kuhusu hilo suala, sasa wewe unajitungia tu kisababu chako!, km unataka arudi muhakikishieni usalama wake.
Kwenye mazingira ya sasa ya ufinywaji wa demokrasia, chama tawala pekee ndio kinafanya shughuli zake za siasa freely, ni mwendawazimu pekee atakaesema CDM inakufa, toeni nafasi sawa kwa vyama vyote uone nguvu ya CDM, chaguzi ndogo za ubunge zote mmeiba kura kwa kutumia wakuu wa wilaya na mikoa, OCD, na wakurugenzi wa majiji na manispaa, wakati CDM wala hawakuwa wanafanya mikutano ya hadhara!, wake up...
umelala usingizi wa pono!