Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Johnson12345

JF-Expert Member
May 29, 2023
206
422
Habari,

Kuna rafiki yangu mmoja nilizoeana nae mda kidogo na tunafamianane kutoka na biashara zetu yeye anaumri wa 43 now. Ila kwa sasa anahali mbaya ya kiafya anaumwa magojwa yasiotibika haya kupona haiwezakani kabisa.

Sasa miaka kadhaa ya nyuma alipata mchepuko, katika kukutana na mchepuka akampatia ujauzito akafanikiwa kupata mtoto wa kiume, kafananae sana maana nimemwona kwenye picha. Baada ya miaka miwili akachepuka tena na huyo huyo mchepuko wake akampa tena ujauzito alimlumu, ila mchepuko alimwambia kuwa mimi nakupenda.

Akaamua kuvunja mahusiano na mchepuko. Ila baadae akaona ngoja tuu awatambulishe watoto kwa kaka zake na dada yake. Alifanikiwa kuwatambulisha ila kwa mkewe hakufanya hivyo. Kutokana na kuaminiana na mke wake.

Sasa ni mogonjwa yeye na mkewe wamejenga nyumba tatu na biashara zao na vitu vingine kama magari. Yeye na mkewe wamezaa watoto 2 tuu.

Shida inakuja hizo mali zote limeandikwa jina lake ila ameshirikiana na mkewe wa ndoa kabisa. Yeye kaniambia tangu aishi na mkewe hajawahi kugombana nae wala kumuona mkewe anashida yoyote. Amenikambia kuwa ni mke mzuri sana na mama bora, hana shida yoyote, hicho ndio kilipelekea hata kuwaambia kaka zake na dada yake wasimwambie mkewe. Hataki mkewe aumie.

Wadau ushauri, maana anaona akiacha tuu mali watagawana na kumuacha mkewe na maumivu makubwa sana. Yeye hilo hataki, sasa alikuwa ananiambia mimi kuwa abadilishe hati ya nyumba na mali zingine kwenda kwa majina ya watoto wa ndoa tuu. Mimi nilikuwa sina cha kumjibu nilibaki namwangalia tuu.

Nikaona isiwe shida ngoja nije hapa JF. Maoni yenu wadau anataka afanye sasa.
 
Daaa ni ishu ngumu sana.

Kuna mama mmoja hivi mume wake alizaa nje wa ndoa, akanyamaza kwa miaka kama 4 hivi. Ila baadae akaamua kwenda kwa mkewe na kumuangukia na kumwambia kuwa mke wangu nisamehe sana, nilichepuka na kupata mtoto huyu hapa. Ila kwa sasa mahusiano na mama yameisha tayari napenda kama utaona vyema mtoto huyu akae hapa apate malezi kama hawa wengine.

Yule mama baada ya kumwambia vile ndoa iliisha palepale.

Yeye mama alisema kuwa , kuja kuniambia hivyo ni kwamba huniheshimu na umedhiilisha kuwa moyo wako hana mapenzi ya kweli na mimi. Na hii imeonyesha kuwa hatuaaminiani.

Ndoa iliisha pale.

Sasa yule mama anakaa mbweni anamaisha fresh anaendasha V8.
 
Hao ni watoto wake , awape asilimia zao, ujinga ni ujinga mkubwa mwanaume unazaa njee halafu eti unaogopa kuwatambulisha watoto wako na kuushi nao eti unamuogopa mkeo, tengeneza bond yako na watoto wako wote watapendana sio wakutane uzeeni, mimi baba yangu alikuwa na ndoa moja ya kikristo ila alizaa na wanawake wengine watano na watoto wote aliwachukua wakiiwa wadogo so tulifahamiana utotoni.

Tulikua pamoja na hadi leo sioni tofauti kati yetu wote ni watoto wa mtu mmoja, na good things mzee alimpatia kila mtoto urithi wake , hata alipofariki hatukugombana wala kugawana chochote, mali ambazo hazikugawanywa zipo chini ya mama yangu mzazi na mimi ndiye msimamizi wa mali hizo za familia.

Kwa sababu mama aliwalea jamaa haawa wote wanamheshimu sana na hata baada ya mzee kufariki jamaa wanafika home kila december na famila zao na mazawadi kibao, teach your son and daugheters to love each others regardless ones born out of wedlock, thats makes famili
 
Mimi nimewahi kushuhudia tukio moja hivi ni mda kidogo.

Mume alifariki bila kuacha mirathi.
Kwenye msiba yeye na mkewe walikuwa na watoto wa kike wawili na wakiume 1 hawafanani na baba yao kivile.
Ila kwenye msiba wakaja watoto wawili wakiume mapacha wamefanana na Baba yao vile vile mpaka kutembea na walikuwa na umri sawa na mtoto wake wa kwanza aliyezaa kwenye ndoa.

Ilikuwa kesi ngumu sana ila mwishowe siunajua ndugu wa mwanaume wakagawa mali sawa.
Yule mama alichukua watoto wake akaondoka nao.

Ila sasa hivi wale watoto wamekuwa wakubwa na maisha yao na mama yao yupo. Ila watoto hawajali kama kuna ndugu kwa upande wa Baba wamewasusa kabisa. Na hata mahusiano na wale watoto wa nje hawana kabisa.
Ndugu wa mwanaume wanalalamika kuwa mama kawalisha watoto sumu, ila yeye anakataa kabisa. Ila ile tukio kipindi linatokea watoto walikuwa ni wakubwa kiasi na walikuwa wanaona mama yao alivyoteseka.

Binti yake mmoja ambaye ni wa kwazwa aliolewa hakumshirikisha hata ndugu upande wa Baba yao.
 
kosa kubwa alizaa na hakuwachukua wakiwa wadogo, nazani angewachukua wakiwa wadogo wakafahamiana na kuishi pamoja ingetengeneza sense of undugu na ukaribu, ujinga unaogopa mke eti atachukia , to mee mke aondoke tu watoto zangu wote wan haki sawa
Mimi nimewahi kushuhudia tukio moja hivi ni mda kidogo.

Mume alifariki bila kuacha mirathi.
Kwenye msiba yeye na mkewe walikuwa na watoto wa kike wawili na wakiume 1 hawafanani na baba yao kivile
 
Duu kuna kaka mmoja yeye ana mkewe walikuwa na watoto 3 wakike tupu. Sasa akaamua kwenda kuzaa nje kutafuta mtoto wa kiume alifanikiwa na kwenda kumtambulisha kwa ndugu kama wote mkewe aligombananae ila wakamwambia tuh huyu ni mtoto wake hata ukachukia haisaidii akakukubali.

Ndugu wa mwanaume wakamwambia kaka yao huyo ni mtoto wako mchukue ukae nae azoeane na wenzie. Yule kaka akamchukua akawa anaishi nae mkewe akanyamaza. Mawifi wakawa wanamsema tuu dada yule kuwa hamtaki mtoto wa mume wake.

Sasa mkewe nae akaamua kuzaa nje, yeye na mkewe ni weupe kwa hio watoto wote ni weupe mpaka wa mume wa nje.

Ila mkewe akachepuka na mwanaume mweusi, mtoto kazaliwa mweusi , mume eee.

Mkewe wake akamwambia huyu mtoto sio wako anaBaba yake.

Kwenye cheti cha kuzaliwa mama akaandika Baba yake halisi na sio mume wake. Yule kaka alilalamika sana kwao.

ILA baba yale alimwambia kuwa Hata wewe ulifanya hivyo hivyo kuwa mpole tuu najua unaumia kuwa mpole tu.

Dada zake walimtukuna sana yule dada. Ndoa ya kikristo. Wakawashauri tuu tulieni mlee watoto hao. Sasa hivi wote ni wakubwa kipindi cha likizo wa nje wote wanaenda kwa wazazi wao kuwasalimia likizo ikiisha wanarudi. Familia inawatoto 5 sasa.
 
Duu kuna kaka mmoja yeye ana mkewe walikuwa na watoto 3 wakike tupu. Sasa akaamua kwenda kuzaa nje kutafuta mtoto wa kiume alifanikiwa na kwenda kumtambulisha kwa ndugu kama wote mkewe aligombananae ila wakamwambia tuh huyu ni mtoto wake hata ukachukia haisaidii.
akakukubali.
Ndugu wa mwanaume wakamwambia kaka yao huyo ni mtoto wako mchukue ukae nae azoeane na wenzie. Yule kaka akamchukua akawa anaishi nae mkewe akanyamaza. Mawifi wakawa wanamsema tuu dada yule kuwa hamtaki mtoto wa mume wake.

Sasa mkewe nae akaamua kuzaa nje , yeye na mkewe ni weupe kwa hio watoto wote ni weupe mpaka wa mume wa nje.
Ila mkewe akachepuka na mwanaume mweusi , mtoto kazaliwa mweusi , mume eee.
Mkewe wake akamwambia huyu mtoto sio wako anaBaba yake.
Kwenye cheti cha kuzaliwa mama akaandika Baba yake halisi na sio mume wake. Yule kaka alilalamika sana kwao.
ILA baba yale alimwambia kuwa Hata wewe ulifanya hivyo hivyo kuwa mpole tuu najua unaumia kuwa mpole tuu.

mwanyaluke
Mkeo akifanya hivi utafanya nn
 
Mwanaume akichit ni sawa mwanamke sio sawa mahusiano yanakufa hapo hapo na mngoni analawitiwa hii dunia haijawahi kuwa fair.. wanaume hatukosei

hii story kama ni ya kweli nampa hongera mwanamke . Ubaya kwa ubaya yani
 
Wewe mtu mmoja kidume unataka mahusiano mazuri na mke wako asiyetaka watoto wa nje ya ndoa, wewe unataka watoto wa nje ya ndoa, unataka hao watoto wa nje ya ndoa wasijulikane na mkeo, na pia unataka mahusiano mazuri na hao watoto mpaka uwape urithi.

Chagua moja, kipaumbele chako ni nini?

Mahusiano mazuri na mke au mahusiano mazuri na haki ya urithi kwa watoto?

Huwezi kupata kila unachotaka kila siku.
 
Back
Top Bottom