Nafikri wewe kama walivyo wachangiaji wengi humu ni wagumu sana kuelewa au labda sijui hamtaki kuelewa, nilichomaansiha ni kwamba sisi hatuwezi kumudu kuwa na maadui wa Isreali, sasa wewe unataja nchi kama USA, Ufaransa n.k hao wanaweza kudili na maadui wa Israeli hata hivyo kila siku wanashikwa juzi kati hapa walishikwa na magaidi wa isis Airport huko huko Ulaya!
Lkn hawa Wazungu wana kila sababu ya kuwa na Israeli kwa maana wana historia nao, kwa mfano huwezi kuwatenganisha Waingereza na Israeli kwa maana ndiyo waliowapa hiyo nchi iliyokuwa inakaliwa na Wapalestina na Wayahudi (hapa naongelea Wayahaudi asilia na siyo Wahamiaji wa ktk Ulaya, Urusi na kwingineko) mwaka 1948 kama zawadi, vile vile Ufaransa ndiyo waliokuwa wanatawala huko Syria , Lebanoni na kwingineko hivyo hao watu wana kila sababu ya kuwa sehemu ya matatizo ya Israeli!
Sasa sisi tuna uhusiano gani na Israeli mpaka tuje tutake tujiingize kwenye magomvi yao? Yaani ni kwa nini adui wa Isreali awe wetu? Angalia shida wanayoipata Nigeria na Boko Haram au hata Kenya tu hapa na Al Shabab sisemi kwamba ni kwa sababu ya Israeli ila nimetolea mfano jinsi hayo mambo yanavyoweza kuwa kero kwenye nchi hivyo sisi mpaka leo hii tumebarikiwa kwa kutokuwa na haya magomvi sasa kwa nini tuyatafute?