Madhara ya kushirikiana na Israeli!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Najua kuna baadhi ya watu wanashangilia sana ujio wa Kiongozi mkubwa wa Israeli kwenye nchi za AM na hata nchi yetu pia iliwakilishwa ingawaje Raisi wetu hakwenda namuunga mkono kwa hilo!

Binafsi naona kwamba siyo jambo la busara kushirikiana na nchi hiyo ya Israeli, na sababu ni kwamba nchi hiyo ina maadui wengi sana na niijuavyo Israeli, Kiongozi wao hakuja hapa kwa sababu anapenda kusaidia nchi zetu kama ambavyo wengi wanaamini, kwani kama ingekuwa ni hivyo kwa nini hakuja miaka 5 iliyopita? kwa nini leo hii? Hivyo basi ingawaje hilo linaweza kuwa kweli kwa upande mmoja lkn pia tusisahau kwamba Israeli wanategemea msaada wetu kwao pindi watuhitajipo, sasa ni msaada gani tutawapa Israeli?

Ninachopenda kuonya mimi ni kwamba sasa hivi Dunia imechafuka na inaendelea kuchafuka siku hadi siku, kitakachokuja kutokea ni kwamba maadui wa Israeli watakuwa maadui wetu, ghafla na sisi tutaingia kwenye hayo magomvi ya akina Irani, Uturuki na sijui Urusi na Isis, Je tunaweza kukabili hali hiyo?

Kulikuwa na sababu kwa nini Mlm.Nyerere alifwata Siasa za ,,kutofungamana na upande wowote ule", alielewa hili, kwani Mlm.Nyerere alisomea Historia tena huko huko Ulaya hivyo uelewa wake wa Siasa za kidunia ulikuwa mkubwa sana na hakuwa mjinga alivyoamua kujitenga nchi na Siasa za Mataifa makubwa au unaweza kusema kutokuchagua upande!

Hivyo tuchekelee kushirikiana na Israeli lkn siku wakituhitaji tusianze kusema hayatuhusu, hapo ndipo tutakapojua MOSAD ni nani, na je tuko tayari kuwafanya maadui wa Israeli maadui wetu?

Tukumbuke kwamba hakuna msaada unaokuja bure, hata ukisikia USA wametoa msaada TZ basi ujue ni lazima kwa mfano computer ziwe za Dell na siyo Toshiba, ukisikia Ujapani wametoa fedha za br. ni lazima Kampuni ya Japani ndiyo ijenge vile vile Uchina, hivyo kama tunachekelea kupata misaada ya Israeli pia tukubali kuwa nao watakapo tuhitaji, hayo mambo ya akina Boko Haram, Al shabab sijui Koni huko Uganda msifikiri yapo tu bila ya sababu ...

Binafsi nisingependa TZ yetu ijiingize kwenye hayo maugomvi, kwani hatuwezi kuhimili kuwa na maadui!

*
In the UN there are many [resolutions] which target Israel and we want to change this with the help of the Africans,” Arye Oded, a former Israeli ambassador to Kenya and Uganda, told German broadcaster DW

Israeli exports to Africa totaled about $1 billion last year, about 2% of its total exports.

With insurgencies and Takfiri militancy growing across Africa, including Qaeda-affiliated al-Shabaab and Daesh-linked Boko Haram, Israeli leaders are looking to sell advanced military equipment to the continent, the New York Times wrote.

Netanyahu is also expected to discuss the eviction of around 40,000 migrants and refugees from Sudan and Eritrea who entered Israel through Egypt.

According to the British daily Financial Times, Israel has reached an agreement with Uganda and Rwanda to resettle the refugees.

Last year, Israel ordered African migrants to choose between deportation and indefinite imprisonment. About 2,000 Africans are reportedly held in Israeli prisons.

inalekea uelewa wakokimataifa na hata historia ya nchi hii ni mdogo sana kwako, hivi unajua nchi hii israel aliifanyia mambo managapi kabla uhusiano wetu haujavunjika.Kuhusu maadui kuna nchi ina maadui kama marekani au china.diplomasia yetu ya sasa ni uchumi hatuwezi kukataa kuwa na uhusiano na israel kwa sababu zisizo na mashiko kama zako
 
Lakini Uchina na USA wanaweza kumudu kuwa maadui sisi hatuwezi, Boko Haramu peke yake wanawatoa jasho Nigeria!
 
Sababu unazotoa sikubaliani nazo kwanza ili upate mafanikio unahitaji marafiki lakini kupata mafanikio zaidi unahitaji maadui

Lakini hatuwezi kuwa na maadui aliokuwa nao Israeli, sisi kama nchi hatuwezi, hatuhitaji na wala hatuna sababu ya kuwa na maadui, kwani kuna nchi nyingi tu hapa Duniani zinakwenda vizuri bila ya kuwa na maadui kama Namibia, Botswana, hata AK yenyewe iko neutral!

Swali langu ni kwamba kesho Israeli akitaka msaada ktk kwetu tutamkatalia vipi wakati tumeshachukuwa wake au unafikiri hii misaada inakuja bure?
 
Tanzania ni nchi huru haichaguliwi marafiki kama kuna nchi hazipendi sisi tushirikiane na israel waende zao hivi unajua hizo nchi unazoshabikia ndio kila siku tunapata malalamiko ya kunyanyaswa raia wetu wakiwamo wanaofanya kazi ya uyaya ndiko wanakoongoza kwa human trafficking
 
Nchi gani hizo ninazozishabikia?
 
Lakini hatuwezi kuwa na maadui aliokuwa nao Israeli, sisi kama nchi hatuwezi, hatuhitaji na wala hatuna sababu ya kuwa na maadui, kwani kuna nchi nyingi tu hapa Duniani zinakwenda vizuri bila ya kuwa na maadui kama Namibia, Botswana, hata AK yenyewe iko neutral!

Swali langu ni kwamba kesho Israeli akitaka msaada ktk kwetu tutamkatalia vipi wakati tumeshachukuwa wake au unafikiri hii misaada inakuja bure?

Sidhani kama iran au nchi yoyote itaanza uadui na Tanzania kisa tuna uhusiano mzuri na isreal. Siasa za kimataifa haziko hivo mkuu. Jordan na Egypt zina uhusiano mzuri na isreal mbona sisikii zikishambuliwa na iran? Kingine Tanzania ni nchi huru tunatakiwa kufanya maamuzi kwa maslahi yetu sio maslahi ya iran au isis.
 
Sasa mpaka Rais wako akuelewe.....

Nafikiri anaelewa na ndiyo maana hakuipa hiyo ziara umuhimu mkubwa kwa kutokuhudhuria na badala yake kamtuma Waziri, hiyo ni tafsiri yangu, kwa Raisi Magufuli jinsi nilivyomsoma mpaka sasa kama akiona mwaliko una umuhimu basi uhudhuria na asipohudhuria ina maana hauna umuhimu kiihivyo!
 
We can not do without Israeli kwa kuwa ni taifa teule la Mungu!

Ni kiini cha imani za watu duniani haswa USA na Ulaya amabao wanamiliki karibu 50% ya uchumi wote wa dunia!
 
Sidhani kama iran au nchi yoyote itaanza uadui na Tanzania kisa tuna uhusiano mzuri na isreal. Siasa za kimataifa haziko hivo mkuu. Jordan na Egypt zina uhusiano mzuri na isreal mbona sisikii zikishambuliwa na iran? Kingine Tanzania ni nchi huru tunatakiwa kufanya maamuzi kwa maslahi yetu sio maslahi ya iran au isis.

Haya mambo yanakwenda ndani sana kuliko unavyodhania, sasa unafikri Misri leo hii kuna Amani ya kudumu? Ninachosema ni kwamba Israeli ana maadui wengi na ipo siku pia ataomba msaada kwetu hajakuja hapa bure hata siku moja, amekuja kwa ajenda maalumu!
 
Back
Top Bottom