Madhara ya kushirikiana na Israeli!

Madhara ya kushirikiana na Israeli!

Batbarosa. Ngoja nikuulize!!

Hivi maana ya *Barbarosa* ni nini? Jina hilo lilikuwa na mahusiano gani na unyama waliofanyiwa Warusi na dikteta mmoja wa Ulaya? Kwa nini umejiita jina hilo ?????

[emoji1321][emoji1321][emoji1321][emoji1321]Napita tuu lakini ...[emoji1321][emoji1321][emoji1321]
 
Duuh...
ndugu hata tamaa ushakata kabisa et "hatuna namna"
uhusiano na israeli ni must kivipi..?
Israel ni nchi muhimu Sana Katika maendeleo hata marekani wanawategemea Sana Israel Katika maendeleo yao ni nchi yenye agano na Mungu atakayeibariki Israel atabarikiwa na atakayeilaani atalaaniwa na Ndiyo maana tz licha ya rasirimali nyingibado tuna umasikini mkubwa.
 
Wawe wamekua wateule au la sioni sababu ya sisi kutokushirikiana nao maana haituathiri kwa vyovyote vile.

Lazima tukubali kwamba tunategemeana ili tuendelee tunahitaji kujifunza kutoka nchi mbalimbali Duniani bila kujali itikadi zao maadui na marafiki zao.

Tukianza kuangalia maadui na marafiki tutakua tunaingilia mambo ya Nchi binafsi.

Ndio maana America wao wana ile ya kwao ya No permanent friends but permanent interest. Once you mess with their interest you are in trouble
 
Hizi sababu ni very shallow.
 
Israel ni nchi muhimu Sana Katika maendeleo hata marekani wanawategemea Sana Israel Katika maendeleo yao ni nchi yenye agano na Mungu atakayeibariki Israel atabarikiwa na atakayeilaani atalaaniwa na Ndiyo maana tz licha ya rasirimali nyingibado tuna umasikini mkubwa.

Kwa nini unasema Israeli ni nchi yenye Agano na Mungu? Yaani umetumia kigezo gani?
 
Najua kuna baadhi ya watu wanashangilia sana ujio wa Kiongozi mkubwa wa Israeli kwenye nchi za AM na hata nchi yetu pia iliwakilishwa ingawaje Raisi wetu hakwenda namuunga mkono kwa hilo!

Binafsi naona kwamba siyo jambo la busara kushirikiana na nchi hiyo ya Israeli, na sababu ni kwamba nchi hiyo ina maadui wengi sana na niijuavyo Israeli, Kiongozi wao hakuja hapa kwa sababu anapenda kusaidia nchi zetu kama ambavyo wengi wanaamini, kwani kama ingekuwa ni hivyo kwa nini hakuja miaka 5 iliyopita? kwa nini leo hii? Hivyo basi ingawaje hilo linaweza kuwa kweli kwa upande mmoja lkn pia tusisahau kwamba Israeli wanategemea msaada wetu kwao pindi watuhitajipo, sasa ni msaada gani tutawapa Israeli?

Ninachopenda kuonya mimi ni kwamba sasa hivi Dunia imechafuka na inaendelea kuchafuka siku hadi siku, kitakachokuja kutokea ni kwamba maadui wa Israeli watakuwa maadui wetu, ghafla na sisi tutaingia kwenye hayo magomvi ya akina Irani, Uturuki na sijui Urusi na Isis, Je tunaweza kukabili hali hiyo?

Kulikuwa na sababu kwa nini Mlm.Nyerere alifwata Siasa za ,,kutofungamana na upande wowote ule", alielewa hili, kwani Mlm.Nyerere alisomea Historia tena huko huko Ulaya hivyo uelewa wake wa Siasa za kidunia ulikuwa mkubwa sana na hakuwa mjinga alivyoamua kujitenga nchi na Siasa za Mataifa makubwa au unaweza kusema kutokuchagua upande!

Hivyo tuchekelee kushirikiana na Israeli lkn siku wakituhitaji tusianze kusema hayatuhusu, hapo ndipo tutakapojua MOSAD ni nani, na je tuko tayari kuwafanya maadui wa Israeli maadui wetu?

Tukumbuke kwamba hakuna msaada unaokuja bure, hata ukisikia USA wametoa msaada TZ basi ujue ni lazima kwa mfano computer ziwe za Dell na siyo Toshiba, ukisikia Ujapani wametoa fedha za br. ni lazima Kampuni ya Japani ndiyo ijenge vile vile Uchina, hivyo kama tunachekelea kupata misaada ya Israeli pia tukubali kuwa nao watakapo tuhitaji, hayo mambo ya akina Boko Haram, Al shabab sijui Koni huko Uganda msifikiri yapo tu bila ya sababu ...

Binafsi nisingependa TZ yetu ijiingize kwenye hayo maugomvi, kwani hatuwezi kuhimili kuwa na maadui!
Unamaanisha hata msaada wa wataalamu kutoka Rwanda hautakuja bure, siyo?
 
Israel na boko haramu, al shabab sijui koni mara
Israel wanahusika vipi na hao waasi wenye imani ya kiislamu
Nonsense Nonsense Nonsense
 
Hahahahahaha et israel aombe msaada kwetu,labda baada ya miaka aliyotuambia Rais Magufuli Tz iwe donor country.
 
Najua kuna baadhi ya watu wanashangilia sana ujio wa Kiongozi mkubwa wa Israeli kwenye nchi za AM na hata nchi yetu pia iliwakilishwa ingawaje Raisi wetu hakwenda namuunga mkono kwa hilo!

Binafsi naona kwamba siyo jambo la busara kushirikiana na nchi hiyo ya Israeli, na sababu ni kwamba nchi hiyo ina maadui wengi sana na niijuavyo Israeli, Kiongozi wao hakuja hapa kwa sababu anapenda kusaidia nchi zetu kama ambavyo wengi wanaamini, kwani kama ingekuwa ni hivyo kwa nini hakuja miaka 5 iliyopita? kwa nini leo hii? Hivyo basi ingawaje hilo linaweza kuwa kweli kwa upande mmoja lkn pia tusisahau kwamba Israeli wanategemea msaada wetu kwao pindi watuhitajipo, sasa ni msaada gani tutawapa Israeli?

Ninachopenda kuonya mimi ni kwamba sasa hivi Dunia imechafuka na inaendelea kuchafuka siku hadi siku, kitakachokuja kutokea ni kwamba maadui wa Israeli watakuwa maadui wetu, ghafla na sisi tutaingia kwenye hayo magomvi ya akina Irani, Uturuki na sijui Urusi na Isis, Je tunaweza kukabili hali hiyo?

Kulikuwa na sababu kwa nini Mlm.Nyerere alifwata Siasa za ,,kutofungamana na upande wowote ule", alielewa hili, kwani Mlm.Nyerere alisomea Historia tena huko huko Ulaya hivyo uelewa wake wa Siasa za kidunia ulikuwa mkubwa sana na hakuwa mjinga alivyoamua kujitenga nchi na Siasa za Mataifa makubwa au unaweza kusema kutokuchagua upande!

Hivyo tuchekelee kushirikiana na Israeli lkn siku wakituhitaji tusianze kusema hayatuhusu, hapo ndipo tutakapojua MOSAD ni nani, na je tuko tayari kuwafanya maadui wa Israeli maadui wetu?

Tukumbuke kwamba hakuna msaada unaokuja bure, hata ukisikia USA wametoa msaada TZ basi ujue ni lazima kwa mfano computer ziwe za Dell na siyo Toshiba, ukisikia Ujapani wametoa fedha za br. ni lazima Kampuni ya Japani ndiyo ijenge vile vile Uchina, hivyo kama tunachekelea kupata misaada ya Israeli pia tukubali kuwa nao watakapo tuhitaji, hayo mambo ya akina Boko Haram, Al shabab sijui Koni huko Uganda msifikiri yapo tu bila ya sababu ...

Binafsi nisingependa TZ yetu ijiingize kwenye hayo maugomvi, kwani hatuwezi kuhimili kuwa na maadui!
Ila Israel wakali Sana wa Masuala ya IT.
 
Sababu unazotoa sikubaliani nazo kwanza ili upate mafanikio unahitaji marafiki lakini kupata mafanikio zaidi unahitaji maadui
ulaya(baba mzazi wa israel),imeanza kuitupa mkono israel,USA chini ya obama haikuwa usa ileile,israel ililalamika antisemitism imerud ulaya juzi hapa,icelanda wamesusia bidhaa za israel,israel inabid achukue muelekeo mwingne
 
SIASA za Dunia zimebadilika.Unahitaji kuwa na marafiki wengi wa ushirikiano kwa maendeleo.
 
Israel ni nchi muhimu Sana Katika maendeleo hata marekani wanawategemea Sana Israel Katika maendeleo yao ni nchi yenye agano na Mungu atakayeibariki Israel atabarikiwa na atakayeilaani atalaaniwa na Ndiyo maana tz licha ya rasirimali nyingibado tuna umasikini mkubwa.
upo kinyume na ukweli,bila mkono wa marekani hakuna israel,anzia kwenye veto tu UN,wengi wa wanaoitwa waisrael ni wazungu wa poland na mataifa mengne ya ulaya
 
Mbona tz tuna urafiki napalestina nahujatoa mapovu

Ni kwa sababu Palestina wanakandamizwa na kuonewa na hii ni kwa mujibu wa UN, USA,EU,AU, SADC hivyo sisi hatuko pekee yetu kwa maana hata Netanyahu mwenyewe haelewani na Obama na nchi za Ulaya kama Uswidi, Denmark na EU wengine ambao wamemtaka awape Wapelestina nchi yao wkt Netanyahu anakaidi makubaliano yaliyofikiwa ya kufanikisha Palestinian state!
 
Kulikuwa na sababu kwa nini Mlm.Nyerere alifwata Siasa za ,,kutofungamana na upande wowote ule", alielewa hili, kwani Mlm.Nyerere alisomea Historia tena huko huko Ulaya hivyo uelewa wake wa Siasa za kidunia ulikuwa mkubwa sana na hakuwa mjinga alivyoamua kujitenga nchi na Siasa za Mataifa makubwa au unaweza kusema kutokuchagua upande!
Haujasema kweli katika suala la Israel na Palestina. Si kwamba Tanzania hatukufungamana na upande wowote, bali tulikuwa tunaiunga mkono PLO ya Palestina na kuilaani Israel. Nakumbuka mwaka 1992 nikiwa sekondari 'nilitembezwa' Matembezi ya Mshikamano kuiunga mkono PLO. kwa hiyo si kwamba hatukufungamana na upande wowote, so please re-check your facts.
 
Mandela aliseka
their enemies should not be our enemies
 
SIASA za Dunia zimebadilika.Unahitaji kuwa na marafiki wengi wa ushirikiano kwa maendeleo.

Lakini usichokielewa kilimchomleta Kiongozi wa Israeli hapa AM siyo hivyo unavyofikri bali amekuja kwa sababu anatafuta marafiki baada ya Wazungu kumgomea wakiwemo Obama na EU kwamba wanamtaka atimize makubaliano na asiendeleze ujenzi na kupora ardhi ya Wapalestina na hicho ndicho kilichomleta kwani anahitaji kura kwenye UN sasa atazipata wapi? Ni Afrika tu na siyo Netanyahu peke yake Raisi wa Korea Kusini alikuwepo hapa juzi pia anahitaji kura zwa Waafrika dhidi ya K .Kaskazini huko UN na wakishazipata hizo kura wataendelea na maisha yao na hakuna kitu Waafrika tutapata!
 
Back
Top Bottom