Madhara ya kushirikiana na Israeli!

Madhara ya kushirikiana na Israeli!

Haya mambo yanakwenda ndani sana kuliko unavyodhania, sasa unafikri Misri leo hii kuna Amani ya kudumu? Ninachosema ni kwamba Israeli ana maadui wengi na ipo siku pia ataomba msaada kwetu hajakuja hapa bure hata siku moja, amekuja kwa ajenda maalumu!
Kwani akiomba msaada kwetu kuna ubaya gani? Mbona sisi tunaomba?
 
Nafikiri anaelewa na ndiyo maana hakuipa hiyo ziara umuhimu mkubwa kwa kutokuhudhuria na badala yake kamtuma Waziri, hiyo ni tafsiri yangu, kwa Raisi Magufuli jinsi nilivyomsoma mpaka sasa kama akiona mwaliko una umuhimu basi uhudhuria na asipohudhuria ina maana hauna umuhimu kiihivyo!
Mkuu usimsemehe Raisi, nakwakikishia sio hivyo umjuavyo, Magu ndiye anayetaka kufufua ubalozi wa Israel.

Kuhusu swala la urafiki na Israel ni jambo la kuamua tu, na hatuwezi kuwa na hofu kuhusu maadui zake. Mbona sisi marafiki na Marekani wakati jamaa anamaadui wengi?

Kuhusu Magu kutokuhudhuria huko Uganda, nadhani Mweshimiwa alikuwa na majukumu mengi siku hiyo pia mweshimiwa hapendi kuudhuria mikutano inayotumia lugha za kigeni yeye anapenda kuzungumza/kutumia lugha yetu ya Taifa sababu ya uzalendo aliojaliwa.
 
Si lazima tuwe na uhusiano na wazungu wote.
Hoja ya mtoa mada ina ukweli ndani yake kwa wakati huu wa gaidi. tahadhari ni muhimu yaani hatupaswi kutazama upande mmoja tu wa shilingi
Jaribu kuangalia kwa mapana upo upotoshaji mkubwa sana kauleta mleta mada si kweli kwamba tukiwa na mahusiano mazuri na israel ndo tiketi ya vikundi vyenye imani kali kuitageti nchi yetu lahasha siamini kabisa juu ya hizi fikra.
 
Hata tukijidai sisi hatutaki mahusiano na israeli haina mantiki tunajipanga kuimarisha jumuiya ya afrika ya mashariki washirika karibu wote wa jumuiya kama kenya,uganda,rwanda,sudan ya kusini wako nae sasa hii inaleta picha gani?
 
Mleta mada wewe dini gani?

Mnisamehe kwa kuuliza hilo swali kwani najua litawakwaza wengi. Ila jibu lake litatoa ya post yake
 
hakuna kurudi nyuma tena. ni nyakati na majira ya Tz kurudisha uhusiano na Israel. we have declared and decreed.
 
wasioipenda Israel mmechelewa. kulikuwa na nyakati mngeweza kushawishi kinyume na Israel lakini sasa it is too late. wait and see. time for restoration my brother has come
 
Ukijiuliza kwanini hakuja miaka 5 iliyopita, angalia mwaka wako uliozaliwa jiulize kwanini hukuzaliwa miaka 5 kabla ya mwaka wako uliozaliws utapata jibu la kipengele hicho cha swali lako.
 
Tz haitakandamizwa tena na hao destiny killers of our nation
 
ifikie maala tukaacha chuki za kidini, maana hapa naona shida ni kwamba Israel na Palestina hawapatani na kupelekea kuingiza isia za Udini Udini.

Tuondokane na tabia ya mtu akiwa na ugomvi na ndugu yako basi wewe nawe ujenge uadui pia na Mgomvi wa ndugu yako.

Sote tunajua ni jinsi gani Israel ilivyopiga hatua kwenye sekta ya kilimo na Teknolojia.

Kama nchi ambayo inataka kupiga hatua basi haina budi kujifunza kwa Israel.

Tuachene na chuki tujenge nchi na taifa kwa kushirikiana na walio endelea.

Uwezi kupiga hatua kwa kujiifunza kwa watu ambao hawajafanikiwa, kama natania basi jifunze kwa mtu ambae hajafanikiwa uone kama utafanikiwa.
 
maadui wa Israel ni wafuasi wa allah na mtume, nawasiotaka uhusiano na Taifa hili teule la MUNGU ni haohao wafuasi wa allah, na wanataka Israel ifutwe kwenye uso wa dunia ni haohao wafuasi wa allah, kwahiyo wewe usitake kutufanya tusijue ajenda na sura halisi ya mleta maada.
Historia inatufundisha kuwa Hata Catholics walikuwa wakiwapiga vita sana mayahudi. Na hata wengi wa Marabii wakiyahudi wanaipiga vita hii nchi ya Israel huku wakisema ni wameharamishwa kuwa na Taifa.
 
hivi nyie hata hiyo marekani imewafanyia nini ndo kusema kwamba marekani ni mshirika mhimu kwa tz,marekani anachukua vingapi vya kwetu tena karibia bure kabisa.
weka evidence ya hivyo marekani inavyochukua bure usituletee story za wanasiasa wa upinzani hapa
 
Lakini Uchina na USA wanaweza kumudu kuwa maadui sisi hatuwezi, Boko Haramu peke yake wanawatoa jasho Nigeria!
Waarabu wenyewe hawana msaada zaidi ya kutuletea Utumwa, Uislamu na Ugaidi!
 
Mleta mada nisaidie hivi vitu hapa.: JE KUSHIRIKIANA NA MTU NDO KUFUNGAMANA NAE?? MBONA TUNASHIRIKIANA NA CHINA,URUSI AMBAO INAONEKANA KAMA NI MAHASIMU WA MAREKANI AMBAE PIA TUNASHIRIKIANA NAE?
NAOMBA UNITOFAUTISHIE KATI YA KUSHIRIKIANA NA KUFUNGAMANA?? JE NI MAKOSA KUSHIRIKIANA NA NCHI NYINGINE? KUNA AINA NYNGI NA SHIRIKIANO IKIWAMO KIJESHI,KIBIASHARA,KISIASA N.K JE HUO UHUSIANO UNAOUSEMA KATI YETU NA ISRAEL NI UPI? TOA USHAHID WA HUO USHIRIKIANO.. naomba unisaidie ili nikubali hoja yako
 
Najua kuna baadhi ya watu wanashangilia sana ujio wa Kiongozi mkubwa wa Israeli kwenye nchi za AM na hata nchi yetu pia iliwakilishwa ingawaje Raisi wetu hakwenda namuunga mkono kwa hilo!

Binafsi naona kwamba siyo jambo la busara kushirikiana na nchi hiyo ya Israeli, na sababu ni kwamba nchi hiyo ina maadui wengi sana na niijuavyo Israeli, Kiongozi wao hakuja hapa kwa sababu anapenda kusaidia nchi zetu kama ambavyo wengi wanaamini, kwani kama ingekuwa ni hivyo kwa nini hakuja miaka 5 iliyopita? kwa nini leo hii? Hivyo basi ingawaje hilo linaweza kuwa kweli kwa upande mmoja lkn pia tusisahau kwamba Israeli wanategemea msaada wetu kwao pindi watuhitajipo, sasa ni msaada gani tutawapa Israeli?

Ninachopenda kuonya mimi ni kwamba sasa hivi Dunia imechafuka na inaendelea kuchafuka siku hadi siku, kitakachokuja kutokea ni kwamba maadui wa Israeli watakuwa maadui wetu, ghafla na sisi tutaingia kwenye hayo magomvi ya akina Irani, Uturuki na sijui Urusi na Isis, Je tunaweza kukabili hali hiyo?

Kulikuwa na sababu kwa nini Mlm.Nyerere alifwata Siasa za ,,kutofungamana na upande wowote ule", alielewa hili, kwani Mlm.Nyerere alisomea Historia tena huko huko Ulaya hivyo uelewa wake wa Siasa za kidunia ulikuwa mkubwa sana na hakuwa mjinga alivyoamua kujitenga nchi na Siasa za Mataifa makubwa au unaweza kusema kutokuchagua upande!

Hivyo tuchekelee kushirikiana na Israeli lkn siku wakituhitaji tusianze kusema hayatuhusu, hapo ndipo tutakapojua MOSAD ni nani, na je tuko tayari kuwafanya maadui wa Israeli maadui wetu?

Tukumbuke kwamba hakuna msaada unaokuja bure, hata ukisikia USA wametoa msaada TZ basi ujue ni lazima kwa mfano computer ziwe za Dell na siyo Toshiba, ukisikia Ujapani wametoa fedha za br. ni lazima Kampuni ya Japani ndiyo ijenge vile vile Uchina, hivyo kama tunachekelea kupata misaada ya Israeli pia tukubali kuwa nao watakapo tuhitaji, hayo mambo ya akina Boko Haram, Al shabab sijui Koni huko Uganda msifikiri yapo tu bila ya sababu ...

Binafsi nisingependa TZ yetu ijiingize kwenye hayo maugomvi, kwani hatuwezi kuhimili kuwa na maadui!

*
In the UN there are many [resolutions] which target Israel and we want to change this with the help of the Africans,” Arye Oded, a former Israeli ambassador to Kenya and Uganda, told German broadcaster DW



Israeli exports to Africa totaled about $1 billion last year, about 2% of its total exports.

With insurgencies and Takfiri militancy growing across Africa, including Qaeda-affiliated al-Shabaab and Daesh-linked Boko Haram, Israeli leaders are looking to sell advanced military equipment to the continent, the New York Times wrote.



Netanyahu is also expected to discuss the eviction of around 40,000 migrants and refugees from Sudan and Eritrea who entered Israel through Egypt.

According to the British daily Financial Times, Israel has reached an agreement with Uganda and Rwanda to resettle the refugees.


Last year, Israel ordered African migrants to choose between deportation and indefinite imprisonment. About 2,000 Africans are reportedly held in Israeli prisons.
Umesahau mawili. TANU Youth League (TYL) iluanzishwa na Rashidi Kawawa ba Joseph Nyerere kwa msaada wa Umoja wa Vijana wa Israel. TYL ndiyo iliyozaa TPDF au Jeshi la Wananchi baada ya maasi ya 1964 kwa msaada wa Jeshi la Israel. Vijiji vya Ujamaa mwaka 1967 vilijengwa kwa mfano na msaada wa vijiji vya pamoja vya Israel viitwavyo kibutzz. Waisraeli. Vita ya Kagera 1978 walikuja Libyan and PLO commandoes kwa makubaliano na OIC kusaidia "nchi ya Kiislamu" imevamiwa na Mkristo Nyerere: wakatuokoa mashujaa wa Kiislamu wengi wao MOSAD trained (Abdallah Twalipo, Muhidin Kimario, Ahmed Kitete, Kombe).

Waarabu wametupa nini zaidi ya tulichopata kwa kumwaga damu SMZ 1964? Nadhani safari ya kwanza jwenda nje ya Afrika JPM aende Israel.
 
Umesahau mawili. TANU Youth League (TYL) iluanzishwa na Rashidi Kawawa ba Joseph Nyerere kwa msaada wa Umoja wa Vijana wa Israel. TYL ndiyo iliyozaa TPDF au Jeshi la Wananchi baada ya maasi ya 1964 kwa msaada wa Jeshi la Israel. Vijiji vya Ujamaa mwaka 1967 vilijengwa kwa mfano na msaada wa vijiji vya pamoja vya Israel viitwavyo kibutzz. Waisraeli. Vita ya Kagera 1978 walikuja Libyan and PLO commandoes kwa makubaliano na OIC kusaidia "nchi ya Kiislamu" imevamiwa na Mkristo Nyerere: wakatuokoa mashujaa wa Kiislamu wengi wao MOSAD trained (Abdallah Twalipo, Muhidin Kimario, Ahmed Kitete, Kombe).

Waarabu wametupa nini zaidi ya tulichopata kwa kumwaga damu SMZ 1964? Nadhani safari ya kwanza jwenda nje ya Afrika JPM aende Israel.


Waarabu wanaingiaje hapa? Unaweza kunisaidia kwenye hili?​
 
Umesahau mawili. TANU Youth League (TYL) iluanzishwa na Rashidi Kawawa ba Joseph Nyerere kwa msaada wa Umoja wa Vijana wa Israel. TYL ndiyo iliyozaa TPDF au Jeshi la Wananchi baada ya maasi ya 1964 kwa msaada wa Jeshi la Israel. Vijiji vya Ujamaa mwaka 1967 vilijengwa kwa mfano na msaada wa vijiji vya pamoja vya Israel viitwavyo kibutzz. Waisraeli. Vita ya Kagera 1978 walikuja Libyan and PLO commandoes kwa makubaliano na OIC kusaidia "nchi ya Kiislamu" imevamiwa na Mkristo Nyerere: wakatuokoa mashujaa wa Kiislamu wengi wao MOSAD trained (Abdallah Twalipo, Muhidin Kimario, Ahmed Kitete, Kombe).

Waarabu wametupa nini zaidi ya tulichopata kwa kumwaga damu SMZ 1964? Nadhani safari ya kwanza jwenda nje ya Afrika JPM aende Israel.
Mimi binafsi nimekuelewa kaka..cjui wachangiaji wengine...[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji106]
 
Back
Top Bottom