Siku hizi mama Ngina akininyima namkumbusha madhara ya kukandamiza ngono na yeye anasalimu amri.
Kusema ukweli kabisa, kama wanandoa wananyimana hiyo kitu, madhara yake yanaweza kuwa makubwa sana, kwani hamjawahi kusikia hata humu JF kuwa mwanaume kamuua mkewe kwa sababu kamnyima unyumba, au eti hakumpikia chakula, hiyo sababu ya kutopikiwa chakula ni shabaha dhaifu tu, lakini nyuma a ugomvi wao ni kunyimana tendo la ndoa.
Ukichunguza sana migogogro ndani ya ndoa nyingi sababu ni tendo la ndoa, aidha mke anamnyima mume kama adhabu (Hii hutumiwa na wanawame wengi sana siku hizi) au mke hatoshelezewi na mumewe tendo la ndoa na mume kuambiwa na mkewe kwamba hajatosheka ni tusi kubwa............ kwa mwanaume tayari huko ni kudharauliwa, na atajiuliza maswali mengi sana,
je kama mie simtoshelezei, ni nani anayemtoshelezea?
Kwa kuwa wanaume wengi hawajiamini na wanatawaliwa na EGO, kuambiwa hivyo na mwanamke ni kudharauliwa na wivu utaongezeka kwa sababu atahisi mke atakwenda nje kutafuta wa kumtoshelezea.....