Madhara ya Kukandamiza NGONO........!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000


Imani nyingi zinasema kwamba ili uwe mtu safi (mtakatifu) inabidi usifanye ngono mpaka utakapoolewa au utakapooa. Na zingine zinasema usifanye ngono maisha yako yote. Hii yote ni kukandamiza ngono, hii yote ni kukataa ngono, hii yote ni kukandamiza nguvu ya mapenzi, hii yote ni kukandamiza na kukataa nguvu ya uhai kwani mapenzi ni nguvu ya uhai. Bila nguvu hii, hakuna uhai. Lakini ukichunguza kwa undani zaidi, utaona kwamba, kiuhalisia unapokandamiza au unapokataa kitu chochote, wewe unakuwa kama sumaku na hicho kitu kinakuwa kama chuma, hivyo unakivuta kije kwako. Unaweza ukajichunguza hata wewe mwenyewe kwa kuangalia mambo mbalimbali ambayo uliyakataa, utashangaa kuona kwamba yote yamekutokea. Kwa hiyo, kutokana na kukandamiza sana tendo hili la kujamiiana, kila wakati binadamu anawaza kingono, anatenda kingono, anacheka kingono, anahisi kingono, anaongea kingono, kila anachokiona ni ngono, mwiAli wake wote umejaa ngono na hata milango yake yote ya fahamu imejaa ngono. Kutokana na hali hii, binadamu amekuwa mtumwa wa ngono, amekuwa mfungwa wa ngono.

Hawezi tena kuwa huru na ngono, hawezi tena kuwa mtawala wa ngono kama maumbile yalivyotaka awe. Kwa kawaida huwezi kuepuka kitu au kuacha jambo kwa kulikataa, kwa kulikandamiza au kwa kulikimbia kwani huu ni udhaifu. Kwa wale wanaomjua vizuri mbuni, watakubaliana na mimi kwamba mbuni akiona maadui hukimbia na kufukia kichwa chake kwenye mchanga, kitendo ambacho yeye hudhani yuko salama eti kwa kuwa hawaoni maadui zake. Ni jambo la aibu kwa binadamu mwenye akili kuishi maisha kama mbuni. Huwezi kuuzima moto kwa kuufunika na majani, huwezi kuukwepa mwiba au msumari kwa kuukanyaga kwani kwa kufanya hivyo utakuchoma zaidi. Binadamu hawezi kuepuka tendo la kujamiiana kwa kulikataa au kulikandamiza, bali ataliepuka kwa kulielewa kwa undani zaidi. Nguvu ya kujamiiana ni kubwa kuliko nguvu yako unayotumia kuikandamiza, ni volkano inayosubiri kulipuka. Ukibahatika kutembelea katika hospitali za vichaa, utashangaa kugundua kwamba karibu asilimia 98 ya wagonjwa hao wameugua kichaa kutokana na kukandamiza tendo la kujamiiana. Pia asilimia 99 ya wanawake wanaougua mpagao au umanyeto (hysteria) hutokana na kukandamiza tendo la kujamiiana.

Tatizo hili la mpagao huwaathiri zaidi wasichana wanaosoma katika shule za wasichana peke yake. Ili kuzuia hali hii isitokee, walimu huwashauri wapishi waweke mafutaa taa kwenye mboga, kitendo ambacho ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Nashangaa watu wanaohusika na haki za binadamu wanasubiri nini kulifuatilia hili. Kwa ushauri wangu, shule hizi zingefutwa ili zote ziwe za mchanganyika kama zilivyo shule za msingi. Madhara mengine yatokanayo na kukandamiza ngono ni ushoga, usagaji, kufanya ngono na wanyama au ndege, kufanya ngono na watoto wadogo, kupiga punyeto, vita, ufisadi, kupungua kwa umri wa kuishi, hasira za ziada, msongo, kujiua, na kadhalika. Lakini siku hizi kuna jambo lingine ambalo ni matokeo ya kukandamiza ngono, nalo ni kuangalia picha za ngono kwenye mtandao.

Kiasili binadamu siyo kiumbe wa kuangalia picha za uchi au za ngono. Jambo hili limezuka kutokana na binadamu kukandamiza ngono. Mwanamke akiuona na kuujua mwili wa mwanamme ukiwa uchi, na mwanamme akauona na kuujua mwili wa mwanamke ukiwa uchi, soko la picha za uchi na picha za ngono litakufa. Jamii na dini zimekandamiza sana ngono kiasi kwamba akili ya binadamu inachemka na ngono. Mwanamme anataka kuuona mwili wa mwanamke, haina tatizo, ni matamanio ya kawaida ya kibinadamu. Mwanamke anataka kuuona mwili wa mwanamme, haina tatizo, ni matamanio ya kawaida ya kibinadamu. Nakumbuka kipindi cha nyuma wakati baadhi ya wanawake walipoanza kuvaa vimini. Wanaume wengi walikuwa wanashindwa kujizuia kuona mapaja ya mwanamke, hawajawahi kuyaona hadharani.

Ndiyo maana wanawake hawa walibakwa hadharani. Lakini kwa sasa hali ipo tofauti sana, wanaume wamezoea kuona wanawake na vimini. Kutokana na binadamu kuvaa nguo, mwili wake umekuwa mbaya. Hii ni kwa sababu haujali tena mwili wake. Anajali zaidi uso wake tu. Hebu jiulize, kwa nini unapokuwa na kipele, chunusi au kovu usoni huwa hujisikii vizuri, huwa unakosa amani. Kila mara utakuwa unajiangalia kwenye kioo, kila mara utakuwa unakishika. Unaomba itokee miujiza kipone muda huo huo. Lakini ukiwa na kipele mgongoni, tumboni au sehemu yoyote ya mwili ambayo imefunikwa na nguo, hali huwa tofauti, huwa hukijali. Hukijali kwa sababu hakuna anayekiona, kimefunikwa na nguo. Kasheshe inakuja kipele hicho kinapokuwa sehemu za siri. Huwa unakijali sana, ingawa katika hali halisi hukijali hata kidogo.

Unakijali tu kwa sababu uliambiwa ukiwa na kipele sehemu za siri ni ugonjwa wa zinaa. Kwa hiyo kukijali kwako ni hofu dhidi ya ugonjwa wa zinaa. Kumbuka mwili ni mmoja, haijalishi kipele kipo sehemu gani ya mwili inabidi ukijali. Kutokana na hali hii, binadamu ameugawa mwili wake katika vipande vipande. Asilimia 99 ya uzingativu wake, ya kuujali mwili wake zipo kwenye zile sehemu zinazoonekana hasa usoni. Huu ni ugonjwa, akili ya binadamu inaumwa, inahitaji dawa. Kama tumbo lako litaanza kuwa kubwa wala hujali kwa sababu unaweza kulificha, unaweza kulifunika. Mwili wako umekuwa mbaya kwa sababu huuachi wazi vinginevyo ungejua kama tumbo limeanza kuwa kubwa. Ukiwaambia watu mia wasimame uchi, wote wataona aibu na wataanza kuficha nyuso zao, kwa nini? Kuna tatizo mahali, hawajali kabisa kuhusu miili yao, wanajali zaidi kuhusu nyuso zao tu. Hii ni mbaya, huutendei haki mwili wako, lakini pia hujitendei haki wewe mwenyewe. Picha za ngono ni punyeto ya akili, hujapewa nafasi ya kumpenda mwanamke, hujapewa nafasi ya kumpenda mwanamme.

Hujapewa nafasi ya kufanya mapenzi na mwanamke, hujapewa nafasi ya kufanya mapenzi na mwanamme. Kutokana na hali hii, akili ya binadamu inachemka na inaanza kufanya punyeto ya ndani. Kwa hiyo picha za ngono zinakusaidia, zinakupa taswira ya mwanamke mzuri na mwanamme mzuri, zinakupa taswira ya mpenzi wa ndoto yako, zinakusisimua. Mwanamme au mwanamke wako uliyenaye hakupi msisimko wowote. Unapokuwa naye unakuwa kama mfu. Kuna watu, hata ule muda wanapofanya ngono na wapenzi wao, huwa wanawafikiria wanaume au wanawake wengine. Kuna wengine huwa wanafikiria picha za ngono wakati wanafanya ngono na wake au waume zao. Wanaweza kufanya ngono pale tu kwenye akili zao wanapowaza au kutengeneza taswira ya mwanamke au mwanamme mwingine anayemvutia zaidi. Wanaweza kufanya ngono pale tu wanajenga taswira ya picha za ngono. Kuna wengine ili waweze kufanya ngono, ni lazima kwanza waangalie mkanda wa ngono. Ikitokea umeme umekatika, hakuna kitakachoendelea. Wakiwaza au kutengeneza taswira hizi ndipo wanapojikuta wanasisimka zaidi. Katika hali hii, mwanamme hawafanyi ngono na mwanamke wake, mwanamke naye hafanyi ngono na mwanamme wake. Anaweza akawa anamuwaza mtu mashuhuri, muigizaji, mtangazaji au shujaa yoyote wakati wanaendelea kufanya ngono.

Kwa hiyo kila kitanda kina watu wanne, ni wengi sana. Kitanda kimejaa, watu wanne kitanda kimoja. Hakuna mguso wa moja kwa moja kati ya wapenzi hawa, wale watu wanaowafikiria kwenye akili yao wamesimama katikati, wamelala katikati yao. Hebu jiulize, ikitokea mmojawapo akafika kileleni, atafika na yupi? Atafika na huyu aliye naye kitandani au na yule aliye naye kwenye akili yake? Hiki ni kitendawili. Lakini ndipo hali ilipofikia. Unatakiwa ufahamu kwamba, punyeto ni mkengeuko wa ngono bila kujali unaifanya kimwili au kiakili, ni matokeo ya kupotoshwa kwa maana halisi ya tendo la kujamiiana, ni matokeo ya kukandamiza ngono. Punyeto siyo hali ya asili, siyo hali ya kimaumbile. Ushoga na usagaji siyo hali ya asili, siyo hali ya kimaumbile. Mahali popote mambo yanapokwenda kinyume na uasilia, kinyume na maumbile yanavyotaka, upotoshaji hutokea, mikengeuko mbalimbali hutokea. Wanaume wakitengwa peke yao, ushoga hutokea, wanawake wakitengwa peke yao usagaji hutokea, punyeto hutokea, biashara ya picha za ngono hushamiri.

Nguvu ya kujamiiana huchemka ndani, hutaka kutoka, hutafuta mahali pa kutokea vinginevyo watu hawa watachanganyikiwa, watakuwa vichaa. Ni ukatili kuwatenganisha wanawake na wanaume kwani ni kitu kimoja. Lengo la kusema yote haya ni kukusaidia uwe halisi zaidi, ukubaliane na mambo ya asili ya kimaumbile. Tatizo ni kwamba, mambo haya hayawekwi wazi. Unapokimbilia kuangalia picha za ngono ina maana kwamba akili yako haipo katika hali ya kawaida. Ni vizuri kuvutiwa na mwanamke mzuri, hakuna ubaya wowote. Lakini kukaa na picha ya uchi ya mwanamke au mwanamme na kusisimuliwa nayo ni ujinga mtupu. Hivi ndivyo watu wanavyofanya na hizi picha za ngono.

Niliwahi kusoma habari moja kuhusu mume ambaye alikuwa hamwamini mkewe. Jamaa huyu alitafuta mtu akamlipa ili achunguze kama mkewe anatoka nje ya ndoa. Yule aliyepewa kazi hiyo alikuja kuleta taarifa baada ya siku mbili. Alikuwa amevunjika mkono, kichwa chake chote kilikuwa kimefungwa bendeji. Kumetokea nini? Yule mume aliuliza kwa shauku, bado hajapata jibu? Yule mpelelezi akajibu, nilijificha ndani ya nyumba yako baada ya wewe kuondoka asubuhi. Baada ya nusu saa kuna mwanamme mmoja alikuja akamfungulia mlango, akaingia ndani. Ilibidi nipande kwenye mti ili niweze kuona vizuri chumbani kwako. Bahati nzuri dirisha lilikuwa wazi, hivyo nilimuona jamaa na mkeo wakiwa uchi huku wakinong'onezana, kumbe walikuwa wanabusiana. Jamaa akaanza kufanya ngono na mkeo na mimi nikaanza kufanya ngono na mimi nikaanguka chini ya mti. Hivi ndivyo jinsi picha za ngono zilivyo. Inabidi uwe mwangalifu sana na mikengeuko yote ya ngono.

Kupenda ni kuzuri, lakini kuota ndoto ya kupenda ni kubaya. Kufanya ngono na mwanamke au mwanamme ni vizuri, lakini kufanya ngono na picha za ngono au taswira ya mwanamme au mwanamke ni vibaya. Kwa nini ufanye ngono na mwanamme au mwanamke ambaye si halisi? Mbona halisi wapo wengi? Kama mwanamme au mwanamke halisi hawezi kukutosheleza au kukuridhisha, je, huyu ambaye siyo halisi atakuridhisha vipi? Hata huyu halisi, baadaye utakuja kugundua kwamba kumbe na yeye ni mauzauza mtupu. Sasa inakuwaje kuhusu ambacho siyo halisi? Narudia tena, huyo mwanamme au mwanamke halisi uliyevnaye, ipo siku utakuja kugundua kwamba, hata yeye siyo halisi. Mambo yote unayoyakandamiza yanatakiwa yatolewe nje. Kutokana na kuyakandamiza kwa muda mrefu yamegeuka na kuwa sumu.

Kama elimu ya jamii ingekuwa na uwezo wa kukufanya usikandamize na badala yake uyatoe nje mambo haya, ungeyatoa mengi sana. Kwa mfano mtoto anapokuwa na hasira, wazazi huwa wanamwambia ‘usiwe na hasira'. Anaanza kukandamiza hasira. Baadaye jambo hili ambalo lilikuwa la muda mfupi, linakuwa la kudumu. Sasa, mtoto hataonyesha hasira lakini atabaki na hasira. Kwa kawaida hakuna mtu ambaye anaweza kuwa na hasira muda wote labda tu kama amekandamiza hasira. Hasira ni jambo la muda ambalo huja na kuondoka. Kwa hiyo, inabidi tuwaruhusu watoto waonyeshe hasira, wawe na hasira, tusiwazuie. Ikitokea mwanamme hajafanya ngono kwa muda mrefu na mpenzi wake utashangaa kuona mwanamme huyu anakuwa na kisirani sana, anakuwa na hasira za haraka haraka. Hali kadhalika hata kwa mwanamke pia. Lakini wakifanya ngono hasira na kisirani hutoweka. Wanandoa wanaijua vizuri hali hii. Hii hutokea kwa sababu, nguvu hii ya ngono inapokandamizwa au isipotoka hubadilika na kutokea kwenye hasira, kumbuka ni nguvu ileile ya ngono.

Usishangae kukuta mtu mwenye hasira za ziada yuko hivyo kwa sababu ya kukandamiza ngono. Askari yoyote, kama anataka kuwa mpiganaji mzuri vitani, inabidi asifanye ngono wakati wa vita kwani hatakuwa na hasira za kupigana, hatakuwa na nguvu ya kupigana. Nguvu itakuwa imetokea kwenye ngono, ni nguvu hiyohiyo. Mikengeuko yote hii ni matokeo ya imani na mila mbalimbali kukandamiza ngono kwa kusema ni dhambi. Ukweli ni kwamba, hii mikengeuko ndiyo dhambi, ngono siyo dhambi. Maana ya awali au maana halisi ya neno dhambi ni usahaulifu, kutokuwa na urazini au kutokuwa na ufahamu. Lakini neno hili limetumiwa vibaya na imani mbalimbali za dini mpaka maana yake halisi imepotea. Neno dhambi linatumiwa kukupa hofu zaidi, kukutisha zaidi. Kila kitu unachokifanya unaambiwa ni dhambi hata kama ni cha kimaumbile, ndiyo maana hata ngono inasemwa ni dhambi. Kila mahali umebanwa, huwezi kuwa huru na haya maisha. Na maana ya awali ya wema (kinyume cha dhambi) ni kuwa na urazini, kukumbuka au kuwa na ufahamu.

Kwa kawaida ikitokea mwanamme au mwanamke asitoshelezwe kimapenzi, huanza kula sana. Ndiyo maana wanawake wengi baada ya kuolewa huanza kunenepa. Na wanapoanza kunenepa, waume zao huanza kutafuta wanawake wa nje. Na kwa kadri jinsi waume zao wanavyozidi kutafuta wanawake huko nje, ndivyo jinsi na wao wanavyokula zaidi. Hii ni kwa sababu, chakula huwa ni mbadala wa ngono, kwa sababu chakula na ngono vyote vina kazi ya kuendeleza uhai katika maisha. Ukweli ni kwamba wanaume walio wengi huwa hawavutiwi sana na wanawake wanene kwa sababu mwanamke mnene anakuwa amechagua chakula badala ya ngono (nafasi ya ngono imechukuliwa na chakula), havutiwi tena na ngono na badala yake anavutiwa zaidi na chakula. Unene maana yake sina hamu na ngono. Sisemi kwamba kila mara ufanye ngono unapojisikia. Unaweza ukafanya au usifanye. Kama umejisikia kufanya na huhitaji kufanya, nakushauri hali hiyo ikitokea utulie, kama upo ndani funga mlango wako, fanya tahajudi kuhusu hali hiyo.

Ninaposema fanya tahajudi nina maana kwamba, iache nguvu hiyo ipande, usiyaruhusu mawazo yako kuingilia, usihukumu(usiseme nzuri wala mbaya), ila kuwa mtazamaji, kuwa mshuhudiaji wa hicho kinachotokea. Utashangaa baada ya muda, hali hiyo itakuwa imetoweka. Kitakachotokea baada ya hapo ni kwamba, ufahamu wako utakuwa mkubwa sana kuliko ulivyokuwa mwanzo. Kwa upande mwingine ni kwamba, watu wenye hamu kubwa ya kupata mali (utajiri) huwa hawana nguvu ya kujamiiana au wanayo kidogo. Wameikandamiza na hivyo imetokea kwenye kutafuta mali, ndiyo maana huwa hawajali kuhusu wanawake. Kwa kawaida, ngono haipo kwenye viungo vyako vya siri kama watu wengi wanavyofikri. Kuna kituo maalumu kichwani kwako ambacho husimamia viungo vya siri. Kwa hiyo, unapokandamiza ngono viungo vyako vya siri havihusiki.

Kuna baadhi ya watu ambao hukata viungo vyao vya uzazi baada ya kusalitiwa na wapenzi wao au kwa kutaka wenyewe ili wawe watawa. Huu ni wendawazimu kwani hali hii haiwasaidii kuwa huru na ngono kwa sababu kituo kinachosimamia tendo hili kipo kichwani. Kwa hiyo, binadamu atakuwa huru na ngono kama elimu hii itaanza kutolewa hadharani na kwa uwazi zaidi. Hata hivyo, zinahitajika juhudi za ziada kuweza kufanikisha jambo hili, yanahitajika maamuzi magumu sana kwani binadamu amefungwa sana na mazoea, anaishi kwa mazoea. Kabla umeme haujagunduliwa na kufahamika, nguvu hii ya umeme ilikuwepo kama mwanga na ilikuwa inaua watu wengi sana. Lakini kwa sasa umeme umekuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha ya kila siku, umekuwa mkombozi. Bila umeme, shughuli nyingi za mwanadamu husimama. Nguvu ya kujamiiana ni umeme ulio hai, unaua watu wengi sana. Swali kubwa hapa ni jinsi ya kuutumia ili ulete manufaa katika maisha ya mwanadamu.

Hatua ya kwanza ni kukubaliana na nguvu hii ya kujamiiana na siyo kusema halifai, unaposema kitu fulani hakifai, huwezi kukitumia au kukifanyia utafiti. Kwa hiyo, itabidi tukubali kwamba tendo la kujamiiana ni jambo la asili kama ilivyo njaa, kama ilivyo usingizi, kama ilivyo kuvuta hewa, kama ilivyo kujisaidia. Kutokana na kuikataa nguvu hii, tunajikuta tunakataa kila kitu. Hii ni kwa sababu ngono ni mzizi wa kukataa, hivyo ukikataa ngono utakataa mambo mengi sana. Kuna uwezekano mkubwa sana wa kukataa chakula, kukataa nguo, kukataa kazi, na mambo mengine. Hii ni kwa sababu maisha yote ni ngono, kwa kuendelea kuikataa ngono utafika mahali utakataa hata maisha yenyewe, na kitakachofuata ni kujiua kwa sababu hata kupumua ni ngono kwani hupeleka hewa ya oksijeni kwenye chembe chembe zako za mwili kuzipa uhai. Kwa maelezo mengine ni kwamba unapoikataa ngono inakuwa chuki, unapoikubali ngono inakuwa upendo. Upendo na chuki ni sura mbili za ngono. Ukiangalia katika jamii ambazo hazijaendelea, huwezi kukuta makahaba au kama wapo ni wachache sana. Lakini jamii zilizoendelea makahaba ni wengi sana. Hii ni kwa sababu jamii zilizoendelea zimekandamiza sana ngono kwa visingizio vya dini (dhambi), masomo, kujijenga na kadhalika. Asilimia ya watu wanaokandamiza ngono ni kubwa zaidi katika jamii zinazoishi mijini ukilinganisha na zile zinazoishi vijijini.

Kutokana na hali hii ya kuendelea kukandamiza ngono, imefika mahali hata pua zetu haziwezi kunusa ipasavyo. Hii ni kwa sababu ngono na harufu vina uhusiano wa moja kwa moja. Ndiyo maana wanyama hawafanyi ngono bila dume kunusa sehemu za siri za jike au mkojo. Kuna harufu ambayo huwaunganisha pamoja, huwafanya wawe kitu kimoja. Harufu hii kama ipo inamaanisha pia kwamba, jike liko tayari kujamiiana. Kama hii harufu haipo, ngono haiwezi kufanyika. Kwa hiyo, unapokandamiza ngono ufahamu pia kwamba uwezo wako wa kunusa nao unaukandamiza. Wanamke wanapokuwa kwenye kipindi cha kupevuka kwa yai, huwa wanatoa harufu hii. Lakini wanaume hawawezi tena kuisikia harufu hii kutokana na kukandamiza sana ngono hali iliyopelekea pua zao kupungukiwa na uwezo wa kunusa. Wale ambao hawajakandamiza ngono huwa wanaisikia harufu hii. Kwa hiyo, ngono inayofanyika bila uwepo wa harufu hii siyo tamu, haiwezi kuwa tamu. Inakosa mawimbi ya harufu ambayo ingewaunganisha na kuwa kitu kimoja (mwili mmoja) angalau kwa huo muda mfupi wa kujamiiana. Harufu hii ikiwepo wakati wa kujamiiana, ngono huwa ni tamu sana.
 

SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
1,750
Ngoja nilale kwanza Mtambuzi ..nimesoma nusu naona ukungu wa machoni..ntamalizia kesho na ntachangia io kesho..lol
 
Last edited by a moderator:

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000
Imekaa vizuri sana
je,kupiga chabo nayo ni madhara ya kukandamiza ngono??
Mkuu kuna tofauti gani kati ya kupiga chabo na kuangalia picha za ngono?
Ni kitu kile kile tofauti ni kwamba chabo ni live na picha za ngono ni mikanda iliyorekodiwa, yaani sio live............
 

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,999
2,000
mkuu kuna tofauti gani kati ya kupiga chabo na kuangalia picha za ngono?
Ni kitu kile kile tofauti ni kwamba chabo ni live na picha za ngono ni mikanda iliyorekodiwa, yaani sio live............

thank you for the lesson mtambuzi
ila naona kama imekwepa kidogo maandiko matakatifu
but,the lesson is good..
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000
Mie nakandamiza sana kuliko nigawe ka pipi bora nikandamize lol
Uzuri ni kwamba madhara ushayajua kwa hiyo usije laumu bure, maana ukweli unaujua lakini unafanya ajizi.
Sijasema ugawe kama pipi, (Umeninukuu vibaya) nimesema pale unapohitaji fanya na yule umpendaye, msinyimane mtasababisha kutawaliwa na hasira zisizo na mashiko wakati sababu mnazijua................

We fanya tu binti wala usiogope, fanya kwa raha zako
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
2,000
thank you for the lesson mtambuzi
ila naona kama imekwepa kidogo maandiko matakatifu
but,the lesson is good..
Maandiko matakatifu yanakataza ngono, hivyo kuzungumzia ngono na kuihusisha na maandiko matakatifu ni kutaka kuwakwaza watu.
 

Hoshea

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,287
2,000
phew, meen that's a long thread brother ntamalizia kesho, couldn't finish lkn nmekuelewa ni bonge la concept a real one, kitu ikipigwa marufuku ndo watu huwa curious about it in a big extent, but kiukweli be it God through the bible, quran etc au wise genious ancestors walokandamiza ngono toka enzi hizo, salute them all, just imagine hii dunia ya sasa ngono isingepigwa marufuku ingekuwaje ase, tungekuwa wengi mnoo
 

Asnam

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
4,259
1,225
dah ngoja niweke alarm asubuhi nidamke kuimalizia why Mtambuzi unaandika ndefu hivi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom