G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Wewe Waziri wa Afya kweli ni mwanamke unayejua uchungu wa mtoto? Kwenye janga hili la Corona unafuata muongozo upi ambao unaelekea kuiua Tanzania?
Tumechoshwa na habari za aina hii kila siku. Pia nikueleze kuwa tunachoshwa na madhila tunayoyaona huku mitaani. Hatujazoea kuishi na maiti sisi! Kama unaona huwezi kufuata mwongozo sahihi kuukabili huu ugonjwa basi ondoka ili tujue tutachukua hatua gani.
Umefikia hatua sasa unatukera waziwazi!

Madereva 25 kutoka Tanzania wamezuiwa kuingia nchini Kenya baada ya kukutwa na virusi vya corona.
Kati ya madereva hao 23 ni raia wa Tanzania , mmoja wa Uganda na mmoja kutoka taifa la Rwanda.
Kulingana na wizara ya afya nchini Kenya raia hao wa taifa jirani la Tanzania walipimwa na kupatiwa matokeo yao katika kipindi cha saa 24.
Wizara hiyo imesema kwamba hatua hiyo inalenga kuwalinda Wakenya dhidi ya maambukizi kutoka kwa raia wa kigeni.
Katika mkutano wake na wanahabari naibu waziri wa Afya rashid Aman amesema kwamba maabara 2 za kuhama hama zitazinduliwa katika mpaka wa Namanga ili kuimarisha upimaji wa wagonjwa wapya.
Aman aidha amewataka Wakenya wanaoishi mipakani kuwaripoti watu wanaowashuku ambao wanajaribu kuingia nchini kwa njia haramu.