Madereva wanaoendesha magari aina ya Subaru na Alteza

Umri wao wengi ni kati ya 25-35 yrs, walioko above hapo wachache sana humiliki gari za vurugu kama hizi.

Kati yao, mabishoo ndio wengi ila wastaarabu ni wachache kuanzia mavazi mpaka uendeshaji.

mzee kwahiyo nikaweke sokoni hichi kigari sio mbona daaah maneno yameshakuwa mengi
 
Ila wengi wao wana tabia zote mdau alizozitaja...


Nitatoa mfano halisi kilichotokea mwezi uliopita..

Tumeenda sehemu nikapaki usafiri wangu kama wengine walivyopaki kufuatana na maelekezo ya mlinzi wa pale..tuakaendelea na kilichotupeleka hapo..

Wakati naondoka nikakuta Alteza imepaki vibaya, sikuwezi kutoka..nikawaomba wahudumu wamwambie jamaa asogeze gari...mhudumu akarudisha jibu jamaa hajigusi wala hajibu kitu...

Meneja wa sehemu hiyo akaenda mwenye, kakanyanyuka kajamaa kamenyoa kiduku, mezani kameweka K vanti, suruali mnyonyo...kanavyotembea sasa nikadhani anakuja kuwasha Range Rover sport ya 2019.

Akawasha Alteza yake, akapiga resi kile kibuyu pale nyuma kikaharibu usikivu, basi akaipaki pembeni.....nikaondoka zangu..

Hawa watoto wakishaendesha hizo gari, wakazifunga vibuyu kwenye exhaust, wanahisi wameshamaliza maisha yote.

 
kwanini mkuu gari ni gari

Ni kweli Mkuu kuwa gari ni gari tu lakini kuna gari zinahitaji kuendana na status ama heshima ya mtu ktk jamii.

Ni kama vile kusema mavazi ni mavazi tuu, kisha mtu mzima mwenye staha ukavaa tight jeans zile za kuchanwa chanwa, micheni mikubwa mikubwa na mapete vidole vyote kumi..

Hii lazima jamii ikuchulie kitofauti sana..
 
Hawa vijana ni bange sana kwa kweli hahahaaa..
Wengi wao haya ndiyo mapigo yao...
Na walio wengi ndani ya gari hakosi maji kubwa, K vanti au konyagi na miraa..
2630123_FB_IMG_16069341487177469.jpg
 
Upo sahihi Mkuu ingawa kwa mtu mzima/ wa umri mkubwa na mstaarabu nikimuona anendesha magari ya aina hiyo yaani huwa namfikiria kitofauti sana.
Aina ya gari ni chaguo la mtu.mazingura nk
Si ajabu Apo ulipo unasaga soli lkn unamshangaa mtu alienunua subaru kisa ni mtu mzima.
Usipende maishA yako yawe magumu kisa ni mitazamo ambayo haina uhalisia wwte.
 
Back
Top Bottom