Polisi: Baadhi ya madereva wa magari ya Serikali huwa ni chanzo cha ajali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, SSP Zauda Mohamed amesema baadhi ya madereva hao wamekuwa hawazingatii sheria, Kanuni na taratibu.

Ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa madereva wa magari ya Serikali Mkoani Morogoro ambapo amewataka wale wanaoendesha viongizi wakubwa Serikalini kuacha kuvunja Sheria za barabarani kwa makusudi jambo ambalo linahatarisha usalama wa maisha, mali na miundombinu ya barabara.

Aidha, SSP Zauda amesema sababu nyinginze zinazosababisha ajali za barabarani ni sababu za kibinaadamu, ubovu wa magari na changamoto za miundombinu za barabara.
Fn8p3hRX0AA8MKM.jpg

Madere.jpg

Madereva.jpg
 
Wapuuzi sana baadhi ya madereva serikalini, leo asubuhi Kuna gari ya serikali ilifanya overtaking sehemu hatarishi kabisa 😡
 
Wapuuzi sana baadhi ya madereva serikalini, leo asubuhi Kuna gari ya serikali ilifanya overtaking sehemu hatarishi kabisa
Dereva wa serikali akishaendesha gari la serikali anahisi nayeye ni serikali.

Mi ningeshauri elimu ya kuajiriwa kuwa dreva wa serikali wangeanzia walau elimu kidato cha 6 au diploma.

Hawa std 7 na form4 huwa akili zao hazina tfauti na madereva wa vifidi pale Arusha
 
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, SSP Zauda Mohamed amesema baadhi ya madereva hao wamekuwa hawazingatii sheria, Kanuni na taratibu.

Ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa madereva wa magari ya Serikali Mkoani Morogoro ambapo amewataka wale wanaoendesha viongizi wakubwa Serikalini kuacha kuvunja Sheria za barabarani kwa makusudi jambo ambalo linahatarisha usalama wa maisha, mali na miundombinu ya barabara.

Aidha, SSP Zauda amesema sababu nyinginze zinazosababisha ajali za barabarani ni sababu za kibinaadamu, ubovu wa magari na changamoto za miundombinu za barabara.
Hapo Morogoro askari akienda tu akili zinamuisha.
Kwa taarifa tu tusome alama za nyakati RTO yeyote aliyetoa tamko kupambana na MADEREVA WA SERIKALI na kuwasemea mbovu aliondolewa mapema sana au alibadilishwa kituo haraka. Hao madereva anaosema ndio hao hao wanamwwndesha IGP, RAIS nk wakikusagia kunguni humalizi wiki.
Hebu tuchunge ndimi zetu.
Kwanza ni Uongo tu, Fleet size ya seikali ni gari 8000 na zaidi. Je ratio ya ajali kwa ukubwa huo wa magari ikoje?
Abood ana Vigari labda 60 je ratio ya ajali ikoje mpaka huyo askari aanze kulaumu magari ya serikali ambayo yeye pia ni mtumishi wake. Huna akili uondolewe tuu
 
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, SSP Zauda Mohamed amesema baadhi ya madereva hao wamekuwa hawazingatii sheria, Kanuni na taratibu.

Ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa madereva wa magari ya Serikali Mkoani Morogoro ambapo amewataka wale wanaoendesha viongizi wakubwa Serikalini kuacha kuvunja Sheria za barabarani kwa makusudi jambo ambalo linahatarisha usalama wa maisha, mali na miundombinu ya barabara.

Aidha, SSP Zauda amesema sababu nyinginze zinazosababisha ajali za barabarani ni sababu za kibinaadamu, ubovu wa magari na changamoto za miundombinu za barabara.
tatizo hakuna wa kuwatoza faini polisi wakiona gali lenye namba za serikali wanajificha
 
Back
Top Bottom