Madenge alivyoitikisa Tanzania

Madenge alivyoitikisa Tanzania

Daah, Harakati za Pimbi! Ni balaa, Nilijua ni real aisee. Nahisi Pimbi ashapata Manzi siku hizii..
Pimbi kila akiseti mipango inayumba tu🤣🤣🤣...Mara kaangukiwa na nazi, mara kaporwa demu. Hahahah sema maisha yaliakisiwa sana na zile katuni.Sio rahisi kwa leo vile visa ku make sense. Mitandao ime take over almost kila kitu.
 
Jamaa alikuja darasani mida ya saa 2 asubuhi na mizuka ya hatari " Jamani madenge,pimbi,ndumilakuwili wamekuja tabora Leo watakuwa uwanja wa mwinyi" Darasa zima lilitimka kwenda uwanjani watu wakawa wanashangaa hawa watoto vipi..!?
 
Nakumbuka siku moja ndumilakuwili alikamatwa kwa wizi kajitetea wapi, wananchi wanahasira na mapanga mashoka wameshika nikajua leo wanamuua balaa lake aliwageuka aliwapa mbata kila mtu alimpiga na silaha yake akakimbia

Madenge siku moja akaambiwa na mwalimu akalete mzazi kwa nin hataki kujibu maswali akaondoka anarudi nyumbani anawaza "huyu mdingi sasa nitamwambia nin anielewe lakini ngoja nifike" akafika akamwambia mzee unaitwa na mwalimu shule wakafika kwa mwalimu, mwalimu anamwambia baba madenge mwanao hataki kujibu maswali darasani baba ake akamuuliza madenge kwa nini hujibu, Madenge akamwambia baba ake "Mwalimu alikua ananiuliza kama baba wewe ni shoga mimi nitajibuje? Mwalimh alikula mbata za hatari.

Mzee kifimbo cheza wa kurekebisha lugha, amezoea anawavizia kwenye kona anawavuta na ile bakora yake anawatandika fimbo za kutosha siku hiyo wanaongea lugha zao wanataka kukimbia akadakwa mmoja kwenye uchochoro akamlaza amchape kumbe mmoja amejificha kwa juu ya ukuta alimteremshia mzee kifimbo tofali la kichwa akamwambia sema nalo hilo hahahhaa nilifurahi sana nikajua amekufa mara namuona toleo lingine
Hahah mzee kifimbo cheza alikuwa ananifurahisha sana maana lugha za kibaharia ndio zilikuwa zinatamba. Utaskia bondeni manaake South Africa, kudondoka maana yake kwenda kule hahahah af baada ya kujieleza wahuni wanakula mikwaju ya hatari🤣🤣🤣🤣
 
Hii ndio sababu pekee ilinifanya kuwa nanunua gazeti la sani na lile jarida.

Nawakumbuka sana
Pimbi
Mapacha (akina chogo)
Ndumila kuwili
Zena na Betina (chibonge na kimbau mbau)
Sokomoko
Kipepe
Lodi lofa (kiboko ya waswahili)
Wale wahuni na kifimbo cheza(kifimbo cheza na wachafuzi wa lugha)
Waandishi na wachoraji walikimbiza sana miaka hiyo. Hivi bado lipo kweli?? Yan gazeti liliuza sana
 
MR x zungu LA unga ilikuwa kwenye jarida LA bongo bila kusahau simulizi ya kuwadi
Yeah Bongo lilikuja ku'take over baada ya Sani kuanza kupotea
Humo kulikua na Riwaya za Msako wa Mr.X; Msako wa Hayawani; Dunia Gunia;....walitokea watukutu km kina Mark Steven Chenje na watunzi mahiri km kina Aloyce James &Aloyce Jacob
All in all Sani ilikua kiboko ya yote
 
Hivi anguko la majarida haya chanzo ni nini hasa?
Kizazi kubadilika pamoja na kuja tugazeti twa bei rahisi tulikokuwa tunatoka kila wiki tofauti na jarida la Sani lililokuwa linatoka kwa vipindi,sikumbuki vizuri ila lilikuwa linatoka baada ya mwezi au miezi miwili.

Mwaka 1996 mjomba wangu nakumbuka alinipa Tsh600 au 900 nikamnunulie Sani kipindi hiko siyo hela ndogo vilipotoka vigazeti vya mia mia vilivyosomwa kila wiki vikawatoa kwenye chuck.
 
Yeah Bongo lilikuja ku'take over baada ya Sani kuanza kupotea
Humo kulikua na Riwaya za Msako wa Mr.X; Msako wa Hayawani; Dunia Gunia;....walitokea watukutu km kina Mark Steven Chenje na watunzi mahiri km kina Aloyce James &Aloyce Jacob
All in all Sani ilikua kiboko ya yote
bila kusahau jasusi la kike
 
Shukurani ya kumbukumbu hizi imwendee Marco Tibasima anayeamsha vionjo vya kuzikumbuka enzi zetu tukilifurahia gazeti la Sani kwa simulizi maarufu kama Maji Mazito by S.M.M. Bawji, kulikuwa na Lodi Lofa, mpambano wa Zena na Betina unaosababishwa na Pimbi, mechi za soka kati ya timu mahasimu Born Town na Bush Stars, vituko vya Kipepe, Madenge...

Michoro marufu ya mwana sanaa Raza Mohamed, Philip Nduguru, John Kaduma, Ted Marealle, Chritian Gregory ' Chakubanga', Douglas Mpoto, Kibonge S. Kibenga 'Majoka', Raza Mohamed, Hayati 'King' Marco Mussa, Ibra Radi Washokera, Chris Katembo, Hayati John Mathias Kaduma 'Fogasta', Ali Masoud Kipanya, Paul Ndunguru, Marco Tibasima, James Gayo, Cloud Chatanda, Fortunatus Ndilla ' Mtaalam'
Kumbe Kipanya katoka mbali.
 
Back
Top Bottom