Habari zenu !!
Ebwana leo nimeona tumzungumzie kipenzi cha watanzania walio wengi aliye julikana kama MADENGE , aliye kuwa akiishi kupitia fikra za mtunzi (àmbaye kwa sina kumbukumbu nzuri alikuwa nani)
.
Kiukweli huyu bwana alipendwa kuliko hata baadhi ya viongozi wengi wa ki serikali ukiachia mbali J. K NYERERE
Licha ya kupata ushindani kutoka kwa wapinzani wake kikazi hapa nawazungumzia akina KIPEPE, PIMBI ,LODI LOFA , Lakini bado hili halikumfanya apotee zaidi ya kuongeza ubunifu kila uchwao kazi yake kuu ilikuwa ni kuhakikisha watanzania ni watu wenye furaha muda wote
Hapa nadhani haya majarida yanayotoa orodha ya mataifa yenye furaha yange fanya. Tafiti zile kipindi cha zama za huyu bwana basi. Isingelikuwa ajabu kwa Tanzania kushika namba za juu.
Wanafunzi wa wakati ule tulitamani siku ikuche ili tukasimuliane habari za mtu huyu kule mashuleni tofauti na ilivyo. Sasa watoto wako bize na season
Kabla ya hizi mambo za mtandao na kiki ,vijiweni habari kuu alikua huyu bwana
Najua wengi mtashangaa mbona namuelezea kama binadamu
Naam hii ni kwa sababu ya umaarufu na mizinguo yake ilifika kipindi Watu wa mikoani tuliamini Madenge anaishi Dar es Salaam, huko vijijini pia taarifa walizokuwa wakizipata na kuziamini ni kuwa madenge yupo mjini.
Uhusika wake ulivutia sana watoto nadhani hii ingeendelea ingetengeneza kizazi cha watoto wenye utamaduni wa kujisomea (Kama ambavyo watu wanapigia kelele jambo hili)
Lakini kipindi kile bila ya kulazimishwa na mtu tulitafuta magazeti kila kona alipo yahifadhi mzee
Najua ingekuwa ni marekani basi Hollywood wangefanya kitu ila kwakuwa ni Tanzania
REST IN PEACE MADENGE childhood hero