Kila mtu kwa imani yake aiombee Tanzania 🇹🇿

Kila mtu kwa imani yake aiombee Tanzania 🇹🇿

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
14,989
Reaction score
36,511
UMEVUKA SALAMA?

Kama umevuka kipindi hiki kigumu, tafadhali tujulishe kwamba uko salama na tuendelee kuwaombea wenzetu.

Watu wengi wameumia na kupoteza wapendwa wao, Kwa imani yako na bila kujali itikadi za kiasiasa, tuiombee Tanzania 🇹🇿 yetu!

Our Tanzanian flag.jpg


  • Tuwaombee wenye madaraka wapewe busara na unyenyekevu unaohitajika katika kipindi hiki.

  • Tuwaombee wote wenye maumivu ya kupoteza ndugu zao kwa dhuluma na ukatili wakapate faraja na haki wanazostahili.

  • Tuwaombee wale wanaotoka kupigania wanachokiamini wawe salama wasidhurike.

  • Tuiombee nchi yetu, nchi ya watoto wetu na ya vizazi vyetu isije kuingizwa kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.

  • Tuombee umoja usiotetereka wenye kuweka nchi kwanza badala ya kikundi au vikundi vya watu wachache.
 
aisee tunatikii oktobaa
Bwana naomba utete nao,
Wale Wanaoteta nami

Naomba upigane na adui zangu wote

Mimi sitaki kubishana nao,
Sitaki kupambana nao,
Nisije nikakosea wakanilaumu

Maana wameshavuta upinde,
Wapo kwenye mangojeo yao

Wamenuna wamekunja sura wana hasira nami,
Kinachowafanya wasinidhuru ni kwamba hawajapata sababu

Wanahesabu hatua zangu, nikosee waninase
Usiache mguu usogezwe, ninaswe kwenye mitego yao

Weka mngojezi kinywani mwangu anilinde nisiropoke

Ombi langu - Ambwene Mwasongwe
 
To every action there’s an equal and opposite reaction, umetetea ushenzi wote wa Samia na genge lake bila huruma kwa waliotekwa na kuuliwa, pushbacks kidogo tuu uharo unawatoka mnataka maombi, glad akili imerudi lakini damage mliyowafanyia watu ni ya maisha, ombea amani na mabadiliko
 
Tumesha omba sana mkuu, ingawa maombi ama kuomba hakuna mwisho ila wala kikomo ila sala , dua, mifungo, maombi ya mkesha, novena nk.
Acha wakati uamue na kusudi la Mungu liwe.
Kusema ukweli athari ni kubwa mno haswa huku dar es laam, kiasi hali inaogopesha ila tumaini la kesho nzuri lipo.
 
To every action there’s an equal and opposite reaction, umetetea ushenzi wote wa Samia na genge lake bila huruma kwa waliotekwa na kuuliwa, pushbacks kidogo tuu uharo unawatoka mnataka maombi, glad akili imerudi lakini damage mliyowafanyia watu ni ya maisha, ombea amani na mabadiliko
Kijana, naona unanifuata fuata kwenye kila uzi.
Ni wapi umeshaniona namtetea huyo mama? Naomba usinihusishe na mambo ya kipumbavu!
 
Back
Top Bottom