Madenge alivyoitikisa Tanzania

ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,317
1,229
Habari zenu !!

Ebwana leo nimeona tumzungumzie kipenzi cha watanzania walio wengi aliye julikana kama MADENGE , aliye kuwa akiishi kupitia fikra za mtunzi (àmbaye kwa sina kumbukumbu nzuri alikuwa nani)
.
Kiukweli huyu bwana alipendwa kuliko hata baadhi ya viongozi wengi wa ki serikali ukiachia mbali J. K NYERERE

Licha ya kupata ushindani kutoka kwa wapinzani wake kikazi hapa nawazungumzia akina KIPEPE, PIMBI ,LODI LOFA , Lakini bado hili halikumfanya apotee zaidi ya kuongeza ubunifu kila uchwao kazi yake kuu ilikuwa ni kuhakikisha watanzania ni watu wenye furaha muda wote

Hapa nadhani haya majarida yanayotoa orodha ya mataifa yenye furaha yange fanya. Tafiti zile kipindi cha zama za huyu bwana basi. Isingelikuwa ajabu kwa Tanzania kushika namba za juu.

Wanafunzi wa wakati ule tulitamani siku ikuche ili tukasimuliane habari za mtu huyu kule mashuleni tofauti na ilivyo. Sasa watoto wako bize na season

Kabla ya hizi mambo za mtandao na kiki ,vijiweni habari kuu alikua huyu bwana
Najua wengi mtashangaa mbona namuelezea kama binadamu
Naam hii ni kwa sababu ya umaarufu na mizinguo yake ilifika kipindi Watu wa mikoani tuliamini Madenge anaishi Dar es Salaam, huko vijijini pia taarifa walizokuwa wakizipata na kuziamini ni kuwa madenge yupo mjini.

Uhusika wake ulivutia sana watoto nadhani hii ingeendelea ingetengeneza kizazi cha watoto wenye utamaduni wa kujisomea (Kama ambavyo watu wanapigia kelele jambo hili)
Lakini kipindi kile bila ya kulazimishwa na mtu tulitafuta magazeti kila kona alipo yahifadhi mzee

Najua ingekuwa ni marekani basi Hollywood wangefanya kitu ila kwakuwa ni Tanzania
REST IN PEACE MADENGE childhood hero
 
Habari zenu !!

Ebwana leo nimeona tumzungumzie kipenzi cha watanzania walio wengi aliye julikana kama MADENGE , aliye kuwa akiishi kupitia fikra za masoud kipanya.
.
Kiukweli huyu bwana alipendwa kuliko hata baadhi ya viongozi wengi wa ki serikali ukiachia mbali JK NYERERE

richa ya kupata ushindani kutoka kwa wapinzni wake kikazi hapa nawazungumzia akina ,KIPEPE,PIMBI ,LODI. LOFA , Lakini bado hili halikumfanya apotee zaidi ya kuongeza ubunifu kila uchwao kazi yake kuu ilikuwa ni kuhakikisha watanzania ni watu wenye furaha muda wote

Hapa nadhani haya majarida yanayotoa orodha ya mataifa yenye furaha yange fanya. Tafiti zile kipindi cha zama za huyu bwana basi. Isingelikuwa ajabu kwa. Tanzania kushika namba za juu

Wanafunzi wa wakati ule tulitamani siku ikuche ili tukasimuliane habari za mtu huyu kule mashuleni tofauti na ilivyo. Sasa watoto wako bize na season

Kabla ya hizi mambo za mtandao na kiki ,vijiweni habari kuu alikua huyu bwana
Najua wengi mta shangaa mbona namuelezea kama binadamu
Naam hii ni kwa sababu ya umaarufu na mizinguo yake ilifika kipindi Wa mikoan tuliamini Madenge anaishi dar es salaam, huko vijijini pia taarifa walizo kuwa wakizipata na kuziamini ni a kuwa madenge yupo mjini..
.
Uhusika wake ulivutia Sana watoto nadhani hii ingeendelea ingetengeneza kizazi cha watoto wenye utamaduni wa kujisomea (Kama ambavyo watu wanapigia kelele jambo hili)
Lakini kipindi kile bila ya kulazimishwa na mtu tulitafuta magazeti kila kona alipo yahifadhi mzee

Najua ingekuwa ni marekani basi hollywood wangefanya kitu ila kwakuwa ni Tz
REST IN PEACE MADENGE chilhood hero
Fix zako. Mchoraji wa Madenge siyo Kipanya. Madenge alikuwa natoka kwenye gazeti la Sani.
 
Lodi Lofa na Sokomoko
IMG-20170905-WA0036.jpeg
 
Hii ndio sababu pekee ilinifanya kuwa nanunua gazeti la sani na lile jarida.

Nawakumbuka sana
Pimbi
Mapacha (akina chogo)
Ndumila kuwili
Zena na Betina (chibonge na kimbau mbau)
Sokomoko
Kipepe
Lodi lofa (kiboko ya waswahili)
Wale wahuni na kifimbo cheza(kifimbo cheza na wachafuzi wa lugha)
 
Shukurani ya kumbukumbu hizi imwendee Marco Tibasima anayeamsha vionjo vya kuzikumbuka enzi zetu tukilifurahia gazeti la Sani kwa simulizi maarufu kama Maji Mazito by S.M.M. Bawji, kulikuwa na Lodi Lofa, mpambano wa Zena na Betina unaosababishwa na Pimbi, mechi za soka kati ya timu mahasimu Born Town na Bush Stars, vituko vya Kipepe, Madenge...

Michoro marufu ya mwana sanaa Raza Mohamed, Philip Nduguru, John Kaduma, Ted Marealle, Chritian Gregory ' Chakubanga', Douglas Mpoto, Kibonge S. Kibenga 'Majoka', Raza Mohamed, Hayati 'King' Marco Mussa, Ibra Radi Washokera, Chris Katembo, Hayati John Mathias Kaduma 'Fogasta', Ali Masoud Kipanya, Paul Ndunguru, Marco Tibasima, James Gayo, Cloud Chatanda, Fortunatus Ndilla ' Mtaalam'
 
Back
Top Bottom