adakiss23
JF-Expert Member
- Jan 23, 2011
- 4,511
- 4,308
Ni kweli mkuu. Kuna dogo mmoja alikuwa mwizi wa boda anatumia mademu kukodisha boda then wanamkaba na kupora. Baada ya hapo ni matanuzi na sherehe mtaani. Bia kama zote. Kuna jamaa polisi mtaani akamfuata akamwambia dogo acha hizi issue kabisa nakwambia kama mdogo wangu. Dogo akajiapiza pale braza sijui nmeacha sijui blah blah nyingi. Jamaa akaondoka. Haijapita siku 3 dogo kauawa nadhani makongo juu walikuwa wanaenda kuvunja godown. Ilitangazwa hata kwenye Media walikuwa katika noah nadhani wanaelekea kwenye tukio.Mkuu watu wanafanya kazi 2 mbili kawaida tu.
Mchana kkoo,jioni anashika mapanga kwenda kupora.
Ukiona polisi wamedeal nae kimyakimya Ujue wanamtambua vizuri tu,
Tusiwalaumu.
Raia Wema wanatoa info toka hapo mtaani wanakokaa.
Kesi zikiwa nyingi inakua kero maana wao wataonekana hawatimizi wajibu wao.
Ndio mwisho wanakupeleka kusikoeleweka.
Na siku hiyo anakufa alikuwa grocery ya mtaani anakula bia mida ya saa 7,8 hivi akaacha washkaji zake akasema naarudi muda si mrefu kumbe ndo anaaenda kula chumba.
So hizi issue polisi wanajua vizuri tu. Ingekuwa polisi wanadeal nazo kisawasawa vijana wengi wangeshazikwa ila huwa wanatoa muda wa kumtaka ajirekebishe