MADALE: Kero ya Kukatiwa maji bila maelezo na kijana wa DAWASCO

Annonymous

JF-Expert Member
May 9, 2013
448
799
Habari wana JF.

Niende moja kwa moja kwenye kelo yangu juu ya Dawasco.

Kumekuwa na changamoto ya kukatiwa maji mara kwa mara na baada ya kukata huyu kijana hatoi maelezo kwa mhusika. Akishakata huwa anadai 15000 kurejesha maji. Navyoelewa mteja anatakiwa kupewa taarifa ya mdomo kisha barua ya maandishi kabla ya kukatiwa maji ikiwa anadaiwa au hadaiwi sio kukata tu ili mladi na kudai elf 15. Huu umeshakuwa mladi wake.

Je, ni sahihi kwa hawa wafanyakazi wa DAWASA kukata kata maji hovyo tu pasi na taarifa yoyote kwa wenyeji (mwenye nyumba) anayemkuta hapo na kudai elf 15 ili kurudishiwa na hiyo 15000 inapokelewa mkononi sio control number (GePG)??

DAWASA
 
Habari wana JF.

Je ni sahihi kwa hawa wafanyakazi wa dawasa kukata kata maji hovyo tu pasi na taarifa yoyote kwa wenyeji (mwenye nyumba) anayemkuta hapo na kudai elf 15 ili kurudishiwa na hiyo 15000 inapokelewa mkoni sio control number (GePG)??

DAWASA

Kuna jamaa alinileteaga hizo chuki, hawezi sahau, hata siku moja, na hatothubutu tena.
 
Kuna jamaa alinileteaga hizo chuki, hawezi sahau, hata siku moja, na hatothubutu tena.
Ulimfanyaje niambie mana huku kwetu ushakuwa mladi ukivusha mwezi mmoja ni tatizo. Kuna mwezi niliwahi kumpa wakala akalipia halafu nkaondoka zangu nlikuwa nadaiwa 1400 (elf 1 na mianne) kumbe yule wakala hakulipa mwezi unaofata nilikatiwa kuuliza eti nadaiwa. Kvp nkawapigia wakasema nadaiwa mwezi nmoja kufuatilia wakala hajalipa. Sasa jama kama kawaida yake kunrejea akataka elf 15000 nimlipe aunge maji nayodaiwa elf moja na mianne.

Yani nilipe elf 15 kwasababu nadaiwa elf 1 na mia4. Nilitaka kumpiga akafungua ila naona round hii ameanza tena bili ninelipa sa9 baada ya mke wangu kunikumbusha yeye kaja kufunga saa11 jioni. Sasa si niugomvi huu. Niambie ulifanya nn naona kila mtu anamlalamikia huyu kijana
 
Dawa ya deni ni kulipa

Ova
Tatizo sio bili kulipa we unaweza kumkatia mtu maji alipe faini 15000 kisa anadaiwa elf moja na mia point?

Je kma nadaiwa amemwambia nani kuwa nadaiwa, namba zangu anazo kwanini hajanipigia au kutuma ujumbe kuwa nadaiwa elf moja na shingapi kwahiyo ananikatia.

Amekuta familia yangu nbona hajaiambia sababu zaidi ya kuianbia nimekata maji nikirudi niambiwe tu nimekatiwa maji sababu hakusema lolote.

Yani kupewa nyundo ndio uvunjie makufuli ya watu eti kwasababu unacho kivunjio
 
Mods tusiharibiane uzi. Nineweka namba zake hapa ili ajulikane aambiwe. Sasa mmeedit uzi mmeweka neno huyu kijana. Kijana yupi wakati hakuna jina lake wala maelezo yoyote ya kumtanabaisha.
Halafu mmefunga edit option sasa inamaana gani ya kutoa taarifa hii kwa Dawasa

Nimetaja ni DAWASA sio dawasco. Kwasababu zamani ilikuwa inaitwa ni kampuni ya kusambaza maji " dar es salaam water supply company" kwasasa ni mamlaka ya kusambaza maji na maji taka "Dar es Salaam Water and Sewerage Authority (DAWASA" ninyi mnatoa dawasa ya sasa hivi mnaweka dawasco wakati dawasco ilishakufa ikafanywa dawasa. Inanaana huu uzi hauihusu dawasa tena ni dawasco. Sehemu zingine mnataja dawasa sehemu zingine dawasco yani uzi ni vurugu tu hauna maana yoyote haieleweki anazungumzwa dawasa au dawasco

Hizo edits zenu zinafanya uzi kuwa hauna maana zinaharibu na kugeneralize tatizo as if ni wafanyakazi wote wa DAWASA wakati ni mmoja tu mwenye shida hiyo

Namba za huyo kijana anayefanya hivyo ni +255xx672958 na 07xx 609 929

Kwenye title nimeeleza ni bila taarifa wala maelezo. Mmetoa neno taarifa mmeacha maelezo. Suala ni taarifa kwa mhusika anayekuwepo sio maelezo. Maelezo ya k2 gani. Mimi nataka taarifa kuwa nakatiwa maji kwasababu fulani sio maelezo ndio maaana nikasema pale juu taarifa wala maelezo vyote vina maana tofauti haya maneno
 
Mod aliyefanya editing ya andiko lako ana uwezo mdogo wa kuelewa mambo. Ijapokuwa alijifanya anaelewa mambo kwa upana wake.

Maxence Melo tafuteni vijana wenye uelewa mkubwa wa mambo! Aliye-hariri andiko la mleta mada amethibitisha mnavyoajiri watu wasio sahihi.

Hata kama andiko likashachapishwa hapa ni mali yenu mnapaswa kuwa makani na kero/malalamiko yanayotolewa na wanajukwaa.

Wanajukwaa wamewaamini, kubadilisha maudhui hakumsaidii aliewasilisha andiko hilo.

Vijana wako wanakwaza!

Asante.
 
Back
Top Bottom