DOKEZO Madaktari Watarajali Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro tunadhalilika mitaani kwa kucheleweshewa posho za kujikimu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Sisi Watarajali (Interns) wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Hospitali ya Mawenzi) tunapitia katika changamoto zenye kuleta ugumu mkubwa katika maisha yetu ya kulitumikia Taifa katika kutoa Huduma za Afya.

Tunapambana kwa juhudi kubwa katika kutoa Huduma za Afya hapa hospitalini licha ya kuwa na mazingira magumu ya utendaji kazi.

Tumekuwa tukipata shida sana kupatiwa stahiki zetu za Posho ya Interns ya kila mwezi, ambazo zipo kwa mujibu wa Sheria, kumekuwa na desturi ya ucheleweshwaji mkubwa wa malipo ya posho zetu kila mwezi, ambapo huingiziwa posho zetu mwenzi wa mbeleni, tena tarehe zilizopitiliza.

Mfano posho ya mwezi wa Julai 2023, tulikuja tukaingiziwa tarehe 18 Agosti 2023 tena baada ya sisi wenyewe interns kuamua kukutana kujadiliana juu ya stahiki zetu, ndipo uongozi ulipata taarifa kuwa tunafanya kikao, wakaingiwa na hofu kwamba tunaweza kugoma, ndio wakaamua kulishughulikia na pesa tukaingiziwa jioni yake.

Hadi tarehe 17 Septemba 2023 posho yetu ya Agosti hatujapatiwa, tumefatilia kwa wahusika hakuna mwenye majibu yenye kueleweka kila mhusika anajibu “Mimi part yangu nimeshafanya”, hayo ni majibu tuliyoyazoea kila mwezi tukifatilia na huu ndio umekuwa utamaduni Hospitalini hapa kuchelewesha malipo ya Posho za Interns.

Hali hii imekuwa ikiiathiri sana maisha yetu kiasi ya kwamba hufikia miezi mingine watu hutolewa ndani ya vyumba vya watu kutokana na kushindwa kulipa kodi kwa wakati.

Kwa kweli tumekuwa wanyonge sana kwani wengi wetu, tumekuwa na hofu ya kufanyiwa figisu ya kuharibiwa Intership zetu endapo tukichukua hatu zitakao waudhi viongozi.

Tunadhalilika kwa kweli huku mtaani.
 
Hadi Leo hamjapewa? Na ni internship ya serikali au? Yani mmepelekwa na serikali au mmeomba kupitia hospitali
 
Naibu waziri wa huko hajaona jambo hilo au ndo Yale tulimuomba barabara ya Sanya juu - - Kia airport akatuwekea km 2?

Bro bro tutendee Haki bana kama ulivyowatendea haki wana Lindi Kwa hospital yao ya sokoine kuwapatia scan machine nasi tujengewe Ile brbr tutakukumbuka
 
Tulia dogooooo,usitake tumwage mchele humu,au wee ni usalama unatuzoom??

Hela yenu imepelekwa TANESCO kupunguza makali ya mgao wa umeme,hebu kuwa mzalendo kuipigania nchi yako,acha malalamiko.

Mtu mwenyewe upo intern kelele nyiiingi,ukiajiriwa mazima je si utatuletea shida sisi viongozi wa juu wa Wizara ya Afya????
 
Pambaneni vijana kudai haki zenu. Maana hakuna namna nyingine. Siku hizi tumerudia yale mambo ya enzi zileee! Enzi za nchi ya kitu kidogo. Yaani mkizubaa tu, wahuni wanawapiga mchana kweupe.
 
Dogo huko kucheleweshewa posho ndo kunafanya ufukuzwe kwenye nyumba uliyopanga??.kodi unalipa milioni mbili kwa mwezi au??..maana nusu ya posho tu ya mwezi mmoja unalipa kodi almost miezi sita kama unakaa sehemu ya 100k..

Hela ya Intern sio ya kuililia hivi..acha ichelewe itakusaidia baadae..january utakuwa juu ya mawe mbaya..unless unauhakika wa ajira baada ya kumaliza intern.

Been there done that.
 
Poleni sana vijana.
Lakini nina swali nje ya mada kama ifuatavyo.....
Hivi kwanini hiyo kada wengi wenu (sio wote) hua mnajiona ni wamuhimu zaidi kuliko kada zingine..??
 
Unaongelea mshahara au call /overtime? Nachojua mshahara unatoka hadhina kwenda account ya hospital, kama watumishi sidhan kama kuna ucheleweshaji
 
Unaongelea mshahara au call /overtime? Nachojua mshahara unatoka hadhina kwenda account ya hospital, kama watumishi sidhan kama kuna ucheleweshaji
Huyu ni intern lakini kilaza.

Ameshindwa kutofautisha posho za hospitali au mshahara wake kama yeye intern.

Akiongelea posho za hospitali nadhani ,hospitali zote uwa wanachelewesha hizo hela.

Lakini hela ya intern kama mshahara haichelewi.
 
Unaongelea mshahara au call /overtime? Nachojua mshahara unatoka hadhina kwenda account ya hospital, kama watumishi sidhan kama kuna ucheleweshaji
Mshahara wa intern unajulikana kama posho ya kujikimu ya kila mwezi ambayo inalipwa na serikali.... Mdau yuko sahihi maana ndo inajulikana hvyo... Kinachodaiwa ni hiyo posho ya mwezi wa nane mpka tarehe hii 19 mwezi wa 9 haijalipwa bado ilihali malipo yameshaingia akaunti ya hospital wiki ya pili sasa... Sasa sijui ni uzembe wa hospitali ya mawenzi ama kuna namna inafanyika
 
Yaani sielewi hospital ya mawenzi ina shida gani, kama rrh zingine intern wanalipwa kwa wakati, inakuwaje kwa mawenzi kunakuwa na ucheleweshwaji wa malipo kwa intern usio kuwa na maelezo yakinifu???? Hili jambo lina makusudi ndani yake.
 
Back
Top Bottom