A
Anonymous
Guest
Mimi ni mmoja wa Madaktari Wanafunzi ambao tulikuwa tunajifunza kwa vitendo kwa muda wa mwaka mmoja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Kitete) iliyopo Tabora.
Moja ya changamoto ambayo tulikutana nayo kwenye mafunzo yetu ni ucheleweshwaji wa malipo yetu (posho) ya kila mwezi.
Mara kadhaa yalikuwa yakichelewa lakini inadaiwa kuwa wahusika walilazimika kulipa hata kwa kuchelewa wiki moja mbili hadi tatu kwa kuwa walihofia yakichelewa zaidi tunaweza kugoma.
Pamoja na hivyo, mwezi mmoja wa mwisho wa mafunzo yetu Oktoba 2023 hatukulipwa posho zetu, tulilzimika kusubiri kama ilivyo kawaida wiki moja, mbili au tatu lakini bado kukawa na ukimya.
Baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu huku tukifuatilia, tukajulishwa kuwa fedha zimeshafika lakini zimepelekwa Hazina Ndogo, na huko ndipo zilipokwama.
Pamoja na hivyo tulipofuatilia hiospitli nyingine wenzetu wote wametuambiwa wao wameshalipwa na hakuna wanachodai, kwa sasa wanaendelea na maisha yao mengine.
Kwa nini Hospitali ya Kitete haijatulipa mpaka sasa na hakuna majibu tunayopewa ya kueleweka?
Kwa kawaida fedha zikitoka Hazina, zinaelekezwa kwenye kituo husika (hospitali) baada ya hapo nipo wahusika wanapewa, na uongozi wa Hospitali unakiri kuwa umepokea fedha lakini zipo Hazina Ndogo, huko zinafanya nini na tayari zimeshapita wiki tano hatujalipwa posho zetu?