USHUHUDA WA KWELI:
Mimi ukweli nakubaliana na madaktari kwa asilimia mia moja hasa wanapodai kudumishwa kwa huduma mahospitali, uwepo wa vifaa vya tiba na madawa.
Wiki mbili/tatu zilizopita tulikuwa kikundi ambapo tulitembelea hospitali moja ya mkoa. Na tulienda moja kwa moja katika wodi ya wazazi na watoto. Hali tuliyoikuta huko kwa kweli inasikitisha. Achia wazazi waliolazwa humo ambapo majority ni wa kima cha chini, ambao hata kuwa na uwezo wa kununua vitu muhimu unaona wazi kabisa kwao ni tatizo. Basi tukakaa na wauguzi ili watueleze changamoto na namna gani wanaweza kusaidiwa. Baadae pia tulipata wasaa wa kuongea na mfamasia wa hospitali na haya ndiyo tuliyoelezwa:
Kwanza Huwa wana upungufu mkubwa wa vifaa muhimu katika wodi ya wazazi. Cha kwanza ni mipira (mackintosh). Kwa wasioijua hii ni ile mipira ya mikojo ambayo huwa inatumiwa katika wodi ya wazazi. Wengi mjuavyo wamama wanaosubiria kujifungua ama waliojifungua huwa wanakuwa na disharge za maji2/damu. Sasa siku hiyo tuliambiwa stock waliyokuwa nayo ilikuwa imeisha imemamliziwa jana yake, na ilikuwa imebaki 15. Wakati on daily basis wanapokea wagonjwa 25/30. Sasa fikiria ukosefu wa hii mipira impact yake nini? Kwanza inabidi ku-reuse hiyo mipira mara nyingi au wengine kutowekewa kabisa katika magodoro. Matokeo yake ni mfumuko wa maambukizi, kutoka na kulalia magodoro yaliyovujiwa maji2/damu. Haya labda wengine watasema wazazi waingie wodini na mipira yako. Jibu ni kwamba sio kila mtu ana uwezo huo, kwa kifupi wengi wa wazazi tuliowakuta sikuhiyo, unaona kabisa huyu hata ukimwambia kanunue nguo ya ndani ni mtihani mkubwa.
Pili - walikuwa pia hawana syringes, nazo wanasema huwa zina msimu zikikosekana zimekosekana.Tatu- pia huwa wanaishiwa gloves, siongei sana imagine kuishiwa gloves wodi ya wazazi. Hatari anayokuwa nayo muuguzi. Maaambukizi nje nje.Nne Huwa wanaishiwa dawa ambazo huwapa wazazi kuzuia utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.Tano tulionyeshwa chumba cha njiti. Hiki ni chumba ambacho hulazwa wamama waliojifungua watoto kabla ya siku. Kwa kifupi hakikuwa na mtizamo wa chumba cha njiti badala tuliona kama ni stoo ya vitu chakavu hakina hata kifaa unachoona hiki ndo kinatumika kuokoa maisha ya njiti. Inamaanisha katika mkoa huu ukijifungua njiti, majaliwa ya njiti kupona yanabaki kwa Mwenyezi Mungu.Pia tukapata wasaa wa kuongea na mfamasia na akadai vitu ambavyo unakuta vinakuwa out of stock, unakuwa hata MSD (bohari ya madawa hakuna). Sasa mie sidhani masuala kama hayo hapo juu yanahitaji mjadala, kwenye maslahi sawa. Fikiria hiyo ni hospitali ya mkoa, matatizo ndo hayo.Mimi nilitegemea serikali ingeweka mkakati toka mgomo utangazwe pale mwanzo namba ambavyo itakabiliana na hizi changamoto na kutangaza wazi katika vyombo vya habari ili wananchi wote wajue jitihada zinazoendelea. Tunavyoambiwa serikali inashughulikia wakati husikiii mshindo nyuma kwa kweli unashindwa kuelewa somo.Cha muhimu hata mkikisisitiza madaktari waendelee na huduma wakati vifaa muhimu hamna, huyo mgonjwa anamtibu vipi? Okay kuna wale wakaotibiwa na vile vifaa/dawa vi chache vilivyopo, wengine je? Kwa hiyo kutokana na huduma hafifu watu wanaendelea kufa wakati vifo vyao vingezuilika kama mikakati maalum ya utekelezaji ingewekwa na kufanyiwa kazi. Sioni kama kuna mtu anaona tu raha amuone daktari anapita wodini wakati uwezo wake wa kutibu umepunguzwa kwa asilimia zaidi 50%. Definetely we have to change. Mwisho kuhusu maslahi ya madaktari, mimi naona katika makundi ambayo yanabidi yapate maslahi mazuri hapa nchini ni madaktari, walimu ana may be polisi (wakipunguza rushwa). Ilitakiwa uuguzi uwe ni hot cake katika maslahi lakini pia iwe ni kazi kuupata, kuhakikisha wale wanaoupata wawe ni matabibu wa kweli waliosoma na kufaulu vizuri kabisa kwa vitendo na nadharia. Tusikumbatie mifumo ambayo tunaona haifanyi kazi. Tupitie mifumo yetu na ile ambayo ni hafifu ibadilishwe na ku adopt mifumo yenye tija!!
Ofcourse mgomo ni mbaya hasa ukikukuta wewe kama victim kipindi unahitaji huduma, lakini migomo husaidia katika kuhakikisha matatizo yanafanyiwa kazi na ni sustainable. So watakaofaidika, ni wale wa hapo mbeleni na kwa kiasi kikubwa vifo vitapungua sana kama kutakuwa na uhakiki wa uwepo wa vifaa, mazingira mazuri na maslahi bora kwa matabibu. EBu turudi nyuma ule mgomo wa kwanza, kama madaktari wasingegoma na kushikilia msimamo wao au wangeamua kurudi mzigoni baada ya kitisho cha kwanza cha kuamriwa warudi kazini tusingejua madudu yaliyokuwa yanaendelea wizara ya afya ambayo yalipelekea uwajibishwaji.
......