Madaktari bingwa Muhimbili waanza mgomo

USHUHUDA WA KWELI:
Mimi ukweli nakubaliana na madaktari kwa asilimia mia moja hasa wanapodai kudumishwa kwa huduma mahospitali, uwepo wa vifaa vya tiba na madawa.
Wiki mbili/tatu zilizopita tulikuwa kikundi ambapo tulitembelea hospitali moja ya mkoa. Na tulienda moja kwa moja katika wodi ya wazazi na watoto. Hali tuliyoikuta huko kwa kweli inasikitisha. Achia wazazi waliolazwa humo ambapo majority ni wa kima cha chini, ambao hata kuwa na uwezo wa kununua vitu muhimu unaona wazi kabisa kwao ni tatizo. Basi tukakaa na wauguzi ili watueleze changamoto na namna gani wanaweza kusaidiwa. Baadae pia tulipata wasaa wa kuongea na mfamasia wa hospitali na haya ndiyo tuliyoelezwa:
Kwanza – Huwa wana upungufu mkubwa wa vifaa muhimu katika wodi ya wazazi. Cha kwanza ni mipira (mackintosh). Kwa wasioijua hii ni ile mipira ya mikojo ambayo huwa inatumiwa katika wodi ya wazazi. Wengi mjuavyo wamama wanaosubiria kujifungua ama waliojifungua huwa wanakuwa na disharge za maji2/damu. Sasa siku hiyo tuliambiwa stock waliyokuwa nayo ilikuwa imeisha imemamliziwa jana yake, na ilikuwa imebaki 15. Wakati on daily basis wanapokea wagonjwa 25/30. Sasa fikiria ukosefu wa hii mipira impact yake nini? Kwanza inabidi ku-reuse hiyo mipira mara nyingi au wengine kutowekewa kabisa katika magodoro. Matokeo yake ni mfumuko wa maambukizi, kutoka na kulalia magodoro yaliyovujiwa maji2/damu. Haya labda wengine watasema wazazi waingie wodini na mipira yako. Jibu ni kwamba sio kila mtu ana uwezo huo, kwa kifupi wengi wa wazazi tuliowakuta sikuhiyo, unaona kabisa huyu hata ukimwambia kanunue nguo ya ndani ni mtihani mkubwa.

Pili - walikuwa pia hawana syringes, nazo wanasema huwa zina msimu zikikosekana zimekosekana.Tatu- pia huwa wanaishiwa gloves, siongei sana imagine kuishiwa gloves wodi ya wazazi. Hatari anayokuwa nayo muuguzi. Maaambukizi nje nje.Nne – Huwa wanaishiwa dawa ambazo huwapa wazazi kuzuia utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.Tano – tulionyeshwa chumba cha njiti. Hiki ni chumba ambacho hulazwa wamama waliojifungua watoto kabla ya siku. Kwa kifupi hakikuwa na mtizamo wa chumba cha njiti badala tuliona kama ni stoo ya vitu chakavu hakina hata kifaa unachoona hiki ndo kinatumika kuokoa maisha ya njiti. Inamaanisha katika mkoa huu ukijifungua njiti, majaliwa ya njiti kupona yanabaki kwa Mwenyezi Mungu.Pia tukapata wasaa wa kuongea na mfamasia na akadai vitu ambavyo unakuta vinakuwa out of stock, unakuwa hata MSD (bohari ya madawa hakuna). Sasa mie sidhani masuala kama hayo hapo juu yanahitaji mjadala, kwenye maslahi sawa. Fikiria hiyo ni hospitali ya mkoa, matatizo ndo hayo.Mimi nilitegemea serikali ingeweka mkakati toka mgomo utangazwe pale mwanzo namba ambavyo itakabiliana na hizi changamoto na kutangaza wazi katika vyombo vya habari ili wananchi wote wajue jitihada zinazoendelea. Tunavyoambiwa serikali inashughulikia wakati husikiii mshindo nyuma kwa kweli unashindwa kuelewa somo.Cha muhimu hata mkikisisitiza madaktari waendelee na huduma wakati vifaa muhimu hamna, huyo mgonjwa anamtibu vipi? Okay kuna wale wakaotibiwa na vile vifaa/dawa vi chache vilivyopo, wengine je? Kwa hiyo kutokana na huduma hafifu watu wanaendelea kufa wakati vifo vyao vingezuilika kama mikakati maalum ya utekelezaji ingewekwa na kufanyiwa kazi. Sioni kama kuna mtu anaona tu raha amuone daktari anapita wodini wakati uwezo wake wa kutibu umepunguzwa kwa asilimia zaidi 50%. Definetely we have to change. Mwisho kuhusu maslahi ya madaktari, mimi naona katika makundi ambayo yanabidi yapate maslahi mazuri hapa nchini ni madaktari, walimu ana may be polisi (wakipunguza rushwa). Ilitakiwa uuguzi uwe ni hot cake katika maslahi lakini pia iwe ni kazi kuupata, kuhakikisha wale wanaoupata wawe ni matabibu wa kweli waliosoma na kufaulu vizuri kabisa kwa vitendo na nadharia. Tusikumbatie mifumo ambayo tunaona haifanyi kazi. Tupitie mifumo yetu na ile ambayo ni hafifu ibadilishwe na ku adopt mifumo yenye tija!!

Ofcourse mgomo ni mbaya hasa ukikukuta wewe kama victim kipindi unahitaji huduma, lakini migomo husaidia katika kuhakikisha matatizo yanafanyiwa kazi na ni sustainable. So watakaofaidika, ni wale wa hapo mbeleni na kwa kiasi kikubwa vifo vitapungua sana kama kutakuwa na uhakiki wa uwepo wa vifaa, mazingira mazuri na maslahi bora kwa matabibu. EBu turudi nyuma ule mgomo wa kwanza, kama madaktari wasingegoma na kushikilia msimamo wao au wangeamua kurudi mzigoni baada ya kitisho cha kwanza cha kuamriwa warudi kazini tusingejua madudu yaliyokuwa yanaendelea wizara ya afya ambayo yalipelekea uwajibishwaji.
......
 
Bravooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!! Safi sana mabingwa wote naomba isiwe muhi2 pekeyake mgomo uwe wa nchi nzima eeh "liwalo na liwe" kama mbwai mbawimbwai tu ....

itakuwa vp endapo ukaugua ghafla utafuta kauli yako? Kitu cha msingi si kuushabikia huu mgomo kwasababu kuna ndugu zetu wanateseka, me nadhan jambo la msingi ungeishaul serikali nin kifanyike ili kuepuka hli janga na si kushabikia tu. TAFAKARI.
 
Under which and whose law are they using to hold our sick hostage?


Una mkataba na Daktari yoyote kuwa amtibu mgonjwa Wako? Na akimdunga sindano za magonjwa mengine kwa hasira je Utajuaje/Utafanyaje? Vunja Mkataba kama vip umfukuze kazi mlete wa kutoka china and bla bla bla! U got to be litle bit more serious guys kuna kazi zingine huwezi lazimisha mtu kufanya sio kama kupalilia maharage unaeza enda kagua kama kweli majani hamna shambani!
 
swali la msingi sana nalojiuliza mimi, kama watu wanailaani serikali kwa kutaka kumuua mtu anayeongoza mapambano ya kutaka serikali iwaongezee pesa (kama wanavyodai kwamba serikali inahusika), Kwanini pia hawamlaumu huyu mtu kwa kushirikiana na wenzake kuwaua watanzania wenzao (kwa migomo) kutokana na sababu hiyo hiyo ya fedha

Mahospitali wagonjwa wengi hufa hata wakiwa wanatibiwa kwa ajili ya kukosa vifaa tiba na madawa. Mbona mna macho lakini hamuoni?
 
It's what happens when you have Serikali dhaifu isiyojali na kusikiliza.Wataamka baadaye wakati maisha ya wagonjwa yalishaishia kuzimu.:embarassed2:
 
Kuna hii myth eti madaktari wanapigania kuboreshwa huduma za afya!

Hawana cha huduma za afya wala nini kwao muhimu ni pesa tu hata ikibidi watu wafe wao wapate pesa!
Mkuu, naomba utuelimishe sisi wengine wenye uelewa mdogo jinsi hii ilivyo kuwa ni 'myth' na na jinsi madai mengine kama huduma mbovu na ukosefu wa vifaa kuwa ni 'myth'.
 
BornTown....chonde chonde kidole na macho.....huyo wa liwalo na liwe athari za mgomo hazimgusi kwa namna yeyote ile...yawezekana hata mimi na wewe hatutibiwi kwenye hizo hospitali za waliogoma au tunakutana nao Regency, Aga Khan, Hindumandal nk....Je watanzania wenzetu wote including ndg zako waliotawanyika maeneo mbali mbali wana uwezo wa kutibiwa huko?? Kwa sasa tu wazima hatujui kesho tutajikuta katika mazingira gani (kama ambavyo Ulimboka hakujua pia)...Mgomo wa madaktari kamwe sio jambo la kushabikia na wanaoadhibiwa katika mgomo huu sio wahusika kwani adhadbu hii haiwagusi wahusika (serekali ) moja kwa moja....
i beg to submit....

na wasiwasi na kurugenzi ya mawasiliano ya afya ya kichwa chako!
 
itakuwa vp endapo ukaugua ghafla utafuta kauli yako? Kitu cha msingi si kuushabikia huu mgomo kwasababu kuna ndugu zetu wanateseka, me nadhan jambo la msingi ungeishaul serikali nin kifanyike ili kuepuka hli janga na si kushabikia tu. TAFAKARI.

Nakimaaniha walichokifanya ni sahihi kwani nimesha lazwa muhimbli tena chini nimetandikiwa godoro tuko wagonjwa 2 godoro moja,sasa jiulizemtu anaitaji drip daktari anakuudumiaje?
Mama anakwenda kujifungua analazwa chini daktari anamuhudumiaje jiulize tu hata ni wewe utamsaidiaje huyu mama?
Mazingira ya kufanyia kazi nimibovu hayafai halafu serikali wanasema ni posho madaktari wanadai kumbe sio hawataki kusema ukweli.

Nilimesha shuhudia kwa macho yangu mtoto anafariki Amana hospital mikononi mwa daktari kwa kukosa kale kasindano kwa kuweka kwenye mshipa ili atundikiwe drip, hospital nzima ilikosa size ya hicho kisindano daktari akatoa hela yake mfukoni akawapa ndugu wa mgonjwa wakatafute hicho kipini walikosa nje sasa kosa ni lanani hapo daktari ama serikali??

Ukiwa na mgonjwa ama ukaugua wewe mwenyewe ukalazwa kati ta muhimbili, amana, mwananyamala au temeke ndipo utakapo jua madaktari wanamaanisha nini kwenye huu mgomo.

Chamsingi serikali iwe wazi iseme ukweli isiwapotoshe wananchi??
 
Je waliokosa dawa iweje hukumu yao tumia akili sio
mkumbo.Hakuna dawa wala vipimo.
 
Ulimboka hakutaka kuuawa angetakaiwa afe asingekuwepo leo kuonesha majeraha. Huyo katumiwa na watu wenye kuta hii nchi isitawalike, na wewe unawajuwa ni kina nani.


Ina maana na wewe unawajua, basi wataje na kama huwataji basi na wewe ni mhusika namba moja waliomtesa Ulimboka, shame on you.
 
Hao madaktari wahukumiwe kifo kwa kila mgonjwa atae kufa kuanzia amri ya mahakama ya kuwata warudi kazini ilipotolewa.


Zomba swala la madaktari kugoma sio kama makuri au waendesha daladala au watu wa mabenki. Hii ni sekta muhimu sana na sasa wao tayari washagoma. Tujikite basi katika suluhisho endelevu lakini sio suluhisho litakaloleta matatizo zaidi. Unaongelea kunyonga kama kitu rahisi kufanya. Kwa sheria zetu ili mtu ahukumiwe kunyongwa ni mpaka rais aridhie hukumu ya mahakama. Rais na serikali yake unayoitetea unataka kuiongezea matatizo makubwa zaidi kwanza kwa kuua na pili kutafuta madaktari toka nje. Sijui kama gharama ya vyote viwili ni sawa na kuwatimizia wanachodai hata kama si mara moja lakini kukawepo na payment schedule itakayoridhiwa na pande zote mbili. Tunaweza tukawabeza madaktari kwa msimamo wao lakini umuhimu wao unaonekana jinsi ambavyo hata rais alikutana nao. Ni wangapi wenye bahati hiyo? Ni wachahche na ishara ya umuhimu wao. Cha msingi hapa tulipofika ni tete ni better kutoa mawazo, maoni endelevu yanaweza kuleta suluhu la kudumu katika emergence situation kama tuliokuwa nayo. Na tunachokiandika JF kisiwe tu ari mradi tuandike tukujua watu wanasoma na kufanya filtering ya maoni na yale constructive yanachukuliwa sio lazima tutangaziwe.

Sasa nisije nikawa retrogressive in my analysis. Napendekeza.

1.Sherehe kubwa za kitaifa ziadhimishwe sio kwa mtindo wa sasa wa gwaride, mialiko ya wageni na mengine yenye gharama bali watu katika wilaya, kata na vitongoji wafanye shughuli za maendeleo kama kusafisha mitaa na kupanda miti

2. Misafara ya viongozi ipunguzwe mpaka nusu labda ya wanausalama ili viongozi wetu wasijedhuriwa. Mfano magari yakiwa yanamsubiri mkubwa madereva huyaacha silence na AC zikiwa on for several hours. Nafikiri hapa ndio tunatakiwa kubana matumizi.

3. Magari yatakayopunguzwa through cutting of misafara yauzwe na pesa ielekezwe huduma za jamii kama afya.

4. Safari za nje za viongozi zipunguzwe na kama ilivyo no.2 hata delegation inayaokwenda na viongozi ipunguzwe. Dunia imeendelea maana tunazo teleconference facilities viongozi badala ya kusafiri wazitumie kuwasiliana.
5.Wigo wa kodi (tax base) uongezwe hasa kwenye wachimbaji wa madini, mafuta, gesi na simu a=za mikononi. Wenzetu waliotuzunguka maeneo niliyotaja yamekuwa ndio chanzo cha mapato ya serikali kwetu ni kinyume chake.

Nawakilisha
 
na wasiwasi na kurugenzi ya mawasiliano ya afya ya kichwa chako!

Ni haki yako haswa uwezo wa kufikiri unapolingana na mkia wa mbuzi...sitakulaumu kwa hilo provided kuwa tupo dunia mbili tofauti interms of IQ.....
 
Mgomo si jambo jema kabisa, na pia kumpiga Bw. Ulimboka ni jambo baya kabisa katika kulishughulikia suala kama hili. Kwahiyo kinachotakiwa ni kulishughulikia jambo hili ili lisiendelee kuleta madhara kwa watanzania. Tatizo hapa haifahamiki vizuri commitment ya serikali ilikuwa itekeleze haya madai ya madaktari katika time frame ipi! na hili ndo naona ni kikwazo hapa, uwazi unahitajika ili kujenga uaminifu katika jambo hili. Serikali ituweke wazi katika hili, sisi kama raia wa tanzania hatuna wa umlilia zaidi ya serikali ambayo inawajibika kwa wananchi kwa namna yote ile. hivyo ni ushauri tu, jambo hili liwekwe wazi ili wananchi wafahamu na pia madaktari wapate kuelewa kipi kipi serikali itawatekelezea na kipi kwa sasa hakiwezekani na mbadala wake ni nini! Mi nauhakika kabisa madaktari ni wasomi na waelewa, na watakuwa tayari kungoja ili wananchi wasio na hatia wasiendelee kuadhibiwa.
 
Back
Top Bottom