Ummy Mwalimu: Lengo la kufanya Private Clinic kwenye Hospitali za Umma ni kutoa motisha kwa Madaktari Bingwa

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
UMMY ed.jpg

Hili suala la Madaktari bingwa kufanya private Klinic katika Hospitali za umma (IPPM) baada ya saa za kazi sio jipya. Tayari linafanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, JKCI, Ocean Road nk. Lilianza kutekelezwa zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Lengo ni kutoa motisha wa kuongeza kipato cha Madaktari bingwa na bobezi walioajiriwa na Serikali. Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali Mikoani, sasa tunataka kushusha utaratibu huu kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa ili kubakiza madakatari bingwa kuendelea kufanya kazi mikoani.

Hili jambo lina tija katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa mikoani. Daktari bingwa anapata na Hospitali inapata. Muhimu kuweka utaratibu mzuri na wa wazi.

NB: Tuna uhaba wa Madaktari bingwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa. Mwezi uliopita tulitangaza nafasi 35 walioomba ni 15 tu. Kama Wizara tutaendelea kuweka mikakati mbalimbali ili kuvutia Madaktari bingwa kufanya kazi ktk Hospitali za umma hasa za mikoani.

Utaratibu wa utoaji huduma za afya baada ya masaa ya kazi (Intramural Private Practice) sio mpya - Kwa Hospital kubwa kama Muhimbili una zaidi ya miaka 20, JKCI na MOI una zaidi ya miaka 15 nk Utaratibu huu wa kutoa huduma hizi "binafsi na za haraka" (private and fast track) baada ya saa za kazi ndani ya Vituo vya Umma unasimamiwa na miongozo mahsusi iliyopitishwa na Bodi za Hospital husika.

Kwa mfano katika Hospital ya Taifa- Muhimbili huitwa Intramural Private Practice at Muhimbili maarufu IPPMBaadhi ya faida za Utaratibu huu ni pamoja na:

1. Kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kuhudumiwa kwa uharaka (kwa kulipia ziada)

2. Kuwatuliza Madaktari kwenye vituo vyao vya kazi na kuwapunguzia adha ya kukimbia kwenye vituo binafsi(maarufu vijiwe au vioski) baada ya muda wa kazi- hii inashusha heshima ya kitaaluma kwao na wengine kulazimika kufanya kazi katika mazingira hatarishi na yenye uwekezaji mdogo wa miundo mbinu na vifaa Tiba kuliko alivyoviacha katika Hospital yake ya Rufaa ya Umma.

3. Kuongeza mapato ya Hospitali za Rufaa za Umma kwani wateja hulipia huduma kwa gharama kubwa zaidi ya bei za kawaida za Serikali. Mapato hayo huongeza uwekezaji unaowafaidisha wagonjwa Wote, unaochangia kuwezesha hospitali kuhudumia wagonjwa wa Msamaha na unaoongeza motisha kwa watumishi wote kwani mapato hayo hugawanywa wa watumishi wote wa hospital husika.

Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya

===

My Take: Kama ni jambo la kitambo, kulitolea kauli kulikuwa kunalenga nini? Acheni ubabaishaji

Pia soma: Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi
 
Kubali umekosea kusema hilo acha kutetea ujinga huo tena jisaishe mapema, kwa kila wataalamu wakihitaji motisha wafanye hivo, mualimu mkuu afungua chekechea yake hapo shuleni, manager wa benki afungua micro finance yake hapo beki. Wengi mnapewa uwaziri ila amjakoma kiakili "social intelligence yenu iko low"
 
MADAKTARI BINGWA KUTUMIA HOSPITALI ZA SERIKALI KUENDESHA PRIVATE CLINIC SIO JIPYA. LINA TIJA ; LITABORESHA HUDUMA KWA WANANCHI - UMMY MWALIMU

Anaandika Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu akiwa Ziarani Mkoani Mkoani Shinyanga.

Utaratibu wa utoaji
huduma za afya baada ya masaa ya kazi (Intramural Private Practice) sio mpya - Kwa Hospital kubwa kama Muhimbili una zaidi ya miaka 20, JKCI na MOI una zaidi ya miaka 15 nk

Utaratibu huu wa kutoa huduma hizi "binafsi na za haraka" (private and fast track) baada ya saa za kazi ndani ya Vituo vya Umma unasimamiwa na miongozo mahsusi iliyopitishwa na Bodi za Hospital husika....kwa mfano katika Hospital ya Taifa- Muhimbili huitwa Intramural Private Practice at Muhimbili maarufu IPPM

Baadhi ya faida za Utaratibu huu ni pamoja na:

2. Kuwatuliza Madaktari kwenye vituo vyao vya kazi na kuwapunguzia adha ya kukimbia kwenye vituo binafsi(maarufu vijiwe au vioski) baada ya muda wa kazi- hii inashusha heshima ya kitaaluma kwao na wengine kulazimika kufanya kazi katika mazingira hatarishi na yenye uwekezaji mdogo wa miundo mbinu na vifaa Tiba kuliko alivyoviacha katika Hospital yake ya Rufaa ya umma.

3. Kuongeza mapato ya Hospitali za Rufaa za umma kwani wateja hulipia huduma kwa gharama kubwa zaidi ya bei za kawaida za Serikali......Mapato hayo huongeza uwekezaji unaowafaidisha wagonjwa Wote, unaochangia kuwezesha hospitali kuhudumia wagonjwa wa Msamaha na unaoongeza motisha kwa watumishi wote kwani mapato hayo hugawanywa wa watumishi wote wa hospital husika.
IMG-20230712-WA0033.jpg
 
3. Kuongeza mapato ya Hospitali za Rufaa za umma kwani wateja hulipia huduma kwa gharama kubwa zaidi ya bei za kawaida za Serikali......Mapato hayo huongeza uwekezaji unaowafaidisha wagonjwa Wote, unaochangia kuwezesha hospitali kuhudumia wagonjwa wa Msamaha na unaoongeza motisha kwa watumishi wote kwani mapato hayo hugawanywa wa watumishi wote wa hospital husika.View attachment 2685579
Wacheni uhuni nyie
 
Ummy amechemka kwa huu uamuzi wake.
Nyinyi wabongo kila kitu ni kupinga tu ndio maana nchi imesimama haiendelei, angalia Rwanda inavyopiga maendeleo, angalia Kenya, Uganda zote hizo zimetuacha sisi tuko kwenye ubishi tu kila mtu kujifanya mtaalamu tuwaachie viongozi tuliowachaguwa wafanye kazi.
 
Utaratibu wa utoaji huduma za afya baada ya masaa ya kazi (Intramural Private Practice) sio mpya - Kwa Hospital kubwa kama Muhimbili una zaidi ya miaka 20, JKCI na MOI una zaidi ya miaka 15 nk

Utaratibu huu wa kutoa huduma hizi "binafsi na za haraka" (private and fast track) baada ya saa za kazi ndani ya Vituo vya Umma unasimamiwa na miongozo mahsusi iliyopitishwa na Bodi za Hospital husika....kwa mfano katika Hospital ya Taifa - Muhimbili huitwa Intramural Private Practice at Muhimbili maarufu IPPM

Baadhi ya faida za Utaratibu huu ni pamoja na:
1. Kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kuhudumiwa kwa uharaka (kwa kulipia ziada)

2. Kuwatuliza Madaktari kwenye vituo vyao vya kazi na kuwapunguzia adha ya kukimbia kwenye vituo binafsi(maarufu vijiwe au vioski) baada ya muda wa kazi- hii inashusha heshima ya kitaaluma kwao na wengine kulazimika kufanya kazi katika mazingira hatarishi na yenye uwekezaji mdogo wa miundo mbinu na vifaa Tiba kuliko alivyoviacha katika Hospital yake ya Rufaa ya Mkoa.

3. Kuongeza mapato ya Hospitali za Rufaa za umma kwani wateja hulipia huduma kwa gharama kubwa zaidi ya bei za kawaida za Serikali......Mapato hayo huongeza uwekezaji unaowafaidisha wagonjwa Wote, unaochangia kuwezesha hospitali kuhudumia wagonjwa wa Msamaha na unaoongeza motisha kwa watumishi wote kwani mapato hayo hugawanywa wa watumishi wote wa hospital husika.
 
Nyinyi wabongo kila kitu ni kupinga tu ndio maana nchi imesimama haiendelei, angalia Rwanda inavyopiga maendeleo, angalia Kenya, Uganda zote hizo zimetuacha sisi tuko kwenye ubishi tu kila mtu kujifanya mtaalamu tuwaachie viongozi tuliowachaguwa wafanye kazi.

shida hata mifumo yenyewe yakuwachagua haijakaa sawa, ndio kila wanapotoa maamuzi raia hawaamini lazima wahoji.
 
Nyinyi wabongo kila kitu ni kupinga tu ndio maana nchi imesimama haiendelei, angalia Rwanda inavyopiga maendeleo, angalia Kenya, Uganda zote hizo zimetuacha sisi tuko kwenye ubishi tu kila mtu kujifanya mtaalamu tuwaachie viongozi tuliowachaguwa wafanye kazi.
Hakuna Nchi inapiga Maendelea kuizidi Tanzania kati ya hizo ulizozitaja..

Hapo Waziri kachemka.
 
Kubali umekosea kusema hilo acha kutetea ujinga huo tena jisaishe mapema, kwa kila wataalamu wakihitaji motisha wafanye hivo, mualimu mkuu afungua chekechea yake hapo shuleni, manager wa benki afungua micro finance yake hapo beki. Wengi mnapewa uwaziri ila amjakoma kiakili "social intelligence yenu iko low"
Kuna mijitu wao kila kitu kupinga tu hata ukimwambia unampenda sana mke wako litakataa tu kikubwa limepinga. Sasa nini kibaya hapa waziri kasema. Haya mambo yapo tunayaona kila siku mahospitalini shida waziri kasema tu.
 
Back
Top Bottom