Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Naomba mwenye uzoefu ama kujua haya magari aniambie kwa kirefu...in terms of spare availability hapa tz.. uimara..fuel economy...na kila kitu kwa ujumla
1. NISSAN JUKE
2. NISSAN QASHQAI

Sent using Jamii Forums mobile app
Juke ni ngumu, na sporty. Kwenye spea nafikiri utasumbuka kidogo, as ni gari ya karibuni 2010/2011. Spare used ni chache. Unless uwe mtunzaji saana, au uwe teyari kununua OEM parts ambazo zitakua expensive. Engine nyingi ni 1.5l 1.6l ambazo ni very economy, so suala la mafuta sio ishu.

Qashqai, pia engine wise ni kama Juke, though yenyewe ina a 2.0l variant. Suala la spea, ni same ishu. Ni magari machache Bongo, so hata wauzaji wa spea wanaogopa kuzileta as wanaweza kukosa wateja. Ila kama unapenza hizo gari, siku hizi kila spea inapatikana, unaagiza tuu.
 
Asante sana mkuu kwa maelezo yako.
Ukisema OEM Parts una mana gani?
Na zipi ni changamoto kubwa kwa Nissan Juke kwa mazingira haya ya Tanzania?
Na vp inaweza kwenda masafa marefu bila kuchemsha??
Na kati ya Juke ya 2010, 2011 na 2012 ipi unaona ni nzuri kwamba ktk matoleo hayo nini hasa kimebadilika...

Haina shida kwa Tanzania. Sema suspension zake ni very firm. So kwa barabara zetu, haitakua comfortable. Pia ndani ni kidogo aise, hakina space kivile.

Kuhusu mwaka, mara nyingi haishauriwi kununua gari za kwanza kwenye generation flani, as huwa zinakua na issues nyingi. So 2010-12 inaweza isiwe nzuri saana. Ingawa vile unanunua used, matatizo mengi yalirekebishwa na first owners. Mfano hizo 2010-13 zilikua na issues na timing chain, ila nyingi zilirekebishwa. Pia sunroof zinaharibka mapema. So epuka models zenye sunroof.

OEM parts inamaanisha Original Equipment Manufacturer parts. Kila toleo la gari linapotoka, manufacturers (au licenced companies) huwa wanatengeneza genuine spare parts za hilo gari kwa miaka kadhaa. Kuanza oil filter mpaka bolts na nuts. Ukifunga hiyo spare, inaweza kuishi muda sawa na kama ile iliyofungwa pindi uliponunua gari jipya, sometimes hata zaidi, maana zinaboreshwa over time. Ila ni expensive. In short, kununua oem parts za Corolla hazipishani saana na za BMW kwa bei.
 
Salamu wakubwa
Gari yangu Toyota kluger inawaka taa hii na kuzima kila baada ya muda
Tatizo ni nini au inaashiria shida gani
Asante wakuu
IMG_0492.jpg

Ni alama kama hiyo namba 62
 
Habari zenu wakuu...gari yangu(Toyota probox) inatatizo la kupata joto sana kwenye tairi za mbele nimejaribu kuikagua kidogo nikagundua ni ile disk ya break inakuwa ya moto kisha inaambukiza kwenye rim...je tatizo ni nini wataalam
 
Kuna sababu nyingi ninazoweza kufikiria. Moja inaweza kuwa brake pads zako zimekwisha, so vyuma vinafanya direct contact na disks (rotors) za brake ambazo kawaida huwa zinapata joto saana wakati unapoendesha gari na kutumia brake, so joto linapita kwenye calipers na kufika mpaka kwenye rims. Ukiongeza na fact kwamba most Probox zinakua na rims za chuma, hivyo zinapata joto sana kuliko zile za aluminium alloy.

Pia inawezekana brake disks (rotors) zako zina mawimbi, kiasi kwamba zinagusa brake components muda mwingi gari linapotembea, hata kama hujatumia brake. So unapotumia brake, joto linakua kali zaidi.

Pia unawezakuta disks za mbele kwenye gari lako sio ventilated (hazina matundu matundu kati ya disk ya ndani na ya nje). Hii sidhani saana, as mara nyingi brake za mbele za gari nyingi za Toyota zinakua na ventilated disks, unless kama ziliwahi kubadilishwa kimakosa. So unaweza kuanza na kucheck pads, kama ziko sawa, piga jack, weka neutral, au free kama ni manual gearbox, zungusha tairi lako, kama halifanyi mzunguko mmoja na nusu freely, then jua disks zinagusana na brakepads hata bila kukanyaga brakes.
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako ndg.Nimekagua nikagundua ni brake pads zinagusana na disks muda wote hata wakati sijakanyaga brake.sasa sijajua kama ni pads zimeisha ama ni disks zimepinda.itabidi nipeleke kwa fundi akalikague vzr.
 
Spare yake ghali service inataka genuine lubricants na parts ila zinadumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naomba uniambie zaidi kuhusu hizi wanaita VolksWagen Passat, kwa kila kitu kwa ujumla??
Hasa spea availability, fuel economy na uwezo wa kwenda masaa marefu kama 1000km bila kuchemsha??
Engine ipi nzuri...1.4T TSI petrol ama 1.6TDi ama 2.0TDi diesel??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom