Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wakuu habari za humu ndani..
Naombeni kujua kama kuna madhara yeyote kama engine oil itazid yani kuvuka kili kidot cha juu cha kwenye stick

Madhara ya kwanza ni kusababisha kkukosa nguvu ktk injin
Kwasbb oil ikizidi plug ama nozel zinakua hazichomi pale ktk mlipuko wa ktk piston kama kawaida yake
Itapoteza moto kutokana na piston kulowana juu oil kwasbb imezidi kupita kiasi
 
Wakuu naomba ushauri,
nataka kununua BMW 3 series, maneno ya watu yanatisha gharama kumantain pia ni ndoa huwez kuuza.....

Kwa uzoefu wenu imekaaje hii?

Mkuu hakuna gari imara kama ya mjerumani
Na huo usemi wa kusema kua ndoa hayo ni yakizamani
Kuhus ughali wa spea ni kwasbb hakuna spea ya mjerumani inakuja feki
Kwa mfano ukinunua shokap zoba ya BMW kweli ni ghali lkn ukiifunga ni mkataba hapo ponda shimo ujuavyo lkn hadi ichoke haipungui miaka mi3
Tafaut na za carina au corola ni miez 6 tu zinaanza kugonga
 
Sidhani kama kuna gari linakuja na shida moja kwa moja, eti kisa tu labda ni toleo fulani au ni brand fulani.
Uimara na ubora wa gari ni matunzo yako mwenyewe tu. Kama upo rafu hata uwe na Land Rover 109 utakuja tu kusema zina shida fulani.
Cha msingi fuata masharti yaloainishwa na gari husika.
Sio gari unapeleka kwa mafundi uchwara na kila kona lina fundi.
Au Oil inatumika hadi inatoka kama maji ya jaruba za mpunga! Au waweka oil uchwara. Kwa mfano: kwanini watu wanasema Nissan xtrail ni mbovu? Oil (Magumashi)+ATF (Magumshi)+Mafundi feki= lazima useme gari bovu.
Kimsingi VW ni gari zuri kama nawe utakuwa na nidhamu nalo kwa kufuata miongozo yake na kukiuka miiko.
Asante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LEGE bei ya injini ya pajero gdi mswaki na nzima yaweza kuwa kiasi gani kwa huko Dar?

Mkuu kwa ushauri nunua injini ya suzuki. SJ14 na gear box yake ibandike humo ktk hio pajero utasahau mkuu na wala haihitaji madifkeshen makubwa kivile tofaut ya kuzisogeza engine mounting na geabox mounting pia na kukata propela
Engine za pajeri GDI zinasumbua saana yaani ktk mitubishi hapo ndo mjapan alichapia ktk hizo injin
 
wakuu naombeni msaada Gari yangu Subaru forestar Jana imeanza kutoa mvumo flani hiv kufuatilia nkagundua ni kwenye tairi nkapiga jeki nakawa nalichezesha tairi likawa linacheza cheza, tatizo litakuwa ni nini?

Mkuu kabla hujanunua wheelbearing cha kwanza peleka hio gari ukapime Wheel Eliment na uhakika inaeza ikawa imeanza kuchoka driving Shaft zake lkn ukafkiri ni wheelbearing
Na dalili za kuanza kuchoka kwa driving shaft pale ukianza kukata kona kali unaanza kuskia kelele hapo ujue tayari shaft hoi
 
kuna jamaa yangu alikuwa na gari rav4 ina engene ya D4 ilimzingua akaamua kubadili na kuweka engene ya 3S, gari imekataa kukaa silance tatizo linaweza kuwa nini na afanyeje manake hiyo gari hata kuuzika imegoma.

Alipobadili hio injini na akaweka ya 3S ilioaswa abadili na CONTROL BOX yake
Control Box ya injin D4 ni tofaut saana na za injin ya 3s na 4S
Injin aina ya 3s na 4s hua mara nyingi ni za gari aina ya Corolla Cresta MarkII
Sasa hapo inakuonesha uhalisia wa tafaut na injin ya D4
Kwa ushauri mwingine kabla hujachkua uamuzi wa kubadili Control Box
Ipeleke kwa mtaalam mwenye DIOGNOSTIC MACHINE
HApo utagundua tatizo fasta
 
Mkuu kwa ushauri nunua injini ya suzuki. SJ14 na gear box yake ibandike humo ktk hio pajero utasahau mkuu na wala haihitaji madifkeshen makubwa kivile tofaut ya kuzisogeza engine mounting na geabox mounting pia na kukata propela
Engine za pajeri GDI zinasumbua saana yaani ktk mitubishi hapo ndo mjapan alichapia ktk hizo injin
Inauzwaje kiongozi

Sent from my TV
 
Msaada wenu gari timing belt ilikatika nikaivuta mpaka mjini sasa nimebadili hiyo timing belt gari imewaka ina misi ya hatari kabisa sasa hawa mafundi wananiambia itakuwa imeharibu vitu vingi sana kwenye engine maana ilipo nizimikia nilijaribu kuiwasha sasa fundi anasema ndio nilifanya makosa hapo sasa amenitajia vitu vingi Mimi sio fundi sivijui ghalama yake anasema inafika 500000 na gari ni cresta gx100 vvti
Wakuu nina swali hapa. Hivi hakuna namna ya kujua kama timing belt inakaribia kukatika au kama inahitaji kubadilishwa?

Kwa nini timing belt ikatike gafla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu nina swali hapa. Hivi hakuna namna ya kujua kama timing belt inakaribia kukatika au kama inahitaji kubadilishwa?

Kwa nini timing belt ikatike gafla?

Sent using Jamii Forums mobile app
Timing belt wakati mwingine naona kama kuna ujinga mjapan alifanya! Hasa ukiangalia suala la kutaka kupunguza uzito kwenye engine. Timing belt kwa macho utaiangalia utaona mpyaaaaaaa! Ila siku mbili mbele inakatika. Bora angebakia na Timing Chain tu mtu unasahau.
Kwa hilo mie naona ungoje tu zamu yako ifike.
Kuna mtu ana Toyota Noah ya Engine 3S, katoka kufanya service kubwa baada ya safari ya mkoa. Kucheki Timing belt imeonekana haina hata ufa mmoja. Ndani ya hiyo wiki imemkatia akipanda kile kilima cha round about ya Mbagala kwenda Mbagala kuu
 
Timing belt ikichoka kwenye dashboard inatoa maandishi T-belt hapo ujue muda wowote inakatika
Sawa mkuu. Nitajuaje kama taa ya timing belt ni nzima? Mfano kama hiyo taa ilisha haribika ina maana haiwezekani kujua kama timing belt inahitaji kubadilishwa!!

Hasa kwa gari ambalo umenunua kwa mtu na hujui kilomita alizobadilishia timing belt

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu msaada gari ninapiga start inapokea vzr lkn haikai sailensa inazima, sasa juz Kati kumbe wife kaipeleka car wash wakaosha Na engine lkn nilipomtafuta aliyeosha akasema maji hayakufika kwenye plug si mgen wa kuosha engine tatizo laweza kuwa nn wakuu
 
Timing belt light imesetiwa automatically kuwaka ile odometer ikifika kilometre 100,000..200,000...300,000 ..etc yaani ina life span ya kutembea kilomita laki moja tu zaidi ya hapo unatafuta majanga ..ukishabadilisha kuna namna fundi anafanya kuizima taa..
Nashukuru mkuu. Sasa sina mashaka. Mie nadili na dashboard yangu tu. Natumai haitanikatikia bila kunionyesha kwenye dashboard.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom