Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,885
MACHACHE HAYA YATAIOKOA SERIKALI NA MACHINGA WAKE.

Anaandika, Robert Heriel

Awamu ya tano ilisitisha Ajira za kila mwaka, ilikuwa awamu ambayo serikali ilipunguza kuajiri Kwa Asilimia kubwa Hali iliyoleta Malalamiko Kwa wasomi waliohitimu vyuoni.

Katika kutatua changamoto hiyo ya Ajira, ndipo wazo la kuruhusu machinga wafanye shughuli zao popote watakapoona panafaa.
Lengo ni kuondoa Yale malalamiko ya kusema hakuna ajira wakati tayari serikali ishafungua mlango mwingine wa kujiajiri ambao ni Machinga.

Miji ikafunikwa, barabara zikafungwa, mitaa ikasongwa, kila Kona machinga, Vijana Kwa Wazee wakajitosha kwenye vibiashara kujipatia kipato, wanawake kwa watoto wakajitokeza huku wasomi wakijivuta vuta kutokana na aibu ya kufanya vibiashara ambavyo waliviona sio hadhi Yao. Hata hivyo walivyoona matumaini ya kuajiriwa yanazidi kufifia wakaona hawana budi kujiunga na machinga. Baadhi wakajiajiri.

Serikali ikaona ilete utambulisho wa machinga Kwa manufaa makuu mawili, moja, serikali ijipatie kipato ambacho waliweka Tsh 20,000 Kwa mwaka. Pili, Wamachinga wawe huru kufanya shughuli zao pasipo na bughuza kwani vitambulisho vitakuwa vinawatambulisha Kama walipa Kodi na moja ya watu wanaochangia pato la nchi. Hilo likafanyika ingawaje halikufanikiwa Kwa Asilimia kubwa kutokana na sababu kadha wa kadha.

Majiji kutekwa na Machinga kuna athari zake, athari nyingi ni Hasi, lakini hatuwezi kuipuuza Athari chanya moja itokanayo na Machinga; nayo ni Kutoa fursa Kwa vijana na watu Kwa ujumla kujiajiri. Watu walijipatia kipato na kulisha familia zao, kuendesha maisha yao na hata wengine kusomesha kupitia Machinga.

Hata hivyo hatuwezi kufumbia macho athari mbaya za Machinga kuyateka majiji hapa nchi, athari hizo ni pamoja na uvunjaji sheria za mipango miji ambapo hupelekea matumizi mabaya ya miundombinu Kama barabara Hali iñayopelekea athari nyingi kama Ajali za barabarani Kwa watembea Kwa miguu, msongamano Kwa wapita njia na watumia vyombo vya Moto Hali iñayopelekea shughuli za kiuchumi kudorora kutokana watu kutumia muda mrefu njiani kutokana na msongamano, Kwa mfano pale Kariakoo, sehemu ambayo ungepaswa utumie dakika moja kutembea kutokana na Machinga kutandaza bidhaa zao hovyo hovyo itakupasa utumie dakika tatu mpaka tano.

Pia usalama ni mdogo kwani watu huibiwa, na kutapeliwa na sio rahisi kupata wa kumkamata kwani Machinga Hana Anuani.

Athari zingine ni serikali kukosa Kodi ya moja Kwa moja kutoka Kwa wafanyabiashra Machinga ambao wengine wanamtaji mzuri tuu wa kulipa Kodi.

Machinga pia wameweza kudororesha biashara za wamiliki wa Fremu za biashara.

Baada ya Magufuli kuaga USO wa Dunia, mambo lazima yangebadilika kwani kiongozi aliyeingia ni mwingine hivyo Mitazamo, Falsafa, muono lazima uwe tofauti.

Awamu hii nafikiri Ajira zitakuwepo, na Hilo limejitokeza hivi karibuni tuu. Sekta binafsi zimeanza kufunguka, serikali ishaanza kuajiri na bila Shaka kuanzia mwakani baadhi ya watumishi wa Umma wataanza kuongezewa mishahara na posho.

Serikali inapoondoa Machinga yapaswa ifikiri vyema namna Bora ya kuwaajiri au kuwatengenezea mazingira rafiki ya wao kujiajiri.

Machinga hutafuta Maeneo yenye watu wengi ambayo watauza bidhaa zao.

Serikali yapaswa kutathmini ni Maeneo gani ambayo yanapendwa na watu au ni rahisi kufikika ambayo Machinga wakiweka biashara zao watajipatia kipato.
Sio iwafukuze na kuwaelekeza Maeneo ambayo watu/wateja hawawezi kufika huko.

NINI SERIKALI IFANYE KUWASAIDIA WANANCHI WAKE AMBAO NI MACHINGA?

1. Serikali itenge Maeneo rafiki Kwa Machinga kufanyia shughuli zao.
Sio itenge Maeneo ilimradi kuepuka lawama wakati Maeneo hayo hakuna Mzunguko wa watu.
Machinga wengi ni masikini, wanahitaji wapate pesa Kwa siku iwe elfu kumi au tano. Kumpeleka Machinga sehemu isiyoeleweka ni kuchochea chuki Yao na serikali.

Eneo Kama Karume ni zuri na ambalo Machinga wengi hujipatia kipato.

2. Ziundwe propaganda, matamasha ya ku-promoti Maeneo mapya na yazamani ambayo Machinga hufanya shughuli zao.

Serikali baada ya kuwapeleka na kuwahamisha Machinga Maeneo Yao rafiki Kwa wateja wao, hatua inayofuata ni kuunda Propaganda Kwa kutumia mbinu anuwai Kama vile kutumia Watu wenye majina makubwa iwe ni viongozi WA serikalini, viongozi wa dini, Wasanii wakubwa au watu mashuhuri ku-promoti Maeneo hayo. Kupitia media propaganda hizo zilenge kutangaza na kutukuza Maeneo hayo ili kufanya watu wahamasike kwenda kujipatia bidhaa huko.

Machinga nao wasifikirie mambo ya bure bure kama wapumbavu, wajisajili kwenye Vyama vya Wamachinga Kwa kila soko, walipe Ada kila mwezi kulingana na watakavyopanga katika vikao/mikutano Yao, Ada hiyo itumike katika Kazi zifuatazo; moja, Kutoa vitambulisho, kulipa viongozi wao, kulipia Matangazo Kwa ajili ya kuunda matamasha na propaganda za kutangaza Maeneo Yao ya kazi ili wapate wateja.

Serikali ichukue Kodi kila kiamba anachomiliki Machinga kulingana na ukubwa wa kiamba, Kama ni meza ya kawaida ya futi tano Kwa nne walipe Tsh 20,000 Kwa mwezi, na iongezeke Kwa kadiri ya ukubwa wa eneo.

Viongozi wa MACHINGA watakaochagulia Kwa kila soko wahakikishe kila mwaka pawepo na tamasha kubwa la Machinga ambalo kazi yake kubwa ni kutangaza eneo Lao, na kutoa Ofa Kwa Kupunguza bei za bidhaa zao kuvutia wateja. Siku hiyo wanaweza kuiita "SIKU YA MACHINGA TANZANIA" Wataipa Kauli mbiu. Kisha waitangaze kwenye vyombo vya habari.

Siku hiyo Machinga wote wa eneo husika wawe katika Sare Fulani watakayoipendekeza, Wasanii maarufu waitwe waburudishe, watu mashuhuri waitwe wainogeshe,

Makampuni na mashirika makubwa yapewe udhamini ili nayo yatangaze biashara zao kupitia siku hiyo.

Eneo liajiri walinzi na wafanya Usafi kufanya eneo la soko liwe salama na Safi muda wote.

3. Serikali ijenge vibanda vya kisasa pembezoni mwa barabara baada ya barabara za wapita Kwa miguu.
Hii isiwe katika katikati ya mji, inaweza kuwa nje kidogo ya mji mathalani kuanzia Kimara mpaka Mbezi, au Kwa Azizi Ally, mtoni mtongani kuelekea Mbagala, Mbezi shule, GoiG kuelekea Tegeta Bunju, Riverside, Epz kuelekea Tabata n.k.

Serikali Kama itashindwa inaweza kutoa tenda Kwa makampuni au mashirika binafsi yajenge Vibanda vya kisasa pembezoni mwa barabara mara baada ya barabara ya wapita Kwa miguu. Vibanda hivyo visijengwe Kwa gharama kubwa, viwe potable vinavyoweza kuhamishika.
Wakodishiwe Machinga ambao hupenda kukaa pembezoni mwa barabara wapitapo watu. Walipishwe Kodi kulingana na eneo husika, serikali ichukue Kodi Kwa mwekezaji, mwekezaji achukue pesa Kwa Machinga, wanaweza kukodisha Kwa mwezi katika ya Tsh 30,000 mpaka 70,000 kulingana na potentialities ya eneo husika.

Wasajiliwe ili mambo yaende Kwa kiutaratibu.

4. Machinga wapewe mikopo kulingana na Hali zao.
Machinga aliyejisajili katika chama cha Wamachinga, akadumu katika chama hicho Kwa zaidi ya miaka miwili mitatu. Apewe ruhusa ya kukopa, serikali pamoja na makampuni ya mambo ya Fedha yaweke utaratibu maalumu wa kuwakopesha Machinga ili kukuza mitaji Yao na kuendesha biashara zao.

Mdhamini Mkuu wa Machinga mbali na vigezo vingine atakuwa ni chama cha Machinga ambacho kitakuwa chini ya serikali kwani watakuwa wanalipa Kodi.
Hii itachochea biashara za Machinga kukua na uchumi wao kupaa, nchi nayo itakuwa imejipatia kipato.

5. Serikali itambue na kuweka utaratibu wa madalali wa bidhaa.
Moja ya sekta nyeti katika majiji makubwa Duniani ni Sekta ya madalali (Brokers). Serikali iandae mpango mkakati WA namna ya kuwatambua na kuwa-promoti Madalali wa bidhaa. Wafanyabiashra wakubwa na wadogo, na wakulima wanajua nguvu ya madalali katika Kazi zao.

Serikali lazima nayo itambue nguvu hiyo na ijue namna ya kuwafanya wachangie pato la nchi.
Dalali ndiye kiungo wa muhimu katika biashara nyingi katika majiji makubwa. Hata serikalini wapo viongozi ambao ni madalali.
Pasipo wao huwezi pata kitu ukitakacho, au pasipo wao huwezi uza bidhaa yako hata iwe Bora vipi.

Madalali na Machinga wanaingiliana Kwa sehemu kubwa, kwani Machinga naye ni sehemu tuu ya dalali anayedalalia bidhaa ya mfanyabiashara Mkubwa.

Serikali iwasajili, serikali haipaswi kutumia nguvu kujipatia kipato Bali yapaswa kuweka utaratibu mzuri utakaowasaidia wananchi kujipatia riziki zao na serikali kujipatia Kodi.

Hayo ndiyo machache Kwa Leo.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
nadahni umetowa mawazo mazuri,ila kuwapangisha sh elf 20 hadi 70 kwa mwezi huyo siyo machinga tena ..na serikali yetu kwa kuwa haifikilio inaweza kweli kuanza kiwapiga machinga haera kubwa kubwa badala ya kuanza labda na kuchangia sh elf 10_20 kila mwezi..hapo wanaweza tengenza pesa kubwa
 
Back
Top Bottom