Rais Samia awapa Machinga kiwanja na milioni 10 kujenga ofisi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,145
Rais Samia ametoa tsh Milioni 10 kwa Wamachinga kwa ajili ya Kujenga ofisi zao

Katibu mkuu wa Shirikisho la Wamachinga mh Venatus Magayane amesema Rais Samia ametoa Kiwanja chenye hati na tsh Milioni 10 kwa mikoa yote yenye Wafanyabiashara wa aina hiyo

Magayane amesema hayo wakati akikabidhi fedha hizo kwa Wamachinga wa Kahama mkoani Shinyanga.
---

1687374938879.png

Shirikisho la Umoja wa Machinga wilayani Kahama mkoani Shinyanga limekabidhiwa kiwanja chenye hatimiliki pamoja na TZS milioni 10 ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa ofisi yao.

Akizungumza Katibu Mkuu wa shirika hilo, Venatus Magayane amesema kila Mkoa wenye wafanyabiashara hao, Rais Samia amewapa TZS milioni 10 na kiwanja chenye hatimiliki kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, hivyo baada ya ujenzi kukamilika machinga watakuwa na nafasi ya kukopesheka na tassisi za kifedha tofauti na hapo awali.

Amesema kwa sasa wameridhishwa na lengo la Serikali chini ya Rais Samia katika kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira rafiki.

Mmoja wa Machinga, Agnes Magoli amesema mara ofisi zitakapokamilika zitawasaidia kuwa wafanyabiashara wakubwa ambao watakuwa wakichangia kodi Serikalini kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Aidha, kwa kuunga mkono jitihada za Rais Samia kwa Machinga hao, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita amewaongezea TZS milioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi hiyo.

Source: Swahili Times
 
cheap politics, himsaidii!Tunataka bandari zetu. Mwanamke ni mwanamke kumbe, nilkuwa nawatetea sana. Urais kwa mwanamke hapana
 
Hii movie Haina Tija Kwa sababu wanakula hizo hela ni hao wanaojiita viongozi wa machinga ila machinga wenyewe hawapati kitu..

Kama Rais anataka kuwasaidia machinga awaelekeze TanRoads au Watu wa Majiji wanapojenga Barabara au Stand zao watoe fursa Kwa miundombinu rafiki Kwa kaiz za Machinga..

Pia wawajengee masoko kama lile la Dodoma maeneo Yale Yale yenye watu wengi.
 
Rais Samia ametoa tsh Milioni 10 kwa Wamachinga kwa ajili ya Kujenga ofisi zao

Katibu mkuu wa Shirikisho la Wamachinga mh Venatus Magayane amesema Rais Samia ametoa Kiwanja chenye hati na tsh Milioni 10 kwa mikoa yote yenye Wafanyabiashara wa aina hiyo

Magayane amesema hayo wakati akikabidhi fedha hizo kwa Wamachinga wa Kahama mkoani Shinyanga

Source: Swahili Times
This is cheap politics. Please Mama do clarify deeply about that zombie DP World which haunts your government.
 
Hii movie Haina Tija Kwa sababu wanakula hizo hela ni hao wanaojiita viongozi wa machinga ila machinga wenyewe hawapati kitu..

Kama Rais anataka kuwasaidia machinga awaelekeze TanRoads au Watu wa Majiji wanapojenga Barabara au Stand zao watoe fursa Kwa miundombinu rafiki Kwa kaiz za Machinga..

Pia wawajengee masoko kama lile la Dodoma maeneo Yale Yale yenye watu wengi.
Sielewi leo imekuwaje umetumia kichwa kufikiri!

Kwanza sikuamini kuwa ni wewe uliyeandika haya, hadi nilipotazama mwandishi ni nani.
 
Back
Top Bottom